Bw. Mkapa aliwahi kukutana na changamoto huko Kilimanjaro baada ya majimbo kadhaa kuchukuliwa na upinzani.
Watu wa maeneo hayo walianza kujenga dhana kuwa serikali ya Chama tawala haikuwa ikiupa mkoa huo fursa sawa na mikoa mingine kwa ajili ya upinzani kushika uongozi. Mkapa alichowajibu ni kuwa "nitateuaje waziri kutoka upinzani?"
Ni ukweli usiopingika kwamba uongozi wa kisiasa unaokuwa madarakani hupatwa na hofu dhidi ya maeneo ambayo chaguzi huonyesha uongozi huo hauungwi mkono. Hili limejitokeza kwa nguvu kubwa katika baadhi ya mikoa hapa Tz katika uchaguzi mkuu uliopita (2015), na yapo maeneo ambayo chama tawala kimeshindwa vibaya.
Upo umuhimu mkubwa wa kumtahadharisha Bw, Magufuli kuwa makini katika kuelekeza fursa na rasilimali zinazostahili kufanyiwa kazi kila pembe ya taifa na kuepuka hofu, jazba, kinyongo na kukomoana kwa sababu za kiitikadi.
Ikijatokea hali ya ubaguzi wa aina yoyote ile, madhara yake yanaweza kuleta mmomonyoko wa mshikamano wa kitaifa na yataisumbua jamii miaka nenda rudi.
Wananchi wa Kanda ya Ziwa Nyanza walimpa support kubwa sana Bw Magufuli, na si tatizo wakipewa nafasi stahiki za kisiasa. Lakini kwenye utendaji wa kiserikali ni muhimu kuunganisha nguvu za kitaaluma na kiuzoefu kutoka jamii zote ili kuwepo uwiano muafaka wa utekelezaji mikakati ya maendeleo.
Mwalimu Nyerere aliwahi sema, dhambi ya ubaguzi hujenga ubaguzi tena, ubaguzi zaidi, na ubaguzi hadi kiama.
Najaribu kutathmini mwenedo wa uteuzi wa Watendaji wapya wa Serikali unaoendelea..
Ninastahili kusahihishwa kama tathmini yangu ina upungufu!