CABINET: JK awaacha Messi, Drogba, Rooney bench na kuwapanga kina Adebayor | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CABINET: JK awaacha Messi, Drogba, Rooney bench na kuwapanga kina Adebayor

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fareed, May 18, 2010.

 1. F

  Fareed JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Rais anapoteuwa baraza la mawaziri huwa kuna considerations nyingi anafikiria, kama vile sifa za mteuliwa na pia hujaribu ku-strike a balance kwenye cabinet kwenye misingi ya ukabila, dini, maeneo ya nchi ambayo mawaziri wanatokea, umri, muungano, gender na mengineyo. Muhimu zaidi, Rais huwa na hulka ya kuwapa uwaziri watu ambao anaona ni wa kambi yake na wamemsaidia kupata Urais au tu maswahiba wake kwa ujumla. Kwa tathmini yangu ya haraka, iwapo Rais Kikwete angekuwa makini kwenye uteuzi wa mawaziri katika wizara 5 tu nyeti tangu alipoingia madarakani mwaka 2005, Tanzania sasa hivi ingekuwa mbali sana kimaendeleo na umasikini usingezidi kushamiri kama ilivyokuwa sasa. Ingawa kila wizara ina umuhimu wake kwenye kuleta maendeleo, lakini kwa mtazamo wangu wizara 5 zifuatazo ndiyo muhimu zaidi kwa mazingira ya sasa ya Tanzania.

  1. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
  2. WAZIRI WA NISHATI NA MADINI
  3. WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA
  4. WAZIRI WA MIUNDOMBINU
  5. WAZIRI WA FEDHA

  Utalii ndiyo unaongoza kwa pato la taifa nchini, lakini bado sekta hii iko duni sana. Serikali imeshindwa kuutangaza utalii wetu aggressively na kusimamia ukusanyaji wa mapato. Bado Kenya inafaidika zaidi na Mlima Kilimanjaro na utalii wa Tanzania. Wakati Tanzania imeshindwa kufikia target ya kupata watalii milioni 1 tu kwa mwaka, Afrika Kusini kabla ya World Cup inapata watalii milioni 8 kwa mwaka!

  Kuna uozo mwingi kwenye sekta madini ambao wote tunajua. Dhahabu yenye thamani ya mabilioni ya dola za Marekani huuzwa kila mwaka na wageni huku nchi ikiambulia punje tu. Haileti maana kuona kuwa pamoja na utajiri wote huu, sekta ya madini haiongozi kwenye kuipatia nchi mapato. Kilimo na Miundombinu bado iko duni sana. Pia wizara ya fedha imeshindwa kusimamia vyema ukusanyaji na matumizi ya mapato ya nchi na kubuni sera sahihi za maendeleo.

  Ukiangalia mawaziri wanaoshikilia nafasi hizi kwa sasa, wote wameshindwa kazi zao. Wako tu kwenye wizara hizi aidha kwa kuwa Rais ni swahiba wao au ameshindwa kutambua unyeti wa wizara hizi.

  There are a lot of mismatches and misallocation of human resources in Kikwete's Cabinet. Mfano mchapa kazi kama John Pombe Magufuli angepewa Wizara ya Maliasili na Utalii angepaisha utalii wa Tanzania na kutimua wezi wote wa meno ya tembo, tourist hunting na misitu within just a year. Au angepewa Wizara ya Kilimo tungeona jinsi kilimo kwanza kinapamba moto. Kwa ufupi, Kikwete is his own worst enemy.

  Matatizo yaliyopo ya umasikini na maendeleo duni ni ya kujitakia mwenyewe. Anachofanya JK kwenye Cabinet yake ni kama kocha wa timu ya mpira ambaye ana kina Messi, Torres, Drogba, Rooney, Tevez kwenye benchi halafu anawapanga kina Adebayor, Bendtner na Berbatov kwenye safu yake ya ushambuliaji ambayo ndiyo hizo Wizara 5 nyeti!
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Hapangi yeye.

  Hutekeleza maagizo ya waliompa kazi toka.........

  Samahani umeme umekatika.
   
 3. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kama mwaka huu atapita. Hataweza tena kuteua mandondocha
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Msameheni bure
   
Loading...