Bwawa lenye tope halimtoi kambare msafi

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Mwaka 2005 aliyechaguliwa kuiongoza nchi mwanzoni kabisa kabisa alionyesha matumaini ya ukombozi wa watanzania maskini hadi watu wakamfananisha na yule aliyepigania uhuru.

Tukajisahau kabisa kwamba huyo aliopolewa kutoka bwawani na kilichomng'arisha ilikuwa ni maji aliyosafishiwa baada ya kuvuliwa lakini ule utelezi wa kukaa miaka mingi bwawani alikuwa bado anao.

Tukaendelea kujipa matumaini na alipokaribia kuponyoka kutoka kwenye dira tuliyoitarajia, sisi tulipiga mayowe eti si yeye bali ni wasaidizi wake ndo sio waaminifu.

Tukampa matumaini yetu tena, lakini kilichotokea hata ndani hakutaka kukaa.

Kutwa nzima yuko kwa jirani anakula stori tu kana kwamba hakuna majukumu nyumbani hadi usiku wa manane ndio anarudi nyumbani na anakuta watoto hawajalala wanasubiri baba arudi na chochote kiwaondolee umaskini lakini wapi!!!

Akijitahidi anarudi na rafiki zake wanaokuja kutuongezea umaskini na kuwatajirisha maswahiba wachache wa baba.

Sisi watoto walaaaaa!!!! Hana mpango. 2015 juzi juzi tu, akavuliwa kambare Mkubwa tena mbabe kweli kweli. Akaonyesha kuwa yeye hatishwi na lolote katika kuwapigania walalahoi.

Akaja kwa kasi kabisa ya kuanza na wale waliopenda kufanya watakayo wao, kuishi maisha wayatakayo, kujilipa watakavyo wao bila kujali wamefanya nini na wengine wanabaki na nini.

Kila kona watu wakapiga vigelegele kuwa kambare tuliyemsubiri kwa miaka mingi si ndo huyo bwana!!!!! Fyuuuuuu!!!!

Wakasahau kwamba alivyotoka bwawani tu, alisahau jambo moja la msingi, kuosha matope aliyotoka nayo bwawani na utelezi wote uishe halafu aepuke kugusana na wale anaowatoa bwawani moja kwa moja kwani utelezi na matope ni rahisi sana kumrudia!

Sasa angalia bungeni, team yake inasubiri kuambiwa nyuma geuka mbele tembea. Wanaogopa kuweka ujuzi wao wasijeambiwa wameharibu wakaharibiwa taswira kwamba na wao wanamajipu, Wanaogopa kutoa ushauri wao wasijeambiwa wao ni viherere, Wanaogopa kutumia utaalam wao wasije ambiwa wao ni vilaza.

Yaani huyu yeye anasema alitakalo, anafanya lililoko kichwani mwake kiasi kwamba hata yule anayemuandikiaga yakuongea Sina hakika kama bado anamkataba.

Namshauri tu huyu bwana, kwasababu bado asubuhi, atafute sabuni aondoe utelezi kwenye ngozi yake kabla ya kwenda kwa wengine, halafu achukue kalam na karatasi aandike yale yote ya muhimu anayopenda kuanza nayo, ayapeleke kwa wataalam wampe ushauri sababu yeye hawezi kuwa alfa na omega, wakimuidhinishia anunue kalamu nyekundu ili aitumie kuweka alama ya vema kwa kila analofanya.

Hapo bwana mkubwa, na kasi yake huenda akawa kambare aliyejitofautisha na waliotoka kwenye bwawa lile. J'mosi njema
 
Nimeipenda sana hii....akipatikana mwandishi aipanue itoshe ukurasa wa gazeti mzimaaa kabisa....
 
Hoja hii imesimama! good point to note na sisi watanzania tunakuwaga vichwqmaji, maana kilasiku huwa hatuishi kuwa na matumaini ya plastiki!
 
Aaah, Kambareeeeh! Sijui kama sabuni itaosha vizuri. Sidhani. Ila umekuja vizuri sana.
 
Ila asil ya kambale kuteleza shombo ubabe vyote vyake ukitaka viishe vyote ladhima umuoshe na ndim majivu je waoshaji tupo teyar maana waoshaji ndo ss
 
Ukitaka jumsafisha kambale lazima umpotezee uhai wake,au umbadilishie bwawa ukimrudisha kwenye bwawa lake matope yanarudi tena.
 
Ila uyu kambele wa safar hii tukimosha to atumrudishi kwenye matope ni bahalin maana bahari aikai na uchafu
 
Nimeipenda sana hii....akipatikana mwandishi aipanue itoshe ukurasa wa gazeti mzimaaa kabisa....

Jifarijini tu.Huyu sio kambare Ni NYANGUMI
Mpaka 2025 mtapiga kelele juu ya mgongo wake Na wala hahisi kitu.
 
We vipi? Watz si wajinga. Walimchagua huyu kambale na kumtosa yule kambale mwingine kwa sababu, kambale aliyetoswa ilitahadharishwa mapema kuwa HASAFISHIKI. Mwulize Kubenea. Kwani we ni mgeni hapa Tz usiyajue haya? Umahiri wako wa kuandika, andika post zenye mantiki na uhalisia si kurembesha lugha tu. Huyu kambale amekuja kwa wakati muafaka, mwacheni afanye kazi.
 
Back
Top Bottom