Bw. Ludovick Utoh (CAG) uchunguzi wake ni kutaka kumfurahisha JK kama fadhila? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bw. Ludovick Utoh (CAG) uchunguzi wake ni kutaka kumfurahisha JK kama fadhila?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng`wanantogwa, Aug 28, 2011.

 1. Ng`wanantogwa

  Ng`wanantogwa Member

  #1
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna tetesi kwamba Bw. Ludovick Utoh amepoteza uwezo na ujasiri wa kuibua ubadhilifu wa fedha za serilkali na kuchunguza usahihi wa matumizi ya fedha za serilkali na mashirika ya umma kwa sababu tayari alishamaliza muda wake na kuongezewa muda mara mbili.

  Kwa nafasi ya Bw. Utoh ni mtu anayepaswa kufanya kazi kwa uzalendo mkubwa sana maana watanzania wamempa dhamana kubwa, sijui kama mnafahamu kuna nyazifa kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais ana uwezo wa kuteua tu lakini hana uwezo wa kuachisha yeye kama yeye bali itakuwa hivyo kupitia jopo la majaji kadhaa wakiwemo wengine kutoka nchi za jumuiya ya madola? nyazifa hizo ni pamoja na CAG na JAJI MKUU.

  Kinachofanyika sasa Bw Utoh anataka kumsaidia na kumfurahisha Mhe, Rais Kikwete na serikali yake isiendelee kupata wakati mgumu lakini vile vile kuongezewa tena muda mwingine pengine amalize kabisa awamu hii ya pili ya JK. Lakini pia tetesi zinasema Bw. Jairo na mhe Rais ni maswahiba wa siku nyingi tangu bwana Jairo akifanyia kazi ikulu pale magogoni.

  Ndugu zangu, ikiwa hizi ni tetesi najua fika humu ndani kuna Great thinkers na kuna watu wenye first hand information nitafurahi kusikia zaidi.Nawasilisha.
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,640
  Likes Received: 2,576
  Trophy Points: 280
  Nani asiyejua kuwa kikwete anachagua watendaj kwa ushkaj.
   
 3. K

  Kibanikolo Member

  #3
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli 8wana ludowick utoh, amekuwa akifanya kazi zake kitaalaam na hajawahi kulaumiwa .naomba tusubiri kamati ya bunge. Ndio umhukumu
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kwa siasa za kibongo bongo INAWEZEKANA CAG kwisha kazi kaingia kwenye inner circle
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,126
  Likes Received: 2,289
  Trophy Points: 280
  Kwa hili la jairo CAG kachemkaaaaa!!!
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,367
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mheshimiwa kuna kitu nadhani watu wengi wanashindwa kuelewa katika kusoma auditing report

  CAG ametoa
  Disclaimer of Opinionhii inamaanisha kutokana na muda na kazi yenyewe bado kuna vitu havijakamilika kwani disclaimer opinion inatolewa kama upitiaji wa ukaguzi haujakamilika au ameshindwa kutoa coment kutokana na vielelezo alivyovipitia,

  kama CAG angetaka kumsafisha basi angetoa UNQUALIFIED OPINION hii ingeonyesha moja kwa moja kwamba jairo amefuata sheria na hakuna makosa.

  kama CAG angetoa QUALIFIED opinion hii ingeonyesha kuwa jairo moja kwa moja amefanya makos katika utekelezaji wa kazi na record zake

  mbali na general comment kuna vipengele ndani ya report CAG amekoment kwamba kuna mismanagement of public fund hii inaonyesha kuwa sheria za utunzwaji wa fedha za serikali hazikufuatwa

  hivyo basi kabla ya kusoma ripoti tuepuke kumuhukumu CAg kwa kusikiliza maneno ya mtu mwingine bali tujenge tamaduni za kusoma riport zenyewe ndio tumuhukumu CAG
   
 7. simtami

  simtami Member

  #7
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 22, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakumbuka kuna mtu tulikuwa na Canada Amerika alifanana jina kama huyu jamaa Ludovick Uttouh nakumbuka yeye alikuja pale ubalzini akaniambia anasoma kozi ya CERTIFIED INDUSTRIAL MANAGEMENT kwa kifupi ni CIMA ambayo inahusu mambo ya utawala wa viwanda ina maana amebobea katika kupanga nani afanye nini na kwa wakati gani na kwa resources gani huku akiamini kwamba kwa mpango alioutoa utazalisha nini kwa nafasi yako. Hii elimu aliyonayo kwa miaka ile Tanzania ilkuwa very sophiscated kweli,nahisi mpaka sasa hivi inawezekana Tanzani haiawahi kupeleka watu kusoma kozi kama hizo au kufanya mitihani kama hiyo katika mambo ya utawala cheti hicho ni kama leseni ya juukabisa ya utawala ambayo yenyewe ina kiapo chake.Sidhani kama yeye binafsi alivyopata cheti hicho kulikuwa na haja kuja kuanza kusomea uhasibu kwani hao wahasibu wenye CPA, ACCA, PGDA, ADA, ATECH na Certificates za uhasibu ana uwezo mkubwa sana wa kuwapangaia kazi kutokana na mahitaji ya kazi inataka nini ,kwa hiyo matokeo ya kazi yatategemea jinsi alivyowapanga watu hao,kwa hiyo kwa taaluma yake hana sababu ya kuchoka kwani yeye hafanyi uhasibu wowote pale ila anapanga watu kutokana na mahitaji ya kazi ukichunguza utagundua hao anaowapangangia kwenda huko ndio wanaotoa jibu .Leo Nakumbuka miaka ya zamani wakati shirika la usafifiri Daresalaam (UDA) ulikuwa ukipanda huna nauli kondakta anakushika utabaki kwenye basi mpaka jioni basi linavyorudi ubungo unakwenda nalo huko mtakutana wengi tu nao wamekamatwa mnapewa kazi ya kuosha mabasi yote yanaoanza kazi kesho yake asubuhi utaondoka na basi linalokwenda njia yako hata majumbani watu walikuwa wanajua usiporudi usiku wanajua utakuwa ulipandabasi huna nauli kwani ukifika nyumbani unaweza sahahau ukaingia umekunja suruari na viatu vina maji,basi inakuwa siri yenu tu, sasa hawa inawezekana hawakufanya kazi tuliyoitarajia wamebakizwa kusafisha mabasi kwani walikuwa kuwa kwenye utumishi wao vitu walivyotakiwa kuvificha wao walikuwa wanaibuka navyo ovyo ovyo mbele ya waTanzania mzee alikuwa hapendi vile ndo maana Luhanjo mpaka sasa kwenye takwimu haonyeshi kama alisha chukua hatua hata kwa Mkurugenzi mmoja wa Halmashauri ambao ripoti za CAG zinaonyesha ndo walaji wakubwa wa fedha za umma.
   
 8. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,753
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwa mtizamo wako.uwezo wake umeshuka mkuu kwa hili
   
 9. Ng`wanantogwa

  Ng`wanantogwa Member

  #9
  Aug 29, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekupata Bw Godwine asante kwa kueleza kwa weledi, lakini tambua kabisa mtu mwenye dhamana kubwa kama Bw. Utoh anapaswa kuwatizama watanzania na kuwahurumia sana na kisha bila kuyumbishwa na waliomuweka hapo aokoe fedha nyingi za serikali zinazopotea kwenye halimashauri zetu; mi nadhani ni Dr. Magufuli tu katika mawaziri wa JK ndo mwenye uthubutu wa kuwajibisha walio chini yake, hata kama Bw Utoh hausiki moja kwa moja katika kuwawajibisha wezi wa fedha za serikali, lakini kuna taarifa kwamba wakaguzi wake wanapokwenda kukagua katika halimashauri wanapewa bahasha, wanajaziwa mafuta, wanalipiwa hotel, kuna ukaguzi hapo? au ndo mwendo wa hati safi kila kukicha! hawezi kuwawajibisha.

  Hivi niulize swali mtanisaidia, ripoti za ukaguzi zinapotolewa na ofisi ya CAG ni chombo gani kingine chenye mamlaka na utaalamu kinafanya cross
  checking kujiridhisha? sheria ama katiba inatamka nini eneo hilo? Hivi unajua kwenye halimashauri zetu kuna madudu mengi sana yanafanyika na yako wazi kabisa fedha zinaliwa,ukaguzi unafanyika, hakuna hatua zinazochukuliwa! hati safi zinatolewa! kwani pesa za MMEM na MMES zimefika wapi? au CAG hawajibiki kuzikagua?

  Si muda mrefu ajali zitahamia madarasani tumesikia sana ajali za barabarani sasa zinakuja za madarasani wanafunzi kuangukiwa na kuta za madarasa kutokana na ujenzi wa hovyo ,pesa zimeliwa matofali yana uwiano hafifu wa simenti na mchanga! tutasikia wanafunzi wanazama na vyoo, ni miradi mingi sana tazama majengo ya hospitali, mabwawa ya maji. Miradi yote hii pesa zake zinatoka serilkali kuu hata kama zingine serikali imezipata kama mkopo au msaada, ofisi ya mkaguzi mkuu ndo yenye mamlaka kujua pesa hizi zimetumikaje. Ndugu zangu mambo hayafanyiki sababu za kujuana, Rushwa na uchu wa madaraka, Pamoja na kwamba unasema Bw. Godwine nisimhukumu CAG lakini napotazama mambo hayo sioni ni kwanini nisimhukumu, yeye akifanya kazi kama inavyopaswa hakika wabadhilifu wote wa pesa za serikali wataishia jela na wengine hawataiba au watapungua basi.
   
 10. G

  Godwine JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,367
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145


  bunge linaweza kuunda kamati maalum au kupitia kamati za hesabu za serikali inaweza kuzipitia ripoti za CAG na kama kuna maeneo ambayo yanatakiwa ufafanuzi wanaweza kuiuliza serikali

  pia lazima pia tutambue kuna udhaifu pia katika mfumo wetu wa kutoa maagizo kwa mfano Luhanjo aliweza kumuagiza CAG kufanya special auditing kwa siku kumi(10 days) pasipo kujua ugumu wa kazi yenyewe kwani kuna wakati ililazimu tume hii kwenda sehemu mbali mbali kati ya dar es salaam na dodoma na kisha wakae chini na kuandika ripoti , je unadhani zinatosha kufanya kazi vizuri

  njia moja ya kupunguza na kuongeza udhibiti wa fedha za umma , CAG amepewa mamlaka ya kuchungua na kupeleka watuhumiwa mahakamani na kusimaia kesi , hii imepitishwa na bunge ili na inangoja saini ya rais kuanza kutumika

  kwahiyo kama tukimpa power CAG ya kutosha na tukiongeza kipengele cha namna ya kuwajibishwa kwake kwa mfano mimi naona wazi kuwa lazima tuongeze kipengele cha uteuzi wa CAG lazima uidhinishwe na bunge na baada ya kuteuliwa kumuondoa pia lazima bunge lishilikishwe sio kazi ya uteuzi wa CAG kufanywa na serikali pekee kwani mtu huyu anaikagua serikali kwahiyo lazima tumlinde dhidi ya serikali

  kama CAG akipewa uhuru na nguvu naamini ubadhilifu utapungua sana
   
 11. Majoja

  Majoja JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 610
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nilikuwa namheshimu sana Ludovick kwa umakini wake na intergrity.
  Nimefanya kazi naye muda mrefu sana uliopita alipokuwa NBAA, Bodi mambayo hata Mzee Mengi na wazito kama Sayore walikuwemo.
  Lakini katika sakata hili amejichafua sana kwa uchafu aliojipaka kwa hili sakata la David Jairo.
  Haingii akilini kuwa fedha ambayo ilichangwa na Idara za serikali, fedha ambazo hazina baraka ya Bunge , Katibu mkuu kiongozi na CAG wanasema hilo ni kawaida.
  Huu ni wizi wa mchana na CAG ametumika kama toilet paper.
  Msimamo wa wananchi mitaani ni kuungana na Bunge na Waziri Mkuu katika hili.
  Ikulu imejivalisha joho la kondoo aliaye kutetea wananchi huku makucha ya mbweha yamejitokeza kupitia Katibu Mkuu wake Luhanjo.
  Hii si picha nzuri hata kidogo.
   
 12. T

  Tata JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,586
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Ili tuweze kuchangia vyema inabidi tuisome hiyo ripoti kuelewa nini hasa kimeandikwa. Vinginevyo tutaishia kusambaza tetesi tu na sidhani kama tukifanya hivyo tutakuwa tunaitendea haki Forum yetu.
   
 13. T

  Tata JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,586
  Likes Received: 527
  Trophy Points: 280
  Kuna maadili kwenye taaluma ya uhasibu na ukaguzi na moja wapo ni kuwa katika kila kazi unayofanya lazima ujiridhishe kuwa umetekeleza wajibu wako wa kitaaluma kwa uangalifu - due professional care. Maana yake ni kuwa kama unadhani kuwa muda hautoshi au hauwezi kupata taarifa za muhimu kukamilisha kazi yako ni vyema ukaliweka hilo wazi na ikiwezekana ukamshauri aliyekupa kazi aongeze muda wa kuifanya kazi hiyo. Vilevile maadili yanawataka wanataaluma wa uhasibu na ukaguzi kukiri pale ambapo hawana uwezo wa kufanya kazi waliyopewa na kuomba msaada zaidi. Ni makosa kitaaluma kukubali kazi ambayo huna uwezo wa kuifanya kwa ukamilifu.


  Hivyo suala la muda haliwezi kuwa kisingizio cha CAG kufanya kazi ya kiwango cha chini kwani alikuwa na fursa ya kumweleza aliyempa kazi kuwa asingeweza kumaliza kazi aliyopewa ndani ya muda mfupi kiasi hicho. Kwa kuwa alikubali basi tunachukulia kuwa aliamini kuwa alikuwa na uwezo wa kuimaliza kwa muda aliopewa.
   
 14. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katika kipindi cha hivi karibuni Ludovick amechemka sana katika fani yake, amepoteza mwelekeo ndiyo maana Halmashauri nyingi zinapewa Hati safi wakati watumishi wake wamekula pesa za umma, miradi ya maendeleo haitekelezeki wamekalia wizi tu. Tunamwomba aachie ngazi.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,469
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  CAG ni mwajiriwa wa Serikali kama alivyo Jairo. Baadhi yetu tunakataa kabisa ofisi ya UMMA kama ilivyo NAO na CAG wake kufanya ukaguzi kwenye ofisi za UMMA kama mawizara, mashirika ya UMMA, wakala za serikali,....
  Tulikuwa na TAC zamani. Mashirika yote ya UMMA yakafa huku inayakagua kila mwaka!
   
 16. G

  Godwine JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,367
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  unachanganya kama muda hautoshi basi kuna taratibu ikiwemo kutoa disclaimer of opinion ambavyo amefanya sasa wananchi kukaa na kusema kwa kumsikiliza luhanjo sio kusoma ripoti yake nayo tatizo

  kuna comenti zake za mismanagement of public fund ambayo luhanjo amesema si Fraud so nini tene mnataka toka kwa CAG au mnataka aseme jairo anyongwe?
   
 17. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  naona kuna mawazo mazuri
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Aug 29, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,863
  Likes Received: 1,640
  Trophy Points: 280
  Mkuu unawezekana ukawa ni mhasibu lakini utumiaji wa maneno hayo hujautendea haki. Nina maana ya maneno kama disclaimer, qualified opinion, unqualified opinion. Hayo maneno ni too general na huwa hayatoi mwanga mzuri katika kuonyesha matatizo ya taasisi. Na maneno hayo huwa yanatumika katika ukaguzi wa kawaida. Na ukitaka kupata ni matatizo gani yapo kwenye taasisi unatakiwa uangalie management letter na siyo opinion ambayo huwa ni too general.

  Katika suala hili kazi ya Utoh ilikuwa ni special audit ambayo inakuwa na terms of reference. Hapa Utoh alitakiwa aangalie hizo hadidu za rejea na kuona kama zinamuwezesha kufanya kazi yake ya ukaguzi maalumu na kuikamilisha kwa muda unaotakiwa na kujiridhisha kuwa atafanya kazi yake kitaalam without limitation of scope. Hivyo angetoa profession opinion kwenye hadidu za rejea na kama angeona kuwa kwa profession yake hadidu za rejea alizopewa zisingemfikisha kokote angeamua kuacha hiyo kazi (resign) - na hii inaruhusiwa kwa mujibu wa taaluma. Kwa kutoa disclaimer of opinion ina maana alichokuwa anakagua hakikaguliki!!! Inabidi tutenganishe kati ya Routine Audit na Special Audit/Investigation.

  Utoh hajatenda haki labda tusubiri haki toka kwa tume ya Bunge ambayo nayo nina shaka kwa kuwa inaaminika pesa huwa zinachangishwa ili kuwalainisha wabunge wakati wa kupitisha budget sasa kwa wao kujichunguza kuwa huwa wanakula, naona shaka. Tusubiri labda wanaweza kujikaanga kwa mafuta yao wenyewe kama sangara.

   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  Aug 29, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 12,863
  Likes Received: 1,640
  Trophy Points: 280
  Mkuu hii ilikuwa special audit kama muda ulikuwa hautoshi angeomba kuongezewa muda si kutoa disclaimer. Hivi nini maana ya disclaimer labda mimi sijui nisaidie ili tuweze kuwa na mujadala ambao ni informed.

  Hakuna suala la kunyongwa hapa. CAG alitakiwa atuambie pesa zilizokusanywa zilitumikaje ama walilipwa akina nani na siyo kusema tu kwmba zilikusanywa milliom 500 na wala si billion 1. Alitakiwa afanye mambo mengi zaidi ili kutufumbua macho. Sasa wacha kamati ifanye mambo yake na kama itafanya kwa mujibu wa kanuni na taratibu si ajabu ukaona CAG anaumbuka.
   
 20. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  <font size="4"><span style="font-family:book antiqua;">
  Me naunga na wewe kwanye hiyo hoja yako Huko Halimashauri ndiko pesa zinakotumika kuna mtu mmoja aliniambia pia tusiwalaumu sana TRA kwa ukusanyaji wao wa kodi wanakubali ndio kuna mapungufu ila nao wanahoji kwa kile hata wanacho kikusanaya je huko kiendako wanachunguza matumizi yake wanao tumi hizo pesa esp kwenye hizo Halmashauri wanakaguliwa ? Je hizo semina watu wanapelekwa zinachunguzwa kweli ni semina?? watu wanapelekwa semina na pesa ya serikali eg South Afrika then after two weeks mtu yuko Mwanza unamuuliza vipi anakujibu hakuna kitu huko ngoja nipotezee muda hapa then nirudi dar nikapokee posho yangu sasa hapo ndipo pesa hupotea hiz semina semina na training za ajabu za kubangwa waweza kuta budget ya idara fulani ni posho tu za idara fulani hapo hamuoni na ndio maana wengi wana mpigia kelele CAG kuwa watu wake wa chini ni wachafu sana na haya yote yana toka huko waendako kukagua.

  My Take:


  Kwa upande mwingine CAG anatakiwa kuwa makini katika utendaji wake kwani wananchi wengi wanayaona haya kuko wilayani na mikoani wakati wa ukaguzi.

  Kuwe na chombo kingine cha kumkagua CAG hizo report zake kikatiba na kisheria ndipo kutakuwa na mstari uliyo nyoooka katika hizo report za ukaguzi
   
Loading...