Mfwatiliaji
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 1,323
- 67
Wananchi sasa waibana Buzwagi
Na Patrick Mabula, Kahama
SAKATA la baadhi ya wanakijiji wenye mali wakiwamo wachimbaji wadogo katika mgodi wa Buzwagi ambao walishagoma kupokea fidia kutoka kampuni ya Barrick kwa madai kuwa wanapunjwa na kwenda mahakamani, wamegoma kuondoa shauri hilo baada ya kutakiwa kufanya hivyo na Serikali.
Wananchi hao wapatao 30 walisema juzi kuwa wamegoma kulitoa shauri hilo kortini, baada ya kuombwa kufanya hivyo ili waelewane nje ya Mahakama na mwekezaji huyo.
Wasimamizi wa madai hayo mahakamani, Bw.Omary Sekerume, Bw. Lameck Makoye na Bw. Issa bin Issa walisema katika kikao na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Brigedia Jenerali Yohana Balele aliwataka kulitoa shauri hilo mahakamani.
Walisema baada ya kuombwa na Mkuu wa Mkoa katika kikao hicho, kuondoa shauri la madai ya fidia walilopeleka mahakamani, baada ya kutoridhishwa na fidia inayotolewa na Barrick kupitia kampuni ya Pangea Minerals, walikataa.
Aliyevumbua dhahabu katika eneo la Buzwagi, Bw.Yahya Bundala, ambaye ni mmoja wa waliokataa kupokea fidia hiyo, alisema waliamua kwenda mahakamani baada ya kutoridhishwa na fidia katika mali zao yakiwamo mashimo ya dhahabu waliyokuwa wanachimba, mashamba, miti, nyumba na makaburi ya ndugu zao.
Bw. Sekelume alisema hawakubali fidia ya sh. 200,000 kwa kila shimo walilokuwa wakichimba dhahabu na sh. 120 kwa meta moja ya mraba ya kila ardhi ya mashamba yao zikiwamo mali mbalimbali.
Alisema wao wanataka Pangea iwalipe fidia ya kila shimo kiasi cha sh. milioni 25 sehemu za maosheo walipokuwa wakikamulia dhahabu, sh. milioni 40 na kila meta moja eneo ya mashamba yao iwe kiasi cha sh. 4,941.
Katika barua iliyotoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama aliyowaandikia yenye kumbukumbu namba cb 75/143/01/3 ya Julai 13 mwaka huu, aliwataka wananchi hao kusaini barua za makubaliano ya fidia ya mali zao na kupisha eneo la Buzwagi kitu ambacho walikipinga.
Aidha, kwenye eneo la mgodi wa Buzwagi zaidi ya watu 538 wanatakiwa kulipwa fidia katika mradi huo, ambapo kati yao tayari wameshalipwa kiasi cha sh. milioni 72.8 ingawa bado kundi la wakijiji na wachimbaji wadogo wapatao 30 bado wamegoma na kuamua kwenda mahakamani.
Awali, Meneja Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold Tanzania, Bw. Deo Mwanyika katika taarifa yake aliyoitoa hivi karibuni kwa Rais Jakaya Kikwete alipotembelea Buzwagi, alisema mgogoro na watu hao upo kwa waliokataa kupokea fidia.