Cabinet Baada Ya Lowassa: Waziri Mkuu Mpya Atakuwa Nani?

katibu tarafa,

..unatumia vigezo gani?

..he is also clean na hana jazba.

..hukuona walipomletea ripoti mbaya ya uchunguzi, akaitisha uchunguzi mpya?
 
Wabongo wenzangu kwa hili tusifanye masihala, tusishabikie majina kwa uswahiba au asili ya kule tunakotoka. Kutaja jina si kazi, tuambizane na utendaji wa hao proposed candidates wetu kipindi chao bungeni. Baadhi ya majina yaliyotolewa sijasikia wakichangia hata hoja yoyote kwa maendeleo ya nchi. KWA NINI ASIWE MWAKYEMBE au mmoja ya wana kamati au moja ya wale waliokataa kuendelea kusikiliza muswada uliokuwa uwasilishe na Karamagi. Kama hawa wote hawafai kwa nini asiwe mbunge wa CCM DR. --- jasiri wa kuuliza maswali nyeti wakati wengine wakiwa kimya? Hii nafasi siyo karanga hasa baada ya kuwekwa pabaya na viongozi wasio na uadilifu. Napenda kuongezea tu kuwa, profession ya Mwakyembe ktk Sheria na uelewa wa wana Kamti wengine vimekuwa ni mchango mkubwa kwa report yao nzuri kiasi vogogo kujiuzuru. Maana imeandikwa kitaalam. Ni kweli kurecycle viongozi haipendezi wala haifai. Umri si hoja!
 
KWANINI ASIPEWE DITOPILE WAJEMANI?mtu kama mwakyembe hatamsumbua hatakidogo
 
kichuguu,

..Mama Kilango elimu yake ni ndogo kuweza kuwa waziri mkuu ktk zama hizi.

..waziri mkuu ni mtu ambaye most likely atakuja kuwa Raisi wetu.

..Naona safe candidate ktk cabinet ni Prof.David Mwakyusa.

Kama MOI tu imemshinda Mwakyusa je atauweza mfupa wa Tanzania nzima na takataka zake? Ilitakiwa ajiuzulu katika lile suala la MOI ili tuwe na imani naye.
Be serious man!
 
wewe tayari ni kafara "bangusilo"

Too difficult to knwow who will be our next PM, It seem as if CCM i almost divided, and JK will try to pick up a guy who will be abble to unite the party, no body at this time.
 
kichuguu,

..Mama Kilango elimu yake ni ndogo kuweza kuwa waziri mkuu ktk zama hizi.

..waziri mkuu ni mtu ambaye most likely atakuja kuwa Raisi wetu.

..Naona safe candidate ktk cabinet ni Prof.David Mwakyusa.

  1. Nilikuwa sijui undani kuhusu elimu yake, lakini katika timu ya CCM, mimi nadhani kwa Mama Kilango ana uzalendo sana.
  2. Wasomi wengi ndio wameiangausha nchi hii ukianzia na Professor Malima; kwa hiyo swala la elimu kubwa pia ninaliangalia cautiously.
  3. Ikiwa ni lazima, basi ni afadhali turudi tulikotoka ili tuanze kujipanga tena upya; tumwombe sana Salim atusaidie jahazi.
 
Wasiwasi wangu ni fisadi mwingine kuwa Waziri Mkuu huo ndio utabiri wangu. tuvute subira
 
MzalendoHalisi,

..Mwakyusa ni Waziri wa Afya, moja ya wizara kubwa Tanzania. kwa msingi huo Uwaziri Mkuu siyo cheo Kikubwa kitakachomshinda.

..as long as unafuata sheria na muongozo wa kazi yako basi masuala kama upole nk hayana msingi ktk utendaji.

..Lowassa ambaye alikuwa mkali mbona kazi imemshinda.

..nafasi ya waziri mkuu inahitaji mtu mwenye busara, mzalendo, na muadilifu.

Kichuguu,

..waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa toka jimboni.

..tukitaka kumrejesha Salim basi ni lazima kwanza tubadilishe katiba. hilo haliwezekani kwa wakati huu kwasababu hatuna PM na inaelekea Mwanasheria mkuu naye atajiuzulu.

..
 
Labda Hawa Ghasia!!

maana machaguzi ya JK hayatabiriki, pamoja na warning zote kutoka kwa JKN bado ndugu Lowassa alikuwa PM!
 
Labda Hawa Ghasia!!

maana machaguzi ya JK hayatabiriki, pamoja na warning zote kutoka kwa JKN bado ndugu Lowassa alikuwa PM!

Mkuu Steve,
Ina maana umetuchoka namna hiyo wana JF hadi ukampendekeza mama Ghasia? Huyu si ndio karekebisha sheria ya ajira na kufanya wawe "wanajiajiri" wao wenyewe sirikalini bila kuchukua damu mpya?
Hafai huyu!
Pendekeza mwanadada mwingine.
 
Apewe Lawrance Masha

Tupe na mchango wake wenye manufaa kwa mwananchi wa kawaida!!Isije kuwa ni baba ya yule partner wa kampuni ya mawakili binafsi ambao kati ya mambo wanayofanya ni kujiuzia majumba ya mashirika ya umma! kama nimekosea samahani. Halafu imeajiri mtoto wa WATU.
 
JokaKuu,

Mwakyusa kumpa u PM ni kumwonea bure.. yeye ongea yake ni sauti ya chini chini.. na usipokuwa makini unaweza usmsikie! Haziwezi kashkash za uPM! Pia uwaziri alipewa kwa kuwa alikuwa daktari wa Mwal. Niambie hapo Afya -two years sasa ni nini amefanya?

Wassira ni ok- ila kumbuka loyalty yake CCM -he at once defected from CCM!

Salim haiwezekani- Raisi, Mwakamu na Waziri Mkuu wawe Waislamu!

Je ni waziri gani mwadilifu apewe uPM?

JK anataka kuua mtandao- huenda akamrejesha Malecela JS!
 
Natabiri PINDA...huyu ndie alikuwa choice yake JK kabla ya wanamtandao wa CCM kumlazimisha na kumpa EL
 
Back
Top Bottom