Buying and selling of used books | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Buying and selling of used books

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rich Dad, Dec 16, 2010.

 1. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wadau hili ni jukwaa ambalo unaweza ukaweka ideas zako zozote za kibiashara, ambapo hata kama wewe utashindwa kuifanya inawezekana ukamwezesha mwezio ambaye ana capital lakini hana idea.

  Hivyo basi kuna hili jambo ambalo nimekuwa nikilifikiria kwa muda mrefu ambalo nadhani linaweza kufanyika ili ku-improve biashara ambazo labda zipo zinaendelea ila mimi sijui.

  Nianze kwa kuwapatia utangulizi:

  Tanzania bado tuna uhaba mkubwa wa vitabu vyuoni, na hasa elimu ya juu ...hivyo hii biashara imetarget zaidi vyuo. Uhaba wa vitabu unatokana na gharama za vitabu vyenyewe na wakati mwingine upatikanaji wa vitabu vyenyewe unakuwa mgumu.

  Hivyo hii biashara inaeza kufanyika kwa mfumo wa kutengeneza online bookstore ambayo itawezesha kuwakutanisha Buyers na Sellers wa ndani ya Tanzania tu!, Sellers anaweza kuwa mtu yeyote ambaye anataka kuuza kitabu chake ambacho kakitumia kwa muda na akihitaji tena kwa wakati huo. Buyers watakuwa ni wanafunzi ambao wanahitaji baadhi ya vitabu ambavyo huenda hawapo kwenye position ya kununua kwa wakati huo.

  Siku za mwanzo inabidi kufanya promotion ya nguvu maeneo ya vyuo ...na kwa kuanzia nadhani ni hapahapa dar es salaam. Wanafunzi waliopo mwaka wa mwisho wenye kumiliki vitabu ni rahisi kukuuzia kama utawapa bei nzuri, then nawe unakuja kuwauzia wale wanohitaji kwa bei juu kidogo but ya chini compared na kitabu kipya.

  NB: - Kuna watakao beza kwa kusema hii idea ni sawa na kinachofanyika amazon.com, but jiulize ni watanzania wangapi wanaotumia facility za amazon?
  - Challenge nyingine kwenye biashara hii ni kutokana na iledhana iliyojengeka kwamba...ukitaka kumfumba kitu mtanzania weka kwenye maandishi
  - Changamoto nyingine ni kwamba watu wengi huwa wana-violate copyrighting rules kwa kutoa photocopy au kuscan bila permission ya mtunzi.

  Yeyote mwenye mchango ambao ni constructive anakaribishwa kuchangia.
   
 2. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,869
  Likes Received: 2,813
  Trophy Points: 280
  Mimi natafuta yule anayeweza kununua vitabu vilivyopitwa na wakati. Nina duka la kuuza vitabu sasa kuna vitabu ambavyo vilipitwa na wakati baada ya kubadilishwa kwa mitaala ya shule za msingi si mnajua jinsi elimu yetu inavyochakachuliwa kila ki-Waziri kinachowekwa pale kinakuja na mtaala wake yaani hadi kichefuchefu. Sasa hivi tena wameleta agenda ya kitabu kimoja hebu jiulize ni vitabu vingapi vanakuwa havitumiki? Hivyo kwa wale wanaoweza kuwa na biashara ya Recycling nawakaribisha au mnipe mawazo ni wapi naweza viuza vitabu hivyo?
   
 3. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ngoja tusubiri wadau wenye uelewa na hili suala la vitabu outdated watufundishe njia mbadala, au kama ni recycling inakuwaje?
   
 4. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2010
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  mimi napenda kusoma na kununua vitabu, naomba uni PM titles ulizo nazo, ila vitabu vya shuleni hapana..if u have management books, novels and biographies, kama ni vya shule only vya Shafii Adams and other Swahili great writers..and NOT shigongo books pls
   
 5. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu kama vp weka titles za vitabu ulivyonavyo jamvini ili yeyote ambaye yuko interested aweze kuwasiliana na wewe,
  Binafsi natafuta kitabu kinachoitwa " Money Masters" kimetungwa na jamaa mmoja anayeitwa John Train. Kama utakuwa nacho tafadhali naomba uni-PM
   
 6. p

  pacificamarine Member

  #6
  Dec 18, 2010
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni idea nzuri sana hasa kwa sisi ambao hatuna uwezo wa kumudu kununua vitabu vipya. Naomba wewe ujitangaze kwenye kumbi za wasomi na kisha kila anayeweka order, uwasiliane nasi. Sisis tutakutafutia kitabu chako kwenye soko la dunia kisha tutakuletea mpaka hapo Dar es salaam.
  Kwa anayetafuta kile kitabu cha "Money Master" sisi tunacho hiki:
  Money Masters of Our Time by John Train (Signed)

  Tuandikie: pacificamarine@yahoo.com ili tufanye biashara
   
 7. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #7
  Dec 20, 2010
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nimekutumia message mkuu!
   
 8. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Fanya utafiti wa soko/wateja - wanafunzi au watu kama Nsiande hapo juu? Nahisi utapata vitabu kwa bei chee ukiagiza toka nje kuliko kununua toka kwa wanafunzi. Mwanafunzi atakaa na kitabu kimoja kwa mwaka mzima au zaidi. Ila watu kama Nsiande atanunua na ndani ya miezi miwili atakirudisha umuuzie kingine at a discount.
   
 9. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hapo umenena, natafuta sana vitabu hivyo
   
 10. p

  pacificamarine Member

  #10
  Jan 7, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Re: Buying and selling of used books

  [​IMG] Originally Posted by pacificamarine [​IMG]
  Hii ni idea nzuri sana hasa kwa sisi ambao hatuna uwezo wa kumudu kununua vitabu vipya. Naomba wewe ujitangaze kwenye kumbi za wasomi na kisha kila anayeweka order, uwasiliane nasi. Sisis tutakutafutia kitabu chako kwenye soko la dunia kisha tutakuletea mpaka hapo Dar es salaam.
  Kwa anayetafuta kile kitabu cha "Money Master" sisi tunacho hiki:
  Money Masters of Our Time by John Train (Signed)

  Tuandikie: pacificamarine@yahoo.com ili tufanye biashara  Nimekutumia message mkuu!

  ++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

  mbona hiyo message sijaipata mkuw wakati vitabu vinaendelea kusubiri wasomaji? Ilete tena bosi!
   
Loading...