Bwana W. J. Malecela - Mwisho wa Uchaguzi Huu ni Mwanzo wa Maandalizi ya Uchaguzi Ujao

Keil

JF-Expert Member
Jul 2, 2007
2,214
803
Bwana William J. Malecela,

Kwanza hongera kwa kujitosa kwenye ulingo wa siasa za CCM ili kupima kina maji. Mara baada ya matokeo hukusita kuja JF kuonyesha uungwana wako kutujulisha matokeo na what is next. Ukigombea nafasi yoyote ile kuna kushinda na kushindwa. Kuja wako kukiri kwamba kura hazikutosha ni mfano mzuri kwa wana siasa, na sio wale ambao mambo yakienda kombo anapotea moja kwa moja.

Katika hilo bandiko la jana ulisema sasa unajipanga upya, mimi ninasema ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao. Siasa za Bongo ndani ya chama chochote zinahitaji maandalizi na uwepo wa mhusika ground zero. Bila network huwezi kufanikiwa, lazima kuwe na sikio linasikiliza kinachoendelea jimboni na wewe mwenyewe unaonekana onekana.

Pamoja na maandalizi hayo, mimi naomba nijikite kwenye mapungufu yaliyojitokeza hapa JF tangu ulipotangaza nia ya kugombea Ubunge wa EAC. Kuna mambo ambayo hayakwenda sawa na kama utajaribu tena kutupa karata yako huko EALA hapo mwaka 2017, itabidi uyaweke sawa mapema ili yasije yakakuathiri.

Mahali ulipoteleza - JF Ilichangia Kupunguza Kura zako
Bandiko lako la kwanza kabisa la kututangazia kwamba sasa unagombea Ubunge wa EAC, lilikuwa zuri sana na lili-set mwanzo mwema kwamba kama kuna mtu ulishawahi kukwaruzana naye huko nyuma hapa JF, basi unaomba msameheane na hivyo kuanza ukurasa mpya. Kwa bahati mbaya hii ni JF huwezi ukapendwa na kushangiliwa na kila mtu, lazima wapo ambao watakuponda na kukukatisha tamaa na wapo ambao watakutia moyo.

Thread hiyo pamoja na nyingine zote zilizofuatia, kwa bahati mbaya ziliku-expose kwa kiasi kikubwa sana na kuwaonyesha wapiga kura wako kwamba wewe ni nani. Kumbuka wapiga kura hawa ni tofauti sana na wale wa majimboni. Wapiga kura wa kuchagua wabunge wa EAC, asilimia 90 au zaidi huwa wanaingia hapa JF ama kwa majina yao halisi, majina ya bandia au wakiwa kama wageni tu (Guests). Sitting room yao huwa ni hapa kwenye Jukwaa la Siasa, tunashinda nao na tunakesha nao hapa. Ukiona Mheshimiwa Mchungaji "Dr." Getrude Rwakatare anaingia JF, then be assured kwamba ni akina "Prof" Maji Marefu tu ndo hawaingii hapa. Uthibitisho wa hili ni kwamba wabunge wengi wa CCM na CCM yenyewe wameishailalamkia JF na walitaka ifungwe. Kwa hiyo chochote unachoandika hapa kinasomwa vizuri sana na wabunge na hao ndio wapiga kura wako.

Kanuni kuu ya siasa, avoid kauli za ajabu ajabu na hasa zilizokaa kimtaani mtaani. Kwa bahati mbaya waliokuwa wanajibizana na wewe walikufikisha mahali ukashindwa kuji-control. Binadam ni wepesi sana wa kum-judge mtu kwa maandishi, na sio kwa kuangalia amefanya nini au atafanya nini. Kuna watu walipokuona kwenye TV jana walikuwa wanashangaa kwamba mbona huyu Bwana hafanani na maandishi ya hapa ndani? [Tafuta thread ya jana ya LIVE kutoka Mjengoni].

Hapa JF self control ni ngumu sana na hasa unapoona kuna watu wanapiga chini ya mkanda. Ndio maana Marehemu Regia (RIP) alikuwa anakaa kimya bila kujibu au anatoka tu. Au akina Zitto na Mnyika hawajibu kila kitu. Maana ukisema ujibu kila kinachobandikwa hapa, mwisho unaweza kutukana. Kitu muhimu ni kuchukua constructive criticisms ambazo zitakujenga na kukufanya u-gain knowledge, maana wapo ambao wataku-challenge na kukupa reference au hint za hoja, pia wapo wengine wataku-criticize bila kuonyesha mapungufu na wengine they will do it just for fun kuona reaction yako. Hicho ndicho kilichotokea kwenye threads zote kuanzia ile ujio wako hapa Bongo kuna watu walienda an extra mile mpaka wakabandika na picha zako, pia ile ya kutangaza nia, ile ya kuteuliwa na CC na ile kura za maoni za wabunge wa CCM.

Ukiwa na nafasi pitia threads zote zinazokuhusu, lazima utaambua mawili matatu ambayo ni mazuri au criticism ambazo ni za kukujenga na sio kukukatisha tamaa. Na pia inawezekana unaweza kugundua baadhi ya mabandiko yako yalikuwa na kasoro.

Chunguza Mfumo wa Upigaji Kura ndani ya Chama
Sijui mfumo wa kupiga kura ukoje, but I guess something is wrong somewhere. Siku ya kura za maoni za wabunge wa CCM ambao wako kama 250 hivi, Bwana William ulipata kura 142 kama sikosei, huku Kimbisa akiwa na kura 193, Makongoro Nyerere alikuwa na kura 123. Kwa mshangao mkubwa matokeo ya jana yameonyesha kwamba una kura 42 ambazo ni za Bunge zima la wabunge 305 waliopiga kura. Makongoro alipata 123 na Kimbisa alipata 210. Je, ina maana ya kwamba kipindi cha wiki moja kinaweza kuwa kimebadilisha mawazo ya wapiga 100 kukunyima kura zao? Hapa nime-assume kwamba wabunge 42 waliokupa kura ni wana CCM wenzako.

Hapa kuna mawili, ama mfumo wa kupiga kura una kasoro, au wakati wewe unapiga kampeni nyuma yako kulikuwa na mtu anakufuata akifuta nyayo zako. Kibaya zaidi whatever ambacho ulikuwa unafanya, ama kilikuwa wazi hapa JF au facebook, kitu ambacho kinamrahishia mtu anayefuata nyayo kujua unaenda wapi na umekutana au unapanga kukutana na nani. Maana sehemu zote ulizoenda Zanzibar, Arusha na kwingineko ulikuwa una andika hapa JF au facebook kwenye wall yako. Strategically kwa siasa za sasa ndani ya CCM ambako makundi yameshamiri na watu wamejenga uadui kulingana na makundi na kwamba wanasimamia nini, kama kuna mbaya wako ni rahisi sana kukufanyia mchezo mchafu wa kukufuatilia akifuta nyayo zako kwa dau la kueleweka.

What is Next?
Kama malengo ni @EALA, then fanyia kazi hayo hapo juu. Kama malengo ni @Mtera [maana ulipotua tu ulisema ulikuwa na ziara za vijijini], then you are safe maana wapiga kura wako ni wachache sana wanaoingia hapa JF. Lakini PR ni muhimu sana, wapiga kura huwa ni wepesi wa kum-judge mtu hata kwa kusikia tu kwa mbali. Bahati mbaya zaidi Mbunge wa Mtera ni mtaalam wa siasa za maneno machafu, anaweza kuwarubuni wapiga kura kirahisi sana na wakati mwingine hata kutumia tu hizi picha zako za madini shingoni. Tanzania huko vijijini bado tuko nyuma sana, issue ndogo kama hiyo inaweza kuwa kubwa na ikashikiwa bango na wananchi wakaona ni hoja na kumbe ni vioja vya kibajaj baada ya kukosa sera anaanza kuuliza nyasi zina rangi gani.

Kila la Heri katika Tafakuri yako on what is next.
 
Keil,

Great analysis......

There can be no truly great Tanzanian without the success of a great Tanzanian society! How we make our choices today is history in the making – whether for the better or for the worse! Whether in damnation or in praise, history and posterity will judge this generation based on the actions and the choices of the moment!!
 
Huyu hata afanyaje hawezi kupata kama si kwa kubebwa. Watanzania tumechoka kuongozwa kifalme, ana ndoto nzuri lakini ifike wakati na majina mengine yatwale nchi hii sio kila siku Baba, mtoto, leo aunt, kesho mjomba kama tuonavyo.
 
Uchambuzi mzuri na wakina uluojaa kila aina ya tafakuri, cha msingi ni kuangalia wapi ulipo jikwaa fitina za kisiasa, rushwa ndo utamaduni uliobaki kwenye siasa za Tanzania (ambazo hazijengi taifa letu). Jitahidi ku control your emotions unapojibu maswali (kwenye trend hapa JF) maana kuna watu kwenye jamii yetu ambo hupenda kuona unareact vipi unapo ulizwa maswali japo mengine hayana staha maana ujue uwakilishi wake ni mpana zaidi ya uwakilishi wa jimbo. HONGERA KWA UAMUZI WAKO WA KUWA WAZI THERE IS ALWAYS NEXT TIME. KEEP IT UP BRO
 
Keil unazungumziaje kuhusu madai ya rushwa aliyo yaibua?
Je kama aliona wabunge wa upinzani wakipokea rushwa toka kwake au kwa mgombea mwingine ni kweli hajui kuwa kuna chombo cha kupambana na rushwa hapa nchini kinacho itwa TAKUKURU?
Kama ameona watu wanapokea rushwa na kunyamaza analeta taswira gani akiwa na uchu wa kutaka kutuwakilisha huko kwenye bunge la EA?
Angepita asingeweza kuhongeka kirais na wawakilisha toka nchi za EA?
 
Zanzibar kuna Abdallah Ally Hassan Mwinyi,bara tuna Makongoro Julius Kambarage Nyerere na wewe William John Malecela ulitaka kuwa mmoja wao?.Acheni hizo wandugu ebu nendeni kwenye sekta zingine sio lazima siasa.Kama mna taaluma zenu kwa nn msiende khudumia watanzania wenzenu huko?.
 
Zanzibar kuna Abdallah Ally Hassan Mwinyi
Bara tuna Makongoro Julius Kambarage Nyerere
na Le Mutuz ulitaka ukae wapi kaka??
rudi baharini ukapambane na mawimbi...
 
Keil unazungumziaje kuhusu madai ya rushwa aliyo yaibua?
Je kama aliona wabunge wa upinzani wakipokea rushwa toka kwake au kwa mgombea mwingine ni kweli hajui kuwa kuna chombo cha kupambana na rushwa hapa nchini kinacho itwa TAKUKURU?
Kama ameona watu wanapokea rushwa na kunyamaza analeta taswira gani akiwa na uchu wa kutaka kutuwakilisha huko kwenye bunge la EA?
Angepita asingeweza kuhongeka kirais na wawakilisha toka nchi za EA?

Mkuu Fidel80,

Swala la rushwa liko complicated, sina hakika kama naweza kujibu maswali yako hapo juu. Siyo William pekee aliyeibua hilo swala, hata Makamba na Zitto wameandika kwenye wall ya facebook.

Kitendo cha kutotoa taarifa TAKUKURU, inawezekana ni kukosa imani na taasisi hiyo. Ndio maana Zitto alilalamika mpaka kwenye magazeti, lakini hakuna mtu wa TAKUKURU aliyechukua hatua ya kwenda kumhoji kwamba ni watu gani ili labda waweke mitego ya kuwanasa. Januri Makamba nae amelalamika lakini hajatoa taarifa. Kwa kifupi ni kwamba hakuna ambaye ana imani na TAKUKURU.

Hili swala la rushwa linavyojitokeza kwa kiasi fulani mimi ninalifurahia, kwa sababu angalau CCM wao wenyewe litaanza kuwakera na kuwaumiza, kwa hiyo lazima watafika mahali watapiga kelele za kutaka TAKUKURU iwajibike. Victim wa kwanza wa rushwa kwenye chaguzi ni CCM wenyewe. Juzi wamemwaga hela nyingi Arumeru lakini wakaambua patupu. Sijasikia wabunge wa upinzani wakilalamika kwamba kuna mmoja katoa rushwa, maana hawana hela za kutoa rushwa. Wapinzani pia wanatakiwa kuongeza kasi ya "sensitization" program, kwamba wapiga kura wakipewa rusha wapokee, siku ya kupiga kura wampe mgombea wanaeona anafaa. Watoa rushwa wakiliwa sana, itafika mahali wataona hailipi tena.

Mwisho, dhamira ya mhusika ndio ambayo inaweza kutoa jibu la kwamba je Bwana William akipewa rushwa anaweza kukubali au kukataa. Hapo siwezi kujua.
 
Mie anitajie tuu majina ya hao baadhi ya wabunge wa upinzani anaodai wanachukua rushwa na roho yangu itapona.

LOL ... hapa inabidi umbane na Makamba Jr. maana na yeye anasema kuna wabunge wa upinzani pia wamepokea mshiko, so anasema ni aibu ya Bunge zima na sio CCM tu!
 
Nakushauri ukalichukue jimbo la Mtera kiulaini kwa tiketi ya chadema. Chukulia seriously
 
Huu ushauri ni wa kuongeza idadi ya wabunge wa CDM tu bungeni (kama atashinda), lakini katika hali halisi sidhani kama chama kinahitaji mgombea kama huyu; haonyeshi dalili yoyote ya kuwa tofauti na umagamba; aendelee tu huko huko CCM.
 
willium anashindwa kuelewa kuwa ccm haitaki jina malecela

ccm kamwe haitampa nafasi mzawa yeyote wa damu ya malecela kwa sababu zilizo wazi

willy ni lazima atambue huu ukweli kama ana taka maisha ya uanasiasa
 
Nakushauri ukalichukue jimbo la Mtera kiulaini kwa tiketi ya chadema. Chukulia seriously

Kashasema baadhi ya wabunge wa upinzani wanapokea rushwa pia.
Kweli unamwona huyu ndio staili ya wabunge ambao chama kinachojiita makini kinataka kuwa nao?
 
Bwana William J. Malecela,

Kwanza hongera kwa kujitosa kwenye ulingo wa siasa za CCM ili kupima kina maji. Mara baada ya matokeo hukusita kuja JF kuonyesha uungwana wako kutujulisha matokeo na what is next. Ukigombea nafasi yoyote ile kuna kushinda na kushindwa. Kuja wako kukiri kwamba kura hazikutosha ni mfano mzuri kwa wana siasa, na sio wale ambao mambo yakienda kombo anapotea moja kwa moja.

Katika hilo bandiko la jana ulisema sasa unajipanga upya, mimi ninasema ni mwanzo wa maandalizi ya uchaguzi ujao. Siasa za Bongo ndani ya chama chochote zinahitaji maandalizi na uwepo wa mhusika ground zero. Bila network huwezi kufanikiwa, lazima kuwe na sikio linasikiliza kinachoendelea jimboni na wewe mwenyewe unaonekana onekana.

Pamoja na maandalizi hayo, mimi naomba nijikite kwenye mapungufu yaliyojitokeza hapa JF tangu ulipotangaza nia ya kugombea Ubunge wa EAC. Kuna mambo ambayo hayakwenda sawa na kama utajaribu tena kutupa karata yako huko EALA hapo mwaka 2017, itabidi uyaweke sawa mapema ili yasije yakakuathiri.

Mahali ulipoteleza - JF Ilichangia Kupunguza Kura zako
Bandiko lako la kwanza kabisa la kututangazia kwamba sasa unagombea Ubunge wa EAC, lilikuwa zuri sana na lili-set mwanzo mwema kwamba kama kuna mtu ulishawahi kukwaruzana naye huko nyuma hapa JF, basi unaomba msameheane na hivyo kuanza ukurasa mpya. Kwa bahati mbaya hii ni JF huwezi ukapendwa na kushangiliwa na kila mtu, lazima wapo ambao watakuponda na kukukatisha tamaa na wapo ambao watakutia moyo.

Thread hiyo pamoja na nyingine zote zilizofuatia, kwa bahati mbaya ziliku-expose kwa kiasi kikubwa sana na kuwaonyesha wapiga kura wako kwamba wewe ni nani. Kumbuka wapiga kura hawa ni tofauti sana na wale wa majimboni. Wapiga kura wa kuchagua wabunge wa EAC, asilimia 90 au zaidi huwa wanaingia hapa JF ama kwa majina yao halisi, majina ya bandia au wakiwa kama wageni tu (Guests). Sitting room yao huwa ni hapa kwenye Jukwaa la Siasa, tunashinda nao na tunakesha nao hapa. Ukiona Mheshimiwa Mchungaji "Dr." Getrude Rwakatare anaingia JF, then be assured kwamba ni akina "Prof" Maji Marefu tu ndo hawaingii hapa. Uthibitisho wa hili ni kwamba wabunge wengi wa CCM na CCM yenyewe wameishailalamkia JF na walitaka ifungwe. Kwa hiyo chochote unachoandika hapa kinasomwa vizuri sana na wabunge na hao ndio wapiga kura wako.

Kanuni kuu ya siasa, avoid kauli za ajabu ajabu na hasa zilizokaa kimtaani mtaani. Kwa bahati mbaya waliokuwa wanajibizana na wewe walikufikisha mahali ukashindwa kuji-control. Binadam ni wepesi sana wa kum-judge mtu kwa maandishi, na sio kwa kuangalia amefanya nini au atafanya nini. Kuna watu walipokuona kwenye TV jana walikuwa wanashangaa kwamba mbona huyu Bwana hafanani na maandishi ya hapa ndani? [Tafuta thread ya jana ya LIVE kutoka Mjengoni].

Hapa JF self control ni ngumu sana na hasa unapoona kuna watu wanapiga chini ya mkanda. Ndio maana Marehemu Regia (RIP) alikuwa anakaa kimya bila kujibu au anatoka tu. Au akina Zitto na Mnyika hawajibu kila kitu. Maana ukisema ujibu kila kinachobandikwa hapa, mwisho unaweza kutukana. Kitu muhimu ni kuchukua constructive criticisms ambazo zitakujenga na kukufanya u-gain knowledge, maana wapo ambao wataku-challenge na kukupa reference au hint za hoja, pia wapo wengine wataku-criticize bila kuonyesha mapungufu na wengine they will do it just for fun kuona reaction yako. Hicho ndicho kilichotokea kwenye threads zote kuanzia ile ujio wako hapa Bongo kuna watu walienda an extra mile mpaka wakabandika na picha zako, pia ile ya kutangaza nia, ile ya kuteuliwa na CC na ile kura za maoni za wabunge wa CCM.

Ukiwa na nafasi pitia threads zote zinazokuhusu, lazima utaambua mawili matatu ambayo ni mazuri au criticism ambazo ni za kukujenga na sio kukukatisha tamaa. Na pia inawezekana unaweza kugundua baadhi ya mabandiko yako yalikuwa na kasoro.

Chunguza Mfumo wa Upigaji Kura ndani ya Chama
Sijui mfumo wa kupiga kura ukoje, but I guess something is wrong somewhere. Siku ya kura za maoni za wabunge wa CCM ambao wako kama 250 hivi, Bwana William ulipata kura 142 kama sikosei, huku Kimbisa akiwa na kura 193, Makongoro Nyerere alikuwa na kura 123. Kwa mshangao mkubwa matokeo ya jana yameonyesha kwamba una kura 42 ambazo ni za Bunge zima la wabunge 305 waliopiga kura. Makongoro alipata 123 na Kimbisa alipata 210. Je, ina maana ya kwamba kipindi cha wiki moja kinaweza kuwa kimebadilisha mawazo ya wapiga 100 kukunyima kura zao? Hapa nime-assume kwamba wabunge 42 waliokupa kura ni wana CCM wenzako.

Hapa kuna mawili, ama mfumo wa kupiga kura una kasoro, au wakati wewe unapiga kampeni nyuma yako kulikuwa na mtu anakufuata akifuta nyayo zako. Kibaya zaidi whatever ambacho ulikuwa unafanya, ama kilikuwa wazi hapa JF au facebook, kitu ambacho kinamrahishia mtu anayefuata nyayo kujua unaenda wapi na umekutana au unapanga kukutana na nani. Maana sehemu zote ulizoenda Zanzibar, Arusha na kwingineko ulikuwa una andika hapa JF au facebook kwenye wall yako. Strategically kwa siasa za sasa ndani ya CCM ambako makundi yameshamiri na watu wamejenga uadui kulingana na makundi na kwamba wanasimamia nini, kama kuna mbaya wako ni rahisi sana kukufanyia mchezo mchafu wa kukufuatilia akifuta nyayo zako kwa dau la kueleweka.

What is Next?
Kama malengo ni @EALA, then fanyia kazi hayo hapo juu. Kama malengo ni @Mtera [maana ulipotua tu ulisema ulikuwa na ziara za vijijini], then you are safe maana wapiga kura wako ni wachache sana wanaoingia hapa JF. Lakini PR ni muhimu sana, wapiga kura huwa ni wepesi wa kum-judge mtu hata kwa kusikia tu kwa mbali. Bahati mbaya zaidi Mbunge wa Mtera ni mtaalam wa siasa za maneno machafu, anaweza kuwarubuni wapiga kura kirahisi sana na wakati mwingine hata kutumia tu hizi picha zako za madini shingoni. Tanzania huko vijijini bado tuko nyuma sana, issue ndogo kama hiyo inaweza kuwa kubwa na ikashikiwa bango na wananchi wakaona ni hoja na kumbe ni vioja vya kibajaj baada ya kukosa sera anaanza kuuliza nyasi zina rangi gani.

Kila la Heri katika Tafakuri yako on what is next.

- Well, mkuu heshima sana kwenye maisha na kwenye siasa kila kitu ni lazima kupima risks, JF haikuhusika in anyway na kushindwa kwangu, naomba nikwambia tena knowing all the FACTS za uchaguzi nilioshiriki, ninasema tena JF had nothing to do with anything, My Facebook had nothing nasema tena absolutely nothing.

- Nimeshindwa na wagombea wenye uzoefu wa muda mrefu sana na chaguzii, wameshindwa na wamewahi kushinda sana, as opposed na mimi na miezi mitatu tu kwenye siasa za bongo, siamini kwamba walioshindwa wote jana ni members wa hapa JF'

- JF na Facebook zimenisaidia sana, hasa na hizi kampeni, isipokuwa nimeshindwa tu na waliokuwa na akili za kampeni kuliko mimi na wenye uzoefu mkubwa sana kuliko wangu, ingawa nimekusikia sana!

Again, JF has absolutely nothing to do with it!

Willie @Dodoma City!
 
Back
Top Bottom