Bwana harusi mtarajiwa afariki akienda kutoa mahari

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
MAISHA ya mwanadamu ni siri ya Mola wake na akiamua kuyakatisha, basi hakuna mwanadamu wa kubisha!

ajalii-1.jpg


NDOTO ZAYEYUKA

Ndivyo ilivyotokea baada ya kuyeyuka kwa ndoto za bwana harusi mtarajiwa, Michael Mapesi aliyefariki dunia akiwa njiani kwenda kumtolea mahari mchumba’ke, Vivian Malamsha, siku chache kabla ya kuuaga ukapera na kufunga ndoa.

Michael ambaye alikuwa mkazi wa River-Side, Ubungo jijini Dar, alikutwa na umauti baada ya kupata ajali mbaya huko Mwanga mkoani Kilimanjaro hivi karibuni, alipokuwa akielekea nyumbani kwa wazazi wa Vivian huko Karatu mkoani Arusha kwa ajili ya kukamilisha taratibu za ndoa ikiwemo kutoa mahari.

Michael ambaye alikuwa ni mwenyeji wa mkoani Mara alikuwa ameongozana na mchumba wake huyo pamoja na baba zake wadogo, wakiongozwa na Demetrius Mapesi ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ongo, Kimara jijini Dar.

BABA MDOGO AELEZA

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa masikitiko baba mdogo huyo, Demetius Mapesi ambaye yeye aliumia mdomo kwenye ajali hiyo na kushonwa nyuzi kadhaa alisema kuwa, tukio hilo lilijiri siku ya Ijumaa Kuu.

Alisema kuwa, ajali hiyo ilichukua uhai wa bwana harusi huyo mtarajiwa na mbaya zaidi alikuwa ameambatana na mchumba wake huyo ambaye alishuhudia mumewe huyo mtarajiwa akifariki dunia, jambo ambalo hawezi kulisahau.

SIMULIZI KAMILI

Alisimulia: “Nakumbuka tulikuwa safarini kuelekea huko wilayani Karatu nyumbani kwa wazazi wa msichana aliyekuwa akiendesha gari alikuwa ni bwana harusi mwenyewe.

“Ilipofika muda wa saa tatu usiku, wote tulijikuta tumepitiwa na usingizi na hapohapo ndipo ajali ilipotokea.

“Hakuna anayeweza kueleza hasa ni nini kilitokea kwa sababu ilikuwa ni ghafla na kila mmoja wetu alikuwa usingizini.”

WAGONGWA NA FUSO

Mapesi aliendelea kusimulia kuwa, baada ya gari ndogo walilokuwa nalo kugongwa na Fuso ambalo lilikuwa limebeba matikitimaji, walishtuka na kumuona dereva wa gari lao ambaye ndiye huyo bwana harusi akiwa na jeraha kubwa kichwani huku wenyewe wakiwa wameumia ambapo mmoja aliumia kwenye mdomo na mwingine miguuni.

WAPELEKWA KCMC

Alisema kuwa, baada ya ajali hiyo, walisaidiwa na wasamaria wema ambao waliwapeleka katika Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro, lakini kwa bahati mbaya, Michael alifariki dunia.

“Kiukweli inauma sana maana mchumba amefariki dunia na kutuachia majonzi makubwa kwani harusi yake ilikuwa ifanyike hivi karibuni.

“Tulishapanga kila kitu kuhusu harusi ndiyo maana Michael alikuwa anakwenda kupeleka posa na kutoa mahari moja kwa moja,” alisema Mapesi.

ALIKUWA MFANYAKAZI WA EXIM

Baba mdogo huyo aliendelea kueleza kuwa, Michael alikuwa akifanya kazi kwenye Benki ya I&M, Tawi la Posta jijini Dar ambapo alifanya kazi kwa mwaka mmoja tu kabla ya kukutwa na umauti huo.“Michael alizikwa katika Kijiji cha Kamkenga, Bunda mkoani Mara siku ya Jumanne wiki hii.

“Kwa upande wake Vivian, baada ya mazishi ya Michael alielekea kwao, Karatu kwa ajili ya kumuombolezea mchumba’ke huyo,” alisema Mapesi.

POLE VIVIAN

Risasi Jumamosi linatoa pole kwa ndugu wa marehemu Michael, Vivian, wazazi na familia yake kwa jumla. Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.


STORI: HAMIDA HASSAN NA GLADNESS MALLYA, DAR.



Chanzo:
Global Publishers
 
Niliiona yutube cku za nyuma. Kweli bwana harusi aliumia vibaya sana.
Tukirudi kwenye hali halisi: Je bwana harusi alikuwa amekomaa kuendesha masafa marefu?
Je alikuwa na uwezo wa kuendesha gari usiku?
Nawaasa madereva wapya wasipende kusafiri safari ndefu hasa usiku. Na ikitokea wakafanya hivyo waende mwendo wa taratibu. Hizi highways zimechukua maisha ya vijana wengi wasio na uzoefu wakijaribu kwenda makwao kuonesha mafanikio. Its a very sad story.
 
Thats why mm huww napenda kuanza dafari saa kumi au kumi na moja asubuh.Hii husaidia kufika sehemu nayotaka kwa wakati mzuri. Inaonekana kama jamaa waliondoka mapema basi walipumzika sana njiani. Au gari ilikua inasumbua
 
Walipitiwa na usingizi wote mpaka dereva? Sio uchawi huo, inawezekana bibi harusi au bwana harusi alimuahidi mtu kumuoa.
Si kweli kabisa..achana na imani potofu!Inawezekana walifunga vioo vya gari kuogopa baridi wakati pia hawakuwasha a/c na kusababisha hewa kuwa kidogo sana.Na kwa muda huo wanaweza kuwa walikuwa wametoka kula,sasa ni rahisi sana kupitiwa na usingizi tena ghafla.
Ila kwa vile sie wabongo na elimu zetu ni kama manyumbu,hutasikia tahadhari ya kufunga vioo inatolewa.Mfano mzuri ni kwenye basi,huwa vioo vikifungwa utaona watu wengi wanapata usingizi mzito sana!
Poleni wafiwa na bi arusi,Mungu awafanyie wepesi
 
Back
Top Bottom