Bwana Tundu Lissu, Hoja ya Chato na Maendeleo ya sasa inajibika Kimantiki

UPUUZI MTUPU!
Salaam Wana JF.

Nimesoma na kuona andiko la Bwana Tundu AM Lissu kutoka Ubelgiji akijenga hoja juu ya maendeleo ya vitu na watu ndani ya eneo la Chato anapotoka rais wa sasa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Sijaona mantiki ya Lissu kupotosha umma wa Watanzania dhidi ya maendeleo ya sasa kwa Chato. Aidha, kabla ya kujenga hoja zangu dhidi ya hoja za Lissu, nitumie jukwaa hili kukanusha upotoshaji wa kumfananisha Rais Magufuli na Madikteta wa Kiafrika akina Mobutu Sese Seko, Felix Houphouet-Boigny, Hastings Kamuzu Banda na wengineo, Kwa hoja hii Lissu umepotosha umma na awatake radhi Watanzania na Rais Mwenyewe, kamwe uwezi kuzifananisha sifa za Mobutu na JPM labda kama hujui uovu na ukatili wa Mobutu Sese Seko.

Aidha Bwana Lissu unaporejea Kitabu cha Peter Kenyon "Dictatorland, The Men Who Stole Africa" Anachokiongelea Mwandishi Peter kwa viongozi wa Kiafrika walionajisi nchi zao hakina uhalisia na kinachofanywa na Rais Magufuli kwa sasa ndani ya eneo la Chato, Mantiki ya Peter Kenyon ni kuwamulika viongozi waliotawala Afrika na kujitajilisha wao wenyewe kimaendeleo dhidi ya Umma yaani wenye nchi, Rais Magufuli anatajilisha Umma kimaendeleo badala yake binafsi ndipo hoja iliposimama hapa.

Bwana Lissu kama unavyojua ni ngumu sana kuzuia watu kusema lakini linapokuja suala la upotoshaji ni sharti tujenge hoja kuepusha kikombe hiki kutamalaki, Bwana Lissu kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika Mkoa wa Geita wilayani Chato ni Jambo la kawaida kwa mantiki kuwa kusudio la Maendeleo hayo ni kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali eneo unalotoka, Umerejea awamu zilizopita ukiwataja viongozi wa awamu hizo nne kuwa hawakufanya kinachofanywa kwa sasa, Bwana Lissu nikujulishe kuwa kila nyakati na mambo yake.

Wakati wa Mwl. Nyerere alifanya kulingana na uhitaji na mipango ya wakati ule lakini pia alinyoshewa kidole na wakosoaji wake wa masuala ya maendeleo, Hivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwahiyo lawama za namna hii hazikuanza leo na kamwe huwezi kuzimaliza lakini zinapopotosha zinajibiwa kimantiki, hata hivyo kila utawala utofautiana kiutawala, tunachokiona sasa sio kile tutakachokiona awamu ijayo ya sita.

Tunge jenga hoja za kumushambulia Rais Magufuli endapo tu kama angekuwa anafanya maendeleo ya namna hii nje ya Tanzania, hata mimi ningeunga mkono hoja kwa kitendo hicho lakini kinachofanywa ni ndani ya ardhi ya Tanzania, Aidha ninge hoji na kukosoa endapo tu Rais Magufuli angekuwa anafanya kwa maslahi yake binafsi na familia yake, lakini kinachofanywa ni kwa maslahi ya umma, Je nongwa inatoka wapi? Au ni husuda tu wa kisiasa kwa sababu ya itikadi za vyama vyetu?

Bwanba Lissu unadriki kulinganisha Mobutu Sese Seko ,Felix Houphouet-Boigny na Rais Magufuli, Je unajua viongozi hawa walitumia kodi za walala hoi kufanya starehe na anasa nyingine za kufuru hata zilizokuwa kinyume na amri kumi za Mungu kwa kujenga majumba ya kifahari kwa familia zao na kuwekeza mapesa mengi kwenye makampuni yaliyo je ya mataifa yao, Kinachofanywa Chato ni uwekezaji wa anasa au kwa mustakabari wa maendeleo ya watu kwa kizazi cha leo na hapo badae? Je baada ya rais muda wake yote yaliyofanyika ndani ya geita yatakuwa mali ya serikali au familia ya Magufuli?

Je, hoja ya kupinga maendeleo ya Chato inatoka wapi na ina mantiki ipi? Hata hivyo bwana Lissu unapo ongelea kisa cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini bwana Zuma aligeuza kijiji chake cha Nkandla kuwa kama ambavyo Magufuli anaigeuza Chato Si kweli, Tuhuma za Zuma ni kujenga Jumba la Kifahari na baadhi ya mambo mengine ya anasa kwa kutumia kodi ya Wana Afrika Kusini badala ya kutumia pesa yake binafsi, na ndo maana mahakama iliamuru arudishe hela na akarudisha, Je ufanano wa Zuma na Magufuli upo wapi hapa bwana Lissu?

Nihitimishe andiko hili kwa kusema kinachoendelea mitandaoni kuhoji na kushambulia kile kinachofanyika Mkoani Geita wilayani chato kama kitu kisichokubalika kwa umma ni upotoshaji ambao sharti Watanzania tuupuuze na tuungane kwa pamoja kuendelea kuijenga nchi yetu katika dhana ya maendeleo na watu wake, Maendeleo hayana ukanda ilimradi tu kinachofanyika kiwe ndani ya ardhi ya Tanzania.

Deogratias Mutungi
 
Hata uwanja wa ndege Mobutu aliujenga nchini kwake, lakini kijijini kwao. Na Lissu amesema kabisa, kilichofanyika huko hakikuwa kwenye mpango kazi wowote wa dira ya Taifa, bali mambo hayo yamefanyika kwakuwa rais anatokea huko. Maelezo ya Lisu yanaeleweka. Na kama kiongozi sio dictator hawezi kudhubutu kufanya upendeleo wa wazi hivyo.
Hivi uwanja wa ndege wa Chato ni mali ya JPM?

Mnaposema haikuwa mpango kazi wa taifa mnao uhakika? Mbona tender ilitangazwa na Mayanga Contractors ikapata kazi?
 
Tunazungumzia upendeleo kwa wilaya Chato kwasababu JPM ni mzawa wa huko!Huoni sasa tunajengewa mazingira ya kuchaguana kikabila kwa kuamini kuwa mzawa atapendelea eneo alilotokea!

Mimi nataka asimame mtu anioneshe kwa ushahidi na data kuwa miradi inayoendelea Chato haina uhusiano wowote na Rais kuwa mzawa wa huko!
Wewe unaamini hakuna uhusiano?Kwamba hata Rais asingekuwa JPM bado miradi hiyo ingefanyika Chato kutokana na mpango wa maendeleo!
 
Salaam Wana JF.

Nimesoma na kuona andiko la Bwana Tundu AM Lissu kutoka Ubelgiji akijenga hoja juu ya maendeleo ya vitu na watu ndani ya eneo la Chato anapotoka rais wa sasa Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Sijaona mantiki ya Lissu kupotosha umma wa Watanzania dhidi ya maendeleo ya sasa kwa Chato. Aidha, kabla ya kujenga hoja zangu dhidi ya hoja za Lissu, nitumie jukwaa hili kukanusha upotoshaji wa kumfananisha Rais Magufuli na Madikteta wa Kiafrika akina Mobutu Sese Seko, Felix Houphouet-Boigny, Hastings Kamuzu Banda na wengineo, Kwa hoja hii Lissu umepotosha umma na awatake radhi Watanzania na Rais Mwenyewe, kamwe uwezi kuzifananisha sifa za Mobutu na JPM labda kama hujui uovu na ukatili wa Mobutu Sese Seko.

Aidha Bwana Lissu unaporejea Kitabu cha Peter Kenyon "Dictatorland, The Men Who Stole Africa" Anachokiongelea Mwandishi Peter kwa viongozi wa Kiafrika walionajisi nchi zao hakina uhalisia na kinachofanywa na Rais Magufuli kwa sasa ndani ya eneo la Chato, Mantiki ya Peter Kenyon ni kuwamulika viongozi waliotawala Afrika na kujitajilisha wao wenyewe kimaendeleo dhidi ya Umma yaani wenye nchi, Rais Magufuli anatajilisha Umma kimaendeleo badala yake binafsi ndipo hoja iliposimama hapa.

Bwana Lissu kama unavyojua ni ngumu sana kuzuia watu kusema lakini linapokuja suala la upotoshaji ni sharti tujenge hoja kuepusha kikombe hiki kutamalaki, Bwana Lissu kinachofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika Mkoa wa Geita wilayani Chato ni Jambo la kawaida kwa mantiki kuwa kusudio la Maendeleo hayo ni kwa manufaa ya Watanzania wote bila kujali eneo unalotoka, Umerejea awamu zilizopita ukiwataja viongozi wa awamu hizo nne kuwa hawakufanya kinachofanywa kwa sasa, Bwana Lissu nikujulishe kuwa kila nyakati na mambo yake.

Wakati wa Mwl. Nyerere alifanya kulingana na uhitaji na mipango ya wakati ule lakini pia alinyoshewa kidole na wakosoaji wake wa masuala ya maendeleo, Hivyo hivyo kwa Mwinyi, Mkapa na Kikwete kwahiyo lawama za namna hii hazikuanza leo na kamwe huwezi kuzimaliza lakini zinapopotosha zinajibiwa kimantiki, hata hivyo kila utawala utofautiana kiutawala, tunachokiona sasa sio kile tutakachokiona awamu ijayo ya sita.

Tunge jenga hoja za kumushambulia Rais Magufuli endapo tu kama angekuwa anafanya maendeleo ya namna hii nje ya Tanzania, hata mimi ningeunga mkono hoja kwa kitendo hicho lakini kinachofanywa ni ndani ya ardhi ya Tanzania, Aidha ninge hoji na kukosoa endapo tu Rais Magufuli angekuwa anafanya kwa maslahi yake binafsi na familia yake, lakini kinachofanywa ni kwa maslahi ya umma, Je nongwa inatoka wapi? Au ni husuda tu wa kisiasa kwa sababu ya itikadi za vyama vyetu?

Bwanba Lissu unadriki kulinganisha Mobutu Sese Seko ,Felix Houphouet-Boigny na Rais Magufuli, Je unajua viongozi hawa walitumia kodi za walala hoi kufanya starehe na anasa nyingine za kufuru hata zilizokuwa kinyume na amri kumi za Mungu kwa kujenga majumba ya kifahari kwa familia zao na kuwekeza mapesa mengi kwenye makampuni yaliyo je ya mataifa yao, Kinachofanywa Chato ni uwekezaji wa anasa au kwa mustakabari wa maendeleo ya watu kwa kizazi cha leo na hapo badae? Je baada ya rais muda wake yote yaliyofanyika ndani ya geita yatakuwa mali ya serikali au familia ya Magufuli?

Je, hoja ya kupinga maendeleo ya Chato inatoka wapi na ina mantiki ipi? Hata hivyo bwana Lissu unapo ongelea kisa cha Rais wa zamani wa Afrika Kusini bwana Zuma aligeuza kijiji chake cha Nkandla kuwa kama ambavyo Magufuli anaigeuza Chato Si kweli, Tuhuma za Zuma ni kujenga Jumba la Kifahari na baadhi ya mambo mengine ya anasa kwa kutumia kodi ya Wana Afrika Kusini badala ya kutumia pesa yake binafsi, na ndo maana mahakama iliamuru arudishe hela na akarudisha, Je ufanano wa Zuma na Magufuli upo wapi hapa bwana Lissu?

Nihitimishe andiko hili kwa kusema kinachoendelea mitandaoni kuhoji na kushambulia kile kinachofanyika Mkoani Geita wilayani chato kama kitu kisichokubalika kwa umma ni upotoshaji ambao sharti Watanzania tuupuuze na tuungane kwa pamoja kuendelea kuijenga nchi yetu katika dhana ya maendeleo na watu wake, Maendeleo hayana ukanda ilimradi tu kinachofanyika kiwe ndani ya ardhi ya Tanzania.

Deogratias Mutungi
Huweziii ukapata ajali ya jeraha kama lile halafu kwa mda mfupi akili ikatengamaa. Mimi naona acheni kuhangaika na mambo ya huyo kijana.
 
Hivi uwanja wa ndege wa Chato ni mali ya JPM?

Mnaposema haikuwa mpango kazi wa taifa mnao uhakika? Mbona tender ilitangazwa na Mayanga Contractors ikapata kazi?

Hata uwanja wa ndege wa Mobutu ulikuwa ni wa nchini kwake, ila ulijengwa kijijini kwake. Mwanza mjini kuna uwanja wa ndege, sidhani kama kulikuwa na uhitaji mkubwa sana wa uwanja mwingine wa ndege wa kiwango hicho ndani ya umbali mfupi hivyo. Kwa sasa una haki ya kutetea hilo, ila atakapotoka madarakani utakuja kuchukua mrejesho.
 
Kwa kuwa Mwanza kuna uwanja ndio Geita usijengwe uwanja? Unajua umbali wa Chato to Mwanza

Mimi sitetei, sioni sababu za msingi kunishawishi kupinga Chato kuwa na uwanja.
 
nyie pumbafu mmeshindwa kupeleka maendeleo kwenu, mnapeleka mikoa mingine
sasa usipo peleka maendeleo kwako/kwenu unategemea ni nani atakuletea au atapeleka?
wacheni mzee afanye maendeleo kwao ili iwe fundisho kwa wapumbafu wanaopachukia makwao.
 
Ndiyo zao hizo hawa MAZWAZWA wanaohaha kumfurahisha huyo anayejiita mwendawazimu kwa kupongeza udikteta an ufisadi wake mkubwa Nchini ili awape TEUZI.
Ndiyo maana ameweka jina lake kamili ili amfurahishe mfalme.
 
Unataka kusema Chato ndiyo Tanzania kwa sababu anatokea huko Rais wa awamu hii au tukueleweje,maana Tanzania ni kubwa na bado ina changamoto nyingi kama zilizoko Chato na si Geita kama unavyoipamba Geita kwa uelewa wako.

Geita ni makao makuu ya mkoa na Chato ni wilaya lakini vipaumbele vingi vimepelekwa Chato anakotokea mheshimiwa badala ya Geita wewe huoni hili ni dosari.
Vipaumbele vingi kama vipi? Hospital na uwanja wa ndege? Kwani mikoa mingine hakuna hospital na viwanja vya ndege vilivyojengwa/ kukarabatiwa?

Geita mjini hakuna hospital?
 
Kwa kuwa Mwanza kuna uwanja ndio Geita usijengwe uwanja? Unajua umbali wa Chato to Mwanza

Mimi sitetei, sioni sababu za msingi kunishawishi kupinga Chato kuwa na uwanja.

Nasema kwakuwa tayari Mwanza uwanja upo, hakukuwa na ulazima tena kwa umbali huo kuwa na uwanja wa kiwango hicho, hasa ukizingatia umbali uliopo. Umbali wa Chato na Mwanza ni mbali kama unaenda na baiskeli au miguu, ila sio kwa ndege. Ni kiongozi mwenye udictator tu anaweza kufanya kinachofanyika sasa. Subiri atoke madarakani ili uone ukweli wa hiki tunachokosoa.
 
Bila kupeoesa macho,yanayoendelea Chato,yanaleta ukanda na ukabila,ule mgawanyo wa resources haujabalance........why alwasy Chato?
 
Back
Top Bottom