bye bye 2008...!

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,753
7,844
...kwaheri 2008 :(

if i could change back the hands of time,...

ningetumia muda kuwa karibu zaidi na rafiki yangu aliotangulia mbele ya haki...

wewe je?
 
attachment.php
 

Attachments

  • Friends-kingdom_04.jpg
    Friends-kingdom_04.jpg
    38.5 KB · Views: 103
TATHMINI MWAKA MPYA 1430 HIJRIAH


Mwaka mpya umeingia
Moja Nne Tatu Sifuri Hijriah
Waumini Yatupasa Kuzingatia
Nguzo za Uislamu Nitakutajia!


Shahada ni Egemeo la Kuanzia
Kisha Swala na Zakati Kufuatia
Swaumu ya Ramadhani Inapotujia
Mwezi Mmoja Kufunga Imefaradhia!


Nayo Hijja Faradhi mara moja pia
Kwa Muislamu mwenye uwezo na nia
Uwezo Kiafya na Pesa za Kusafiria
Na Familia Mahitaji Tosha Kuwaachia!


Makkah kwanza na Minah Kuhirimia
Arafah na Muzdalifah nazo Kupitia
Jamaraat Shetani Mawe Kumtupia
Nae Mnyama Kuchinja Hijja Kumalizia!


Muharram Mwezi Mosi Ikiwadia
Tukae Misikitini Vikundi kufikiria
Mwaka Jana Mambo gani Tuliazimia
Tuchuje mafanikio na Yale Yaliyosalia!


Hijriah Mjo Wake Unakumbushia
Kurejea Madhambi Tuliyotenda Kutorudia
Kwa Dhati ya Moyo Ima Kutubia
Ibilisi Mwaka Mpya budi Kumkimbia!


Maendeleo ya Uislamu Mikakati Kuipangia
Awali ni ELIMU ya Dini na Dunia
Vyuo Vikuu Watoto Fursa Kuzitumia
Ummah wetu Kunufaika Wakihitimia!


Turatibu Taaluma kwa Zote Jinsia
Kilimo na Mali Asili Kuvikazania
Mazao ya Biashara Viwe Ndio Njia
Ya Waislamu Maendeleo Kuwafikia!


Ya-Rabi Tunakuomba Kutujaalia
Tuendako Tuweze Maisha Kupalilia
Tushikamane TAQ’Wa Peponi Kujitayarishia
Waja Wako Dua Maridhawa Takabalia!

A A M I I N! A A M I I N!!


___________________________________
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom