Bwana harusi mtarajiwa avamiwa na majambazi

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444

Bw.Edward na Mkewe Mtarajiwa Elizabeth, siku ya send off Mjini Same, wikiendi iliyopita.
Operl+3.JPG

Bwana harusi mtarajiwa akiwa wodini

Afisa Habari Daraja II wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Edward Denis Nkomola amevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo, nyumbani kwake Changanyikeni Dar es Salaam na kujeruhiwa vibaya mwilini.
Edward Nkomola ni bwana harusi mtarajiwa na maandalizi ya harusi yake yapo katika hatua za mwisho ambapo ndoa yake ilitarajiwa kufungwa Juni 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Afisa Habari mwenzake wa Wizara hiyo Ndugu Nicodemus Thom Mushi, tukio hilo lilimkuta Nkomola majira ya aa saba usiku, ambapo majambazi wanane wakiwa na silaha mbalimbali, walivamia nyumbani kwake na wakitaka wapewe fedha alizokusanya kwa ajili ya harusi yake.
Taarifa hiyo inasema kuwa kabla ya majambazi hao kufanikisha adhma yao hiyo walivunja mlango wa chuma (grill) na mlango wa kawaida na kuanza kumshambulia kwa mapanga na kumjeruhi mara kadhaa kichwani, kumvunja mkono, kumjeruhi kwa panga pajani na kumwibia samani za ndani, fedha, simu na vifaa mbali mbali vya harusi.
Wiki iliyopita alitoka Wilayani Same kwenye Send Off ya mke wake mtarajiwa Elizabeth.
Nkomola amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha Mifupa MOI akipatiwa matibabu na hali yake inaendelea kusimamiwa na madaktari kwa ukaribu zaidi.

chanzo: MO BLOG

Natoa pole na kumtakia nafuu ya haraka ili atimize ndoto yake ya kufunga ndoa.
 
Pole saa mtarajiwa. Sasa tuwe macho na michango watu wachangiaji wawe wanalipia kupitia bank na slip ziwasilishwe katika vikao. Hakila binadamu ni hatari sana.
 
Pole saa mtarajiwa. Sasa tuwe macho na michango watu wachangiaji wawe wanalipia kupitia bank na slip ziwasilishwe katika vikao. Hakila binadamu ni hatari sana.

Yaani hali si nzuri hata kidogo hadi michango ya harusi daaah!! Pole kwa bwana harusi aisee ila tuu wasije kuwa wamemharibu ile shuhuli inayotumika kwenye ndoa maana pamoja na mengine hiyo dushee ndo ndoa yenyewe.

Ila kuvamiwa na majambazi siku chache kabla ya harusi ni ajali tuu na mkosi au kuna mkono wa mtu? Watu wa karibu watakuwa wanajua hili maana hao majambazi wamekomba hado samani zake za ndani kuonesha wameamua kumfilisi ilhali yeye anaanza maisha.
Je sio komoa ya kumzalisha au kutembea na binti mwingine na akamtosa na ameamua kuoa mshana mwingine? Bwana harusi na ajihoji.
Je sio kuwa huyo binti alikuwa na mchumba mwingine na akamuacha kwa ajili ya huyu bwanaharusi mtarajiwa na sasa huyo aliyeachwa anaamua kumjeruhi huyu jamaa kama kumpa message kuwa umeniibia mchumba wangu.
Kama hakuna lolote kati ya hayo juu basi itakuwa ni majaribu tuu ambayo ataendelea kukutana nayo kwenye ndoa yake.
Ni mtazamo wangu tuu si kingine.
 
Yawezekana hujuma toka kwa wale alio wapiga chini au hujuma toka kwa mwanamke kwa jamaa zake alio wapiga chini.
 
poleni sana bwana harusi mtarajiwa, walaaniwe hao majambazi na wakafie mbali
 
Yaani hali si nzuri hata kidogo hadi michango ya harusi daaah!! Pole kwa bwana harusi aisee ila tuu wasije kuwa wamemharibu ile shuhuli inayotumika kwenye ndoa maana pamoja na mengine hiyo dushee ndo ndoa yenyewe.

Ila kuvamiwa na majambazi siku chache kabla ya harusi ni ajali tuu na mkosi au kuna mkono wa mtu? Watu wa karibu watakuwa wanajua hili maana hao majambazi wamekomba hado samani zake za ndani kuonesha wameamua kumfilisi ilhali yeye anaanza maisha.
Je sio komoa ya kumzalisha au kutembea na binti mwingine na akamtosa na ameamua kuoa mshana mwingine? Bwana harusi na ajihoji.
Je sio kuwa huyo binti alikuwa na mchumba mwingine na akamuacha kwa ajili ya huyu bwanaharusi mtarajiwa na sasa huyo aliyeachwa anaamua kumjeruhi huyu jamaa kama kumpa message kuwa umeniibia mchumba wangu.
Kama hakuna lolote kati ya hayo juu basi itakuwa ni majaribu tuu ambayo ataendelea kukutana nayo kwenye ndoa yake.
Ni mtazamo wangu tuu si kingine.

Kweli mkuu, yote yawezekana kuwa kuna kisasi ila pia maisha magumu ya siku hizi yamewafanya watu wasiwe na ujira rasmi kwa hiyo ni crimes kwa kwenda mbele. Najaribu kuona jinsi harusi inagharimu halafu uahirishe wakati kila kitu umeshalipia hasa ukumbi, na mengineyo. Yaani binadamu unyama umetujaa sasa.
 
Back
Top Bottom