Butiku: Tanzania sio mali ya vyama vya siasa, tufuate katiba na sheria

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,377
2,000
BUTIKU: TUKO KWENYE WAKATI MGUMU

MZEE Joseph Butiku, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, amevitaka vyama vya siasa kufuata misingi ya Katiba, ili kuirudisha nchi kwenye mstari ulionyooka.

Akizungumza katika uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Asasi za Kiraia ya mwaka 2019/2020, uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mzee Butiku amesema Taifa limetetereka katika kutumia katiba na sheria.
“Tulitetereka kidogo kwenye kutumia katiba na sheria, na ndio maana tulipojitahidi kurekebishika ilikua ngumu. Sasa kurudi si rahisi,” amesema Mzee Butiku.
Mzee Butiku ameeleza kuwa, vyama vya siasa vinatakiwa vitambue ya kwamba Tanzania si mali yao, bali ni mali ya Watanzania.

“Vyama vitambue kwa mujibu wa katiba, Tanzania sio yao, ni ya Watanzania na wako kwa ajili ya kusimamia shughuli za Watanzania. Viongozi wa ndani ya vyama watambue hivyo hivyo,” amesema Mzee Butiku na kuongeza;

“Na wafanye jitihada za kulielewa hili zaidi. Na itakapohitajika kufanya mabadiliko, ifanye kwa utaratibu. Serikali ya sasa hivi ni ya CCM, tunaisema. Lakini kwa serikali zijazo utaratibu ni huo huo, tutasema kwani ndivyo tulivyokubaliana.”

Mzee Butiku amesema ni vyema serikali, vyama vya siasa, asasi za kiraia na Watanzania kwa ujumla wakatambua kwamba kila mtu ana wajibu wa kuheshimu uhuru, utu na haki za binadamu.

“Tunastahili haki za binadamu kama zinavyotajwa kwenye katiba. Kwa nini tunabishana? Wengine waoga, hamuwezi kusema, wengine ni wanafiki hawawezi kusema,” amesema Mzee Butiku.

Ameeleza kuwa, Taifa lililojaa waoga, wanafiki na wapenda fedha haliwezi kusimamia na kujenga haki.

“Mimi nikiwa rais, mshauri wangu akiwa muoga, atanisaidia? Nimewahi kuwa msaidizi wa rais, ni kazi ngumu. Huwezi kumsaidia kama muoga, mnafiki, mzurulaji, mwizi na mpenda hela, huwezi,” amesema Mzee Butiku.

Mzee Butiku amesema ni jukumu la kila Mtanzania, kuisimamia serikali kwa kuwa bila wananchi hakuna serikali.
Amesema hata Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichukia watu wanafiki, na kwamba alitaka watu wazungumze.

“Baba wa Taifa alituachia utamaduni wa kuzungumza, hakuogopa wazungumzaji. Kikubwa kwake ni mazungumzo, majadiliano. Alichukia tabia ya watu kujitutumua na kuonea watu. Alitaka watu wazungumze,” amesema Mzee Butiku.

Wakati huo huo, Mzee Butiku amekemea tabia ya baadhi ya vijana kufanya siasa chafu kwa kuwatukana watu, na kutoa wito kwa wazee kuwakanya vijana wenye hulka hizo.

“Vijana msiwe makuwadi, acheni kuwa makuadi. Mnatumwa kutukana, muache na nyie wazee mkiwaona muwaite muwaseme. Hatuwezi, wakati tuna vikao, tuna vyama. Watoto wanatok, wanatukana hivi hivi, hii ni tabia gani taifa gani?” amehoji Mzee Butiku na kuongeza;

“Watu wenye tabia hii ni uhuni, haifai haifai haifai.Tumsaidie rais wetu. Wakati mwingine unaweza ukadhani anatumwa, anatumwa na nani
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
13,804
2,000
Mbona kazunguka sana badala ya kusema tu sisi isijimilikishe nchi ?
 

Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
12,363
2,000
Mzee Butiku;
Wewe ni mzee mwenye heshima nchi hii;

1.Kuna Chama cha Siasa kimejimilikisha nchi, yeyote mwenye mawazo au itikadi tofauti na chama hicho anageuzwa adui wa Taifa.

2.Kuna kiongozi anaogopwa kuliko kifo kiasi kwamba hata walioteuliwa kuwa washauri wake ni kama wanapokea mshahara bila kazi maana hakuna wanachoshauri.

3.Chama kilichotakiwa kuongoza serikali kimejigeuza Chama tawala. Yaani badala ya "kuongoza" serikali chenyewe kimejigeuza Chama dola, kinatawala na kuburuza nchi.

4.Kiongozi wa nchi ndiye katiba. Yaani badala ya nchi kufuata katiba inafuata mawazo ya mtu mmoja. Anafanya mengi yaliyo kinyume cha katiba lakini hakuna wa kukemea hali hii. Hata kwenye familia baba akiwa mlevi na mbabe kwa familia anatafutiwa watu wa kumdhibiti, lakini kwa Tanzania hili haliwezekani, limeshindikana, yeye ndo Seriakli, ndiye Bunge ndiye Mahakama.

*Katika hali kama hiyo unategemea kuwepo umoja wa kitaifa?
*Unategemea katiba ifuatwe na watu wa chini huku viongozi wakiisigina kwa nyayo zao?
*Unadhani Nani ana wajibu wa kurekebisha hali hii kama siyo nyie wazee mliowahi kuwa na mamlaka nchi hii na mmestaafu kwa heshima?
 

mwakijembe

JF-Expert Member
Mar 20, 2017
1,451
2,000
Mzee Butiku asizunguke sana, matatizo mengi ya nchi yetu ni madaraka makubwa aliyonayo rais kikatiba. Hata sasa tatizo la kujimilikisha nchi ni matokeo hayo hayo ya rais kuwa na madaraka makubwa kupita kiasi. Katika mazingira ambayo rais hashitakiwi usitarajie akiwa na busara kidogo kama ilivyo sasa, atatii katiba au kusikiliza ushauri ambao hautaki. Katiba hii inayomfanya rais kuwa mungu, ilitungwa enzi za hao hao akina Butiku na msingi wake ilikuwa ni wao kujipendekeza kwa Nyerere.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom