C.C.M Haina uhalali wa kuendelea kuwa chama cha siasa, 'Hakijasajiliwa'. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

C.C.M Haina uhalali wa kuendelea kuwa chama cha siasa, 'Hakijasajiliwa'.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtoto Wa Mbale, Apr 14, 2012.

 1. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Msajili wa vyama vya siasa nchini ndg. John Tendwa amekiri kuwa CCM hakina uhalali wa kuwa chama cha siasa kwani hakikusajiliwa kwa mujibu wa sheria. Akizungumza katika kipindi cha kila wiki cha 'This week in Perspective' kinachorushwa na Tbc1, ndg Tendwa alikubali kuwa ccm haikusajiliwa na hivyo inafanya siasa kinyume cha sheria. Hata hivyo alitetea uvunjaji huo wa sheria kwa madai kuwa 'ccm ilikuwepo' kabla ya kuanza kwa vyama vingi mwaka '92 hivyo hapakuwa na haja ya kusajiliwa upya kwa mujibu wa sheria.

  My take:
  Wanasheria fungueni kesi mahakamani kupinga ccm kuendelea kuwa chama cha siasa kwani ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi.
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii ni kali, maana majina ya vyama vilivyokuwepo huko nyuma yalipigwa marufuku kutumika. Sielewi vizuri hii ilikuwa na maana gani?
   
 3. Royals

  Royals JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 1,430
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ai kiti changu nlichokalia nakiona cha moto. Itakuwaje na hawa jamaa walichachamaa sijui itakuwaje au nng'atuke mapema?
   
 4. YanguHaki

  YanguHaki Senior Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki ni kituko cha mwaka! Hoja kwamba CCM ilikuwepo kabla ya sheria ya vyama vya siasa ni upuuzi kwani sheria inataka vyama vyote visajiliwe kuanzia kuwepo kwa sheria hiyo! Tendwa anapotosha umma kwa kauli kwamba hakukuwa na ulazima wa chama kusajiliwa baada ya sheria ya vyama vya siasa kutungwa. Akiri tu CCM imevunja sheria na achukue hatua bila kusita. Huo ndio utawala wa sheria!
   
 5. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,569
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwa mtaji huu inabidi ccm ishitakiwe kwa kujishughulisha na siasa wakati si chama cha siasa, magari ya zamani yalisajili
   
 6. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hilo nalo neno!
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,572
  Likes Received: 18,349
  Trophy Points: 280
  Bahati mbaya sikubahatika kumsikia Tendwa, ila kiukweli, mhe. Tendwa ni mmoja wa vilaza wakubwa sana kwenye siasa za Tanzania ambaye kazi yake kubwa ni kupiga kelele tuu kama debe tupu!.

  Sii kweli kuwa CCM haikusajiliwa, ukweli ni kuwa CCM ilisajiliwa na kupatiwa certificate namber moja ila kitua mbacho CCM haikufanyiwa, haikupewa intern registration, wala kuhakikiwa na kupatiwa usajili wa kudumu, bali kilipatiwa usajili wa kudumu bila kuhakikiwa kwa hoja kuwa maadamu CCM ndio kilikuwa chama tawala, hivyo kimekidhi vigezo outright!.

  Kitu ambacho sio halali kwa CCM, ni kitendo cha kuendelea kuhodhi rasilimali za Watanzania waliochangishwa kwa nguvu enzi za chama kimoja au walizomilikishwa na serikali enzi hizo. Umiliki wa mali nyingi za CCM sio halali na wanasheria makini wanaweza kulisimamia hili haki ikatendeka.

  Baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi, CCM imeanza na mtaji mkubwa wa wanachama, hivyo kilitakiwa kurejesha serikalini mali zote kilizozipata kiserikali na kingeruhusiwa kuziretain zile mali za Tanu ambazo zimetokana na michango ya wanachama, ili vyama vyote vianze moja na kuleta ushindani wa haki!.

  Mpaka sasa, mtaji mkubwa wa CCM ni ruzuku ya hazina inayojivunia kila mwezi kutokana na kuongoza kwa idadi ya wabunge. CCM imekuwa ikichaguliwa kwa mazoea sio kwa sababu inapendwa sana!. Sasa Watanzania wameanza kuamka hivyo 2015 sio tuu inaweza kupoteza mtaji wake mkubwa wa ruzuku, inaweza kupigwa chini jumla, kama Spirit ya Chadema kule Arumeru itasambazwa nchi nzima, there will be no way out 2015 CCM ni chali, na ndipo wanasheria watatinga mahakamani kuipokonya rasmi mali ilizikwapua na to mark the sad end of CCM!.
   
 8. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mhhh kazi ipo!
   
 9. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Sasa hapa sijui majaji wataamua vipi. sijui nani anakwenda mahakamani au Tumwachie Rev Mtikila?
   
 10. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  CCM haija wahi kutimiza sheria hata sikumoja labda kabla sijazaliwa....
   
 11. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  sasa kwanini asiwaambie wajisajili?mbona usajili wa simu ulikuja baada ya watu kuwa na line na wata wanakimbia sajili.
   
 12. p

  plawala JF-Expert Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo Tendwa naye ni kada wa CCM na hicho cheo kapewa na raisi anayetokana na CCM,hiyo tu inatosha yeye kutowachukulia hatua akihofia mustakabali wa kibarua chake
   
 13. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Huwa wana switch side ghafla
   
 14. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimependa mchango wako, umejenga hoja vizuri sana. Nilihisi kama si yule 'Pasco' wa kila siku. Big up kamanda.

  Bado ukweli unabaki pale pale, ccm haikukidhi matakwa ya sheria ya vyama vya siasa. Katika nchi ya kidemokrasia na utawala wa sheria, hakuna aliye juu ya sheria. Kazi ya msajili wa vyama ni kuhakikisha kuwa sheria inafuatwa. Huu ni wakati wa Tendwa kuwajibika.
   
 15. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pasco katika michango yako mizuri huu nao unaweza kuuweka katika kumbu kumbu zako. Ni log kwa PC natafuta post hii nakupa like.
   
 16. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,696
  Likes Received: 17,751
  Trophy Points: 280
  Wajumbe hata computer/phones zenu zinaonyesha haya maandiko ya Pasco, au ni yangu tu? Bila shaka amezaliwa upya, tumuunge mkono
   
 17. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,916
  Likes Received: 2,341
  Trophy Points: 280
  We mtoto , ni rahisi kumpeleka mahakamani baba yako kwa kukuzaa kuliko kuipeleka CCM mahakamani.
   
 18. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  waliogopa kukisajili kwa hofu ya kupoteza majengo na mali zingine nyingi ?
   
 19. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,930
  Likes Received: 1,462
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani huwa mnashindwa tu kumwelewa Pasco,huwa anasimamia anachokiamini bila kujali itikadi za chama.
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hapa kuna utata mkubwa sana, hivi si niliwahi kusikia kuwa CCM ilikabidhiwa hati ya usajili No.1? na ndiyo source ya wimbo wao wa 'nambari wani'. 'Jaji' Liundi ndiyo msajili wa kwanza atafutwe ajibu hili, huenda Tendwa hajaliona file la usajili.

  Lakini sishangai kwa kauli hizi za Tendwa huenda ni mbinu ya kubadili jina la Chama kutoka CCM na kuwa jina jingine 'Rebranding' ili kuwasahaulisha wananchi na montrosity of the so called 'CCM', .
   
Loading...