Bw. Ludovick Utoh (CAG) uchunguzi wake ni kutaka kumfurahisha JK kama fadhila?

Yaani amejizalilisha kwenye taaluma yake na kuonyesha kumbe haata housegirl anaweza kazi auditor very stupid
 
Mkuu hayo maneno ni mazito sana!! Siyo kwamba amejidhalilisha yeye tu bali amewadhalilisha hao ambao tunaambiwa ni ma auditor na ni wataalamu. Inabidi wamchukulie hatua kwa kuwadhalilisha kiasi kwamba Mkuu umefikia kulinganisha kazi ya auditor na housegirl.
 
Nilikuwa namheshimu sana Ludovick kwa umakini wake na intergrity.
Nimefanya kazi naye muda mrefu sana uliopita alipokuwa NBAA, Bodi mambayo hata Mzee Mengi na wazito kama Sayore walikuwemo.
Lakini katika sakata hili amejichafua sana kwa uchafu aliojipaka kwa hili sakata la David Jairo.
Haingii akilini kuwa fedha ambayo ilichangwa na Idara za serikali, fedha ambazo hazina baraka ya Bunge , Katibu mkuu kiongozi na CAG wanasema hilo ni kawaida.
Huu ni wizi wa mchana na CAG ametumika kama toilet paper.
Msimamo wa wananchi mitaani ni kuungana na Bunge na Waziri Mkuu katika hili.
Ikulu imejivalisha joho la kondoo aliaye kutetea wananchi huku makucha ya mbweha yamejitokeza kupitia Katibu Mkuu wake Luhanjo.
Hii si picha nzuri hata kidogo.

Katuaibisha wahasibu wenzake kweli, nilipomuana kwenye ile movie was down coz ni kati ya vichwa vichache nilivyokuwa naviamini katika kulinda maadili yetu kama wahasibu
 
Mkuu hii ilikuwa special audit kama muda ulikuwa hautoshi angeomba kuongezewa muda si kutoa disclaimer. Hivi nini maana ya disclaimer labda mimi sijui nisaidie ili tuweze kuwa na mujadala ambao ni informed.

Hakuna suala la kunyongwa hapa. CAG alitakiwa atuambie pesa zilizokusanywa zilitumikaje ama walilipwa akina nani na siyo kusema tu kwmba zilikusanywa milliom 500 na wala si billion 1. Alitakiwa afanye mambo mengi zaidi ili kutufumbua macho. Sasa wacha kamati ifanye mambo yake na kama itafanya kwa mujibu wa kanuni na taratibu si ajabu ukaona CAG anaumbuka.

nakubali ya kuwa kuna mapungufu katika mfumo mzima wa nguvu za uhuru wa CAG kwani alichofanya luanjo ni amri kwa CAG na kilichopatikana kutokana na ukaguzi huu kiliwakilishwa kwa luhanjo mwenyewe

imefika wakati basi tuangalie vyombo vyetu na jinsi ya kuunda tume zetu na nafasi ya kiutendaji za wajumbe wa tume hizi, kwa mfano kitendo cha luanjo kuunda tume ya ukaguzi na kuipa agenda na namna ya kufanya kazi na muda wenyewe ilikuwa ni kosa la kiufundi ambalo lazima tuangalie ili lisije kutokea tena(bunge linatakiwa kurekebisha ili na kumpa uhuru zaidi CAG)

mimi nilidhani baada ya kutokea kwa tatizo ili basi luanjo alitakiwa kumwambie CAG kachunguze pasipo kumban akachunguze akaunti gani na zipi si za kuchunguza na nadhani yeye CAG angejua ni namna gani ya kufanya ukaguzi huu kwa maoni yangu angefanya(forensic
audit) na ambayo ingempa nafasi kuwa ya kusaka ushaidi wowote ndani ya akaunti za serikali na ata kwenda nje ya akounti za watu binafsi walioshiriki katika mgao huu wa fedha

nadhani pia tuangalie kuwa je ni haki kwa CAG kuambiwa amchunguze katibu mkuu wa wizara na ripoti hii pia amkabidhi katibu mkuu kiongozi?

kutokana na kutokuwa huru ndio mana ata komenti zake amekuja na majibu ya mkato kwa mfano mtu anakuambia moja kwa moja kaangalie kama fulani kaiba shs bilioni moja? katika ukaguzi list ya kazi zako nazo zinaweza kukubada uhueu wako. nadhani katika list za kazi zake angeambia (nenda kaangalie kama kuna upotevu wa fedha au matumizi mabaya) sio kuambia na kiasi kamili

kwa upande wangu naona CAG amefanya kazi hii kwenye mazingira magumu sana na sidhani kama kuna mtu ambae alinyimwa uhuru kama CAG katika tume hii na ni muda wa kuangalia ni namna gani ya kumpa uhuru

wito katika katiba mpya tuweke vipengele vya kumlinda na kumpa uhuru CAG, dhidi ya watumishi walio juu yake na ingefanyika vivyo hivyo kwenye mahakama zetu hili kuwe na uhuru wa kufanya kazi
 
Comment yangu kwa mtari wako wa mwisho nime ongezea

"wito katika katiba mpya tuweke vipengele vya kumlinda na kumpa uhuru CAG na kumkagua nae CAG, dhidi ya watumishi walio juu yake na ingefanyika vivyo hivyo kwenye mahakama zetu hili kuwe na uhuru wa kufanya kazi"
 
Unajua jamani tusiwe tunalaumu pasipo kujua kinachofanyika, someni kifungu cha 143 cha katiba mtaona yote! Utouh saiv muda wake wa u CAG umeisha,maana aliingia wkt sheria inasema cag asitaafu akiwa na miaka 60,ila ktk kipindi chake ndo ikaongezwa mpk miaka 65! Kwa sababu huwez kua madarakan na ukafaidi mabadiriko ya sheria,kwaiyo ilibidi utouh asitaafu miaka kma 2 au 3 nyuma! Anachofanya rais mpk sasa anampa mkataba wa mwaka 1 1 ili aweze kumcontrol kma saiv,mana saiv utouh hawezi kubishana na rais sbb akifanya hivyo apewi mkataba mpya!HILI LINA MNYIMA UHURU

Pia ofc ya NAO ni ya umma,huwezi ukawa ofc ya umma ukachunguza ofc za umma hizo hizo,ilibidi NAO ijitegemee ila mpk sasa mishahara,marupurupu na sheria ni sawa na za watu wa wizarani,hili pia lina mnyima uhuru CAG,imagine anaenda kukagua utumishi au hazina na anawapa hati chafu kama walivyotakiwa!unazan kitakachofuata ni nn?kama sio hizi ofc kuibana ofc ya cag????

Me nazan inabidi tupige kelele ili CAG apewe nguvu sana na awe independent ili hela zetu tujue zinaenda wapi na sio kulaumu tu bila kujua ttz nyuma!

Nihayo tu
 
Pia bado tukiangalia pamoja na hayo mapungufu yote niliyoaanisha hapo juu bado amefanya kazi nzuri yeye na ofc yake,ila niambie lini umesikia selikali wamefanyia kazi ushauri wake?

Nihayo tu
 
mimi nadhani hakuchemka ila ni kama yale ya Zombe. Unamchunguza mtu makosa famba hali wakijua hilo siyo kosa analotuhumiwa
 
Kusoma najua wabongo sio utamaduni wetu ila hata kusikiliza inakua sasa ni tabu.Utouh alisema shutuma za kwamba jairo kachangisha bilioni kupitia taasisi ishirini sio kweli ila ukweli ni kwamba jairo kachangisha five hundred million plus na ni kupitia taasisi tano.mengine alimuachia luhanjo aamue.sasa kosa lake ni lipi?
 
bunge linaweza kuunda kamati maalum au kupitia kamati za hesabu za serikali inaweza kuzipitia ripoti za CAG na kama kuna maeneo ambayo yanatakiwa ufafanuzi wanaweza kuiuliza serikali

pia lazima pia tutambue kuna udhaifu pia katika mfumo wetu wa kutoa maagizo kwa mfano Luhanjo aliweza kumuagiza CAG kufanya special auditing kwa siku kumi(10 days) pasipo kujua ugumu wa kazi yenyewe kwani kuna wakati ililazimu tume hii kwenda sehemu mbali mbali kati ya dar es salaam na dodoma na kisha wakae chini na kuandika ripoti , je unadhani zinatosha kufanya kazi vizuri

njia moja ya kupunguza na kuongeza udhibiti wa fedha za umma , CAG amepewa mamlaka ya kuchungua na kupeleka watuhumiwa mahakamani na kusimaia kesi , hii imepitishwa na bunge ili na inangoja saini ya rais kuanza kutumika

kwahiyo kama tukimpa power CAG ya kutosha na tukiongeza kipengele cha namna ya kuwajibishwa kwake
kwa mfano mimi naona wazi kuwa lazima tuongeze kipengele cha uteuzi wa CAG lazima uidhinishwe na bunge na baada ya kuteuliwa kumuondoa pia lazima bunge lishilikishwe sio kazi ya uteuzi wa CAG kufanywa na serikali pekee kwani mtu huyu anaikagua serikali kwahiyo lazima tumlinde dhidi ya serikali

kama CAG akipewa uhuru na nguvu naamini ubadhilifu utapungua sana

Nakubaliana na wewe Bw. Godwine na hasa kuhusu utoaji wa maagizo, hili nalo limekuwa tatizo katika serikali, magizo mengi ya serikali yamekuwa yanayolenga amakujinufaisha mtu binafsi au kujinufaisha kisiasa zaidi, tena ni maagizo yasiyojali utafiti,tathmin na uhalisia. mifano ni mingi tu JK=kubomolewa kwa uzio, Pinda+JK=Kuzuia bomoa bomoa NK. Vilevile hapo kwenye RED ni matumaini mapya kwa watanzania lakini nina wasiwasi na utekelezaji wake maana Tanzania n iwazuri wa kutengeneza sera,sheria na kanuni nzuri ambazo mwisho wa siku hatuzitekelezi!
 
<font size="4"><span style="font-family:book antiqua;">

Me naunga na wewe kwanye hiyo hoja yako Huko Halimashauri ndiko pesa zinakotumika kuna mtu mmoja aliniambia pia tusiwalaumu sana TRA kwa ukusanyaji wao wa kodi wanakubali ndio kuna mapungufu ila nao wanahoji kwa kile hata wanacho kikusanaya je huko kiendako wanachunguza matumizi yake wanao tumi hizo pesa esp kwenye hizo Halmashauri wanakaguliwa ? Je hizo semina watu wanapelekwa zinachunguzwa kweli ni semina?? watu wanapelekwa semina na pesa ya serikali eg South Afrika then after two weeks mtu yuko Mwanza unamuuliza vipi anakujibu hakuna kitu huko ngoja nipotezee muda hapa then nirudi dar nikapokee posho yangu sasa hapo ndipo pesa hupotea hiz semina semina na training za ajabu za kubangwa waweza kuta budget ya idara fulani ni posho tu za idara fulani hapo hamuoni na ndio maana wengi wana mpigia kelele CAG kuwa watu wake wa chini ni wachafu sana na haya yote yana toka huko waendako kukagua.

My Take:

Kwa upande mwingine CAG anatakiwa kuwa makini katika utendaji wake kwani wananchi wengi wanayaona haya kuko wilayani na mikoani wakati wa ukaguzi.

Kuwe na chombo kingine cha kumkagua CAG hizo report zake kikatiba na kisheria ndipo kutakuwa na mstari uliyo nyoooka katika hizo report za ukaguzi

Kaka! haya mambo wanayajua, yote kabisa! tatizo ni hao waliopewa mamlaka ya kuwajibisha wanakosa ujasiri wa kufanya hivyo maana na wao ni sehemu ya tatizo, kwani hujawahi kusikia upande wa polisi na uhamiaji, afisa anapangiwa mahala asipokuwa anamkumbuka mzee anahamishwa ,mara moja tena wakati mwingine anahamishiwa makao makuu wao wanaita kukalia bench!
 
Unajua jamani tusiwe tunalaumu pasipo kujua kinachofanyika, someni kifungu cha 143 cha katiba mtaona yote! Utouh saiv muda wake wa u CAG umeisha,maana aliingia wkt sheria inasema cag asitaafu akiwa na miaka 60,ila ktk kipindi chake ndo ikaongezwa mpk miaka 65! Kwa sababu huwez kua madarakan na ukafaidi mabadiriko ya sheria,kwaiyo ilibidi utouh asitaafu miaka kma 2 au 3 nyuma! Anachofanya rais mpk sasa anampa mkataba wa mwaka 1 1 ili aweze kumcontrol kma saiv,mana saiv utouh hawezi kubishana na rais sbb akifanya hivyo apewi mkataba mpya!HILI LINA MNYIMA UHURU

Pia ofc ya NAO ni ya umma,huwezi ukawa ofc ya umma ukachunguza ofc za umma hizo hizo,ilibidi NAO ijitegemee ila mpk sasa mishahara,marupurupu na sheria ni sawa na za watu wa wizarani,hili pia lina mnyima uhuru CAG,imagine anaenda kukagua utumishi au hazina na anawapa hati chafu kama walivyotakiwa!unazan kitakachofuata ni nn?kama sio hizi ofc kuibana ofc ya cag????

Me nazan inabidi tupige kelele ili CAG apewe nguvu sana na awe independent ili hela zetu tujue zinaenda wapi na sio kulaumu tu bila kujua ttz nyuma!

Nihayo tu

Binafsi nimekuelewa bwana Madched! lakini Dah! safari bado ni ndefu nahisi kukata tamaa vile! haya bwana.
 
Mnashanga nini kuhusu CAG? Kiongozi Mtanzania aseme ukweli? Haijawahi kutokea katika hadithi zote za kuumbwa kwa Tanganyika. Labda miujiza itokee!!
 
Kusoma najua wabongo sio utamaduni wetu ila hata kusikiliza inakua sasa ni tabu.Utouh alisema shutuma za kwamba jairo kachangisha bilioni kupitia taasisi ishirini sio kweli ila ukweli ni kwamba jairo kachangisha five hundred million plus na ni kupitia taasisi tano.mengine alimuachia luhanjo aamue.sasa kosa lake ni lipi?

Mkuu hayo yote sawa. Ni kweli aligundua kwamba zilichangishwa million 500 na siyo billion moja lakini mtoas tuhuma yeye alienda mbali zaidi akasema hizo pesa zilichangishwa kwa ajili ya kuwahonga wabunge ili wapitishe budget. Sasa na huyu mkaguzi alikuwa natakiwa atuambie hizo million 500 zilitumikaje? Yeye ni mtaalamu wa mahesabu ya fedha? Kutuambia tu kwamba zilikusanywa million 500 na siyo billion moja ni upupu.
 
mheshimiwa kuna kitu nadhani watu wengi wanashindwa kuelewa katika kusoma auditing report

CAG ametoa
Disclaimer of Opinionhii inamaanisha kutokana na muda na kazi yenyewe bado kuna vitu havijakamilika kwani disclaimer opinion inatolewa kama upitiaji wa ukaguzi haujakamilika au ameshindwa kutoa coment kutokana na vielelezo alivyovipitia,

kama CAG angetaka kumsafisha basi angetoa UNQUALIFIED OPINION hii ingeonyesha moja kwa moja kwamba jairo amefuata sheria na hakuna makosa.

kama CAG angetoa QUALIFIED opinion hii ingeonyesha kuwa jairo moja kwa moja amefanya makos katika utekelezaji wa kazi na record zake

mbali na general comment kuna vipengele ndani ya report CAG amekoment kwamba kuna mismanagement of public fund hii inaonyesha kuwa sheria za utunzwaji wa fedha za serikali hazikufuatwa

hivyo basi kabla ya kusoma ripoti tuepuke kumuhukumu CAg kwa kusikiliza maneno ya mtu mwingine bali tujenge tamaduni za kusoma riport zenyewe ndio tumuhukumu CAG

Asante ndugu mtaalamu..........kosa lake ni kukubali kuitoa hiyo disclaimer of opinion kwa public badala ya client wake (Rais) ambaye naye alitakiwa kuwaambia stakeholders wa nchi (raia)......ambaye hakufanya hivyo.........Luhanjo has no right to speak about audit issues
 
kuna kitu tunatakuwa tujue , pindi CAG anapofanya auditing za kwawaida ndio utaratibu wa kawaida unafuatwa. lakini alichokifanya pale ni special audit na yeye alikuwa ni kiongozi wa tume iliyoundwa na luhanjo sasa basi huwezi kupewa kazi na tume iliyoundwa na luhanjo then ukatae kumpa ripoti yeye aliyeunda tume hii. lilikuwa ni jukumu la luhanjo kama yeye hastahili kusoma basi ampelekee bosi wake na si CAG,

CAG alifanya kazi kama tume na majibu ya tume mara nyingi kama si zote yanapelekwa kwa aliyeunda Tume
 
Kwa hiyo haikuwa AUDIT REPORT bali COMMISION OF INQUIRY REPORT?.....kama ni hivyo ni sawa....nilelewavyo mimi CAG hateuliwi na hawajibiki kwa LUHANJO.......kwa hiyo hakuna client-audit relation hapo
 
kwahiyo unataka kusema luhanjo hakuwa na mamlaka ya kuunda tume ile? na kama yes kwanini?
 
Back
Top Bottom