Bye bye DSTV! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bye bye DSTV!

Discussion in 'Sports' started by Ibrah, Jul 19, 2010.

 1. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #1
  Jul 19, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mlitutesa sana
  Mlituumiza sana
  Mlitutenga sana
  Bye-bye DStv!

  Mliringa sana
  Mkaongeza matabaka
  Ya walala hai
  Na walala hoi
  Bye-bye DStv

  Bei yenu ilikuwa ghali
  Kwa watu wa ghali
  Mara dola sabini
  Mara dola sitini
  Bye-bye DStv


  Leo nimekutana na tangazo la DStv katika kituo cha daladala hapa Arusha, sikuamini macho yangu. Ilibidi nisogee karibu na kuanza kulisoma kwa makini. NAdhani baadhi ya watu walinishangaa. Tangazo hilo lilinifanya nije na utenzi huo Byebye DStv!

  Ati DStv sasa wamekuja na punguzo kwa wateja wao! Unapata channeli zisizopungua 25 kwa malipo ya shilingi 13,500/- kwa mwezi (vi9gezo na masharti yao kuzingatiwa!) Chaneli nyingi kati ya hizo 25 zinapatikana katika king'amuzi cha TBC; kuna TBN, TBC, Citizen, Trace, BeT nk. Chaneli za nyongeza ni ESPN, KBC, Gospel na Muslim.

  Ilinikumbusha miaka ya ukiritimba na wizi waliotufanyia DStv kabla ya TBC kuja na ving'amuzi vya kichina-china. Walijipangia bei za ajabu-USD 60-70! Leo DStv wenyewe wamekubali yaishe. NAdhani watabaki wakiringia Super sports pekee ambayo ndo itawafanya wale wa madaraja ya juu kutupiga bao hapo lakini ikiwa TBC watalipia mechi zaidi za Premier League mwezi August ni wazi ngoma itakuwa droo.

  Kwetu sisi wengineo ambao tuliwachukia DStv kwa ukiritimba na ubaguzi wao wa bei zao za kuruka, lau tumepata mahali pa nafuu kidogo.

  NAkumbuka miaka ile ya kati ya 1990, DTV walikwa wakituonyesha mechi nyingi tu za Premier League kabla ya kuja hao DStv na kudai wao ndo wenye haki pekee ya kurusha mechi hizo Tanzania.

  Hongera TBC,angalau kukomesha urasimu na majivuno ya DStv.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jul 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  TBC2 bado hawajaeneza huduma nchini kote, kwa hiyo bado maumivu yapo kwa ambao hawaishi Dar, Dodoma, Mwanza na Arusha!
   
 3. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Still bado ntaendelea na DSTV,kama mdau wa michezo sijaona chanel ya maana kwenye hivyo vingamuzi vya Wachina
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,830
  Likes Received: 10,142
  Trophy Points: 280
  Hata kidogo ni dawa
   
 5. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #5
  Jul 20, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  TBC kaza buti(hata kama Business partner wako ni mchina)... endeleza ushindani..Mwanzo daima mgumu!!! Binafsi naona ni bora nilipe huduma ya king'amuzi kwa huduma za TBC (nichangie maendeleo ya habari TZ) kuliko kwa hawa wageni ...DSTV watasalimu amri kwani nao wananunua haki za kutangaza vipindi vyao kama wengine..!!
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145


  Ni kweli itachukua muda lakini ikiwa kama TBC wataendelea na kasi hii, naamini ifikapo mwakani nchi nzima yaweza kuwa imefikiwa.


  Hata wao DStv mamejua hilo ndo maana katika hizo channels 25 Supersports hazimo, lakini ikiwa TBC watang'amua hizo channels za michezo, DStv watasalimu amri. Ni suala la wakati tu hata ninyi loyal customers mtawakimbia.
   
 7. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ingawa DSTV wana bei za juu, ukweli upo pale pale events kubwa za michezo duniani, narudia events kubwa za michezo duniani unazipata sehemu moja kutoka kwao.

  Wale wapenzi wa Formula One, Athletics (IAAF Diamond League), Tour de France, Golf Majors, SBK, MotoGP, NBA, Tennis Majors + Ligi zote kubwa za soka duniani wataelewa nini nasema. Hii ni bila kusahau CNN, BBC, Sky, Euro News kwa upande wa habari.

  Ni vigumu kupata-(kwa Afrika) Cable subscriber wa kukupa Sports events kama hizi kwa pamoja.

  Kitu bora siku zote ni ghali.
   
 8. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #8
  Jul 20, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  dstv ni mwisho wa matatizo!
  HAILINGANISHWI KABISA
   
 9. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #9
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Daah, Ibrah aliingia kwa kishindo kuiponda DSTV, naona wengi wamemkata maini kwa kuwa against na mtazamo wake. Hapa bila channel inayofanya coverage ya sports kwa wingi, sidhani kama watu watakuelewa, ukizingatia maisha yenyewe magumu na mahali pa kujifariji ni kwenye sports !
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jul 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hata huko ambako TBC2 haiko, DSTV haiko pia au ni watu wachache sana wenye uwezo wa kulipia hayo ma-DSTV
   
 11. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #11
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mkuu, inategemea nini hasa unachokihitaji. SIku nyingi sana nimekuwa siwapendi hawa DStv kwa kuwa ghrama zao ni juu mno. Naamini kabisa TBC wataweza kutupatia Sports channels kwa bei nafuu kuliko DStv, si unakumbuka GTv? Mbona waliweza kutupatia channels nyingi tu za michezo kwa gharama nafuu kuliko DStv?

  Mimi kwa sasa angalau natosheka na thamani ninayolipia king'amuzi cha TBC. Premier League inaanza mwezi ujao naamini tutaona mechi nyingi zaidi za Premier League kuliko mwaka jana maana uwezo wa kifedha wa TBC kununua haki za kupokea na kurusha mechi za Premier utakuwa umeongezeka.
   
 12. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #12
  Jul 20, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ibrah, channel pekee zilizokuwa zinauza GTV decoders ni zile za English Premier League, lakini zaidi ya hapo hawakuwa na michezo mingine kama ilivyo DSTV na ndiyo maana walionekana nafuu. Ni kwa sababu wao waliangalia tu EPL, with time kama wangetafuta rights za michezo mingine kama DSTV wasingecheza mbali katika subscription fee.

  Ndiyo maana nasema Kitu Bora ni Ghali.
   
 13. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #13
  Jul 20, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  haaaaaaaaaaaaaa bravoooooooooooo chanel ten,itv na tv tumaini ni ivyo ndo ninavyoweza ku acces
  ma dstv sjui manini sjui :fish2: ya kichna tbc ni kitendawili kwangu!!!!!!!!!!!

  aya nyie maclassic jadilini mambo yenu mi simo kwenye class i
  hongereni
   
 14. C

  Chap Member

  #14
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkosoaji nayo hayo maneno ya uhakikaaa
   
 15. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #15
  Jul 20, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Ukweli ni kuwa ni vigumu sana ku-access michezo yote na haiwezekani kushuhudia michezo yote at a time. Tukipata hiyo EPL inatutosha kabisa, so TBC wakipata haki ya EPL kwa mechi zote utashuhudia anguko kubwa sana la wateja kwa upande wa DStv na ndo maana wamefikia hatua ya kuchaji Tsh. 13,500/- , siku TBC wakipata haki ya EPL hao DStv watafika hata kuchaji kama TBC- ni suala la muda tu!
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jul 20, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Lakini bado DSTV wanacoverage kubwa inapokuja suala la michezo! Kwa sisi wapenzi wa ligi ya Italia bado TBC haijatusaidia sana, labda kwenu mnaopendelea ligi ya kwa malkia!
   
 17. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #17
  Jul 20, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mkuu Ibrah:

  Bila TBC(1 or 2) kuwa na "Sports Channels" bado DSTv wataendelea "kula vichwa": Kwa ujumla "audience" ipo interested na:

  1. Sports
  2. Drama/Movies
  3. Others

  DSTv bado wanaongoza kwa item(s) 1 and 2.
   
 18. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #18
  Jul 20, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi nalipia DsTV kwa sababu kubwa moja: EPL, kama TBC au mwingine atapata rights za kurusha angalau 90% ya michezo ya EPL nitahama DsTV. Tatizo ni kwamba hawadumu, walikuja GTV tukanunua ving'amuzi wakatutoroka bila hata kuaga lakini DsTV, mwe kila siku wapo ili mradi umelipia.
  Kila kizuri kina gharama
   
 19. Belo

  Belo JF-Expert Member

  #19
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 11, 2007
  Messages: 11,281
  Likes Received: 4,286
  Trophy Points: 280
  Ibrah ninachofahamu ni kuwa tangu siku nyingi DSTV walikuwa na package za aina 3,but premium ndio ina chanel nyingi na bei yake ni kubwa.TBC walianza kwa mbembwe wakasema wanaonesha La Liga at the end wakaonyesha mechi hata 20 hazifiki,wakaja tena wataonyesha Premier league wakaishia kuonyesha game za Sunderland VS Newcastle,Hull VS Blackburn.
  GTV walitoza bei ndogo lakini wako wapi sasa
   
 20. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #20
  Jul 20, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naungana na wewe baba enock,mbali na ughali wao,hawa jamaa is the best!!

   
Loading...