Bwana Senzia Lushino, Afisa Tarafa Kata ya Moshi Magharibi Amsimamisha Kazi Mwalimu Honest Shirima kuanzia leo

Manfyantona

Member
Dec 24, 2019
13
20
Afisa Tarafa ya Moshi Magharibi Bwana Senzia Lushino mwishoni mwa wiki hii ametembelea Shule ya Sekondari Korongoni iliyoko manispaa ya Moshi Mjini katika kata ya Soweto na kukuta Mwalimu mtoro sugu bwana Honest Shirima hayupo.

Mwalimu huyo anatumia muda mwingi kuendesha Bajaj mjini moshi muda mwingi hivo kushindwa kutimiza majukumu yake ya kila siku shuleni.

Mkuu wa Shule bwana Jumanne alipoulizwa kutoa taarifa za mwalimu huyo alisema kuwa licha ya kumukanya na kumtaka ajibu barua aliyomwandikia mwalimu huyo amekuwa akikaidi na hajaijibu.

Mkuu huyo alidai kuwa swala la mwalimu huyo alijaribu kuwashirikisha walimu wengine na kujaribu kumshauri mwalimu huyo akaae kwenye mstari ila hawakuzaa matunda. Baada ya kuona wamegonga mwamba ilibidi swala la mwalimu huyo alifikishe kwa boss wake Afisa Elimu. Mkuu huyo anadae kuwa mwalimu huyo aliitwa manispaa na Afisa Elimu nako hakutii wito na hakwenda.

Afisa Elimu Kata nae alipoulizwa kusema chochote kuhusu huyo mwalimu nae alisema kuwa taarifa za utoro wa mwalimu huyo anazo na kuwa amekuwa akipata malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya mwalimu huyo.

Afisa Elimu kata aliongeza kuwa kwa kushirikiana na Mkuu wa Shule wamejaribu kumwita ili wamuonye ila mwalimu huyo amekuwa akikataa wito.

Baada ya maelezo hayo ya Mkuu wa Shule na Afisa Elimu Kata, mbele ya walimu wengine, Bwana Senzia aliwahoji wakuu hao hali ya ufaulu wa Somo analofundisha mwalimu huyo na kuambiwa kuwa somo la mwalimu huyo ( Commerce ) linaongoza kufelisha kila mwaka na kuwa hata matokeo ya mwaka jana ya kidato cha nne yalikuwa mabovu sana.

Kwa uchungu mkubwa, bwana Senzia alionesha kukasilika na kuwalaumu Afisa Elimu kata na Mkuu wa Shule kwa kutofikisha taarifa hizo za utoro wa mwalimu huyo ofisini kwake na badala yake wao waliamua kumlea na kumfumbia macho mwalimu huyo kitu ambacho si sahihi kiutendaji. Ndipo alipowaomba wajitadhimini utendaji kazi wao kama wanafaa kuendelea katika nyadhifa zao.

Baada ya hayo, ndipo alipotoa amri ya kumsimamisha Kazi mwalimu huyo bwana Honest Shirima mpaka uamuzi wa vikao vya juu utakapokaa na kuamua vinginevyo.

Aliongeza tena kuwa atahakikisha mwalimu huyo ameachishwa kazi au amehamishwa kwenye Tarafa yake kwani ana mamlaka ya kufanya hivo maana yeye ni mshauri wa Mkurugenzi ambaye ndiye mwajiri wa watumishi wite waliopo kwenye tarafa yake ya Moshi Magharibi.

Aliongeza pia kuwa mwalimu huyo (Honest Shirima) atafunguliwa mashitaka mahakamani na Takukuru ya wizi wa fedha za umma kwa kulipwa mishahara bila kufanya kazi.

Mwisho, aliwaasa walimu wa shule hiyo kuipenda kazi yao na kuwa wadilifu kwa kuepuka utoro kazini na kusema kuwa kama mtu anaona kazi ya walimu haimfai au haitaki basi aache kazi maana mitaani kuna watu wengi mno wanatamani kazi hii na hawana.
 
Hana mamlaka ya kisheria ya kumsimamisha wala kumfukuza kazi ,

Huyo afisa tarafa analikuwa analopoka tu iliyo na mamalaka ya kumfukuza mwalimu ni TSC A.K.A TSD

sent from toyota Allex
Ndio maana kaema Hadi Vikao vya juu vitakapokaa.Kwa hiyo unataka arndelee kuendesha Bajaj zake bila kusimamishwa kazi ?
 
Ndio maana kaema Hadi Vikao vya juu vitakapokaa.Kwa hiyo unataka arndelee kuendesha Bajaj zake bila kusimamishwa kazi ?
We unashabikia lakini hunui taratibu za kiutumishi ? Mtumishi hawajibishwi na kila mtu soma standing oder za utumishi wa umma ..

Ila kwa kuwa upo mtaani unasubiri fungulia dog ,mwezi wa tatu .........ukibahatika kupata ajira serikali ndio utajua ninachokiongea kwa sasa endelea kushabikia

sent from toyota Allex
 
Kama mshahara hautoshi kwanini asiendeshe hiyo bajaji? Kwataarifa tu ni kwamba watumishi wengi wa serikali kutokana na maslahi duni wanajiongeza kwa njia zingine kujipatia kipato.
 
Mwajiri ni mkurugenzi wa halmashauri, ndiye mwenye mamlaka ya kuajiri na kusimamisha kazi watumishi walio chini ya halmashauri. Huyo afisa tarafa ni kiazi tu, na aliamua kujifurahisha.
 
Huyo afisa tarafa mbona kimbele mbele sana, hana mamlaka ya kumtimua mtumishi wa umma aache usnitch
 
Kajifunze kwanza kuandika wewe Lushino. Unaandika kama umetoka pori leo jioni!

Hiyo nafasi ya Afisa Tarafa uliipataje na vyeti vyako feki? Lushino kwa kiha ni kinem.b.e

***Mbire mwene Nyamwonyo***
 
Viongozi wetu bwana kitu hekima hamna. Hata mkurugenzi hawezi kunisimamisha kazi. Isipokuwa TSC wilaya. Takokuu wachunguze nini wakati Mwalimu anapiga pindi.. Tujadili insue ya utoro full stop. Then Sheria iamue
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom