BVR Kilosa madudu tupu

mysee

Member
Apr 4, 2014
74
9
Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa imefanya ubabaishaji katika mchakato wa kupata wanaostaili kufanya kazi ya BVR baada ya kutoa tangazo la nafasi ya kazi hii kinyemela na kutoelekeza waombaji kuambatanisha vyeti vyao vya it kama halmashauri nyingine zilivyo fanya.

Hili limepelekea kuwaacha watu wengi wenye sifa za kufanya kazi, Wilaya hii ubabaishaji umechukua nafasi kubwa sana kuliko utaalamu.

Jambo hili limesha itia serikali hasara kwakuwa mara ya kwanza ulifanyika ubabaishaji katika zoezi la vitambulisho vya Taifa wakatumia watu hawa hawa ambao baadhi yao bado wapo hatua ya kutumia penseli wakaboronga leo hii mchakato unarudiwa.

Tutafika?
 
Mimi nimeshangaa kuona laptop wanayotumia ni aina ya Accer na siku zote tumeaminishwa kuwa computer kwa ajir ya matumiz ya serikal ni Dell, Hp companq au Toshiba.
 
Kilosa katika ubora wake,sijui kwanini hiyo wilaya,halafu naona kama ni wilaya ambayo haimulikw mulikw na serikali kuu......poleni wana Kilosa,wasalimie wana Mkwatani,Magomeni,Muhomwa,Kichangani,Mtendeni.....I miss the place
 
Ndivyo walivyo kilosa kila kitu uwanajfanya wajua kuchakachua
madiwani wenyewe wa Kilosa washajikatia tamaa kabisaaa,haya watendaj wameamua kuwa wapigaj,leo hii wilaya kibao zinasonga mbele yaan kilosa inashuka tu,jamani inashangaza sana,
 
Ni kweli kwa huu mchakato unafanyka kbabaishaj sna mm nliomba hapa dumila tena nna sifa zote lakn majna yametoka holaa
 
Ivi iyo kilosa c ndiyo mjini yao kwa wenyeti ccm hawakuambulia hata kiti ki1?
 
Mimi nimeshangaa kuona laptop wanayotumia ni aina ya Accer na siku zote tumeaminishwa kuwa computer kwa ajir ya matumiz ya serikal ni Dell, Hp companq au Toshiba.

Tambua kuwa mashine zimeagizwa kama complete set zikiwa na kompyuta tayari, huenda mtengenezaji wa bvr ana mkataba na acer na sio kampuni nyingine kama dell, toshiba,nk. Kwa hali hiyo serikali ingekwepea wapi? Licha ya hivyo je acer zimesababisha tatizo lolote?
 
Back
Top Bottom