Butiku: Mjadala Katiba mpya uheshimu iliyopo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Butiku: Mjadala Katiba mpya uheshimu iliyopo

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by mzambia, Jan 3, 2011.

 1. m

  mzambia JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  KATIBU Mkuu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), Joseph Butiku, amesema kauli zinazopishana kuhusu masuala yanayohusu mustakabali wa nchi ikiwamo suala la Katiba mpya, zinaashiria kukua kwa demokrasia lakini akaonya kuwa mjadala huo unapaswa kulinda na kuheshimu katiba iliyopo.

  Akizungumza na Mwananchi mwishoni mwa wiki iliyopita. Butiku alisema mjadala ni mzuri na unaonyesha kukua kwa demokrasia, lakini lazima uheshimu katiba ya sasa.


  "Migongano hii ni dalili za kukua na kukomaa kwa demokrasia, kama tukiwa na uvumilivu mwishowe mazungumzo hayo yatatupa matokeo mazuri," alisema Butiku na kuongeza:


  "Katika mjadala huu wa katiba mpya, kila anayetoa maoni yake, aeleze mtazamo wake sio kuwakejeli wengine."

  Butiku ambaye pia ni kada wa CCM, alisema ni bora kila mtu kutopuuza linalosemwa na mwingine, wajadiliane kwa kusikilizana.

  Alisema badala ya mjadala huo kuendelea kufanywa kuwa wa vyama vya siasa na baadhi ya watu, ni vema ukashirikisha wananchi wote ambao ni walengwa wa katiba hiyo.


  Butiku ambaye alikuwa msaidizi wa karibu wa Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere, alisema watu wanaojadili hoja ya katiba mpya wasisahau kuwa, bado Tanzania ina katiba na inahitaji kulindwa na kuheshimiwa.


  Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana, alisema migongano ya mawazo baina ya viongozi hao, ni matokeo ya kukurupuka kuzungumzia mambo bila kufanya utafiti wa awali.

  Dk Bana alisema migongano hiyo ni funzo kwa marais ambao ndio wenye mamlaka ya kuteua viongozi wa nafasi mbalimbali serikalini.


  "Sisemi kuwa AG (Jaji Frederick) Werema hafai, la! ila kutokana na cheo chake lazima awe makini kwa anachokisema, katika mambo mazito ya nchi," alisema Dk Bana.


  Dk Bana ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Siasa na Uongozi cha UDSM, alisema kitendo cha kugongana kwa kauli za viongozi wa serikali, kinaleta tafsiri tofauti kwa wananchi, hivyo ni bora wakawa makini kwa kila kitu watakachokizungumza.


  "Nafikiri kukurupuka kwa viongozi wa serikali kunawababaisha wananchi, kwani kunaibua maswali mengi bila ya majibu," alisema Dk Bana.


  Dk Bana ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mpango wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (Redet), alisema mgongano huo unaweza kutafsiriwa kuwa ni kiashiria cha kupanuka kwa demokrasia.


  "Huyu mwanasheria wetu kwanza amerukia tu hili suala, yeye halimuhusu, hii ni kazi ya wanasiasa, yeye sio mwanasiasa, tulitarajia kutokana na hali ya siasa ilivyo nchini angeshauri serikali kulichukua na kulifanyia kazi," alisema Dk Bana.


  SOSI: MWANANCHI


  WAZO : HUYU NAYE HAELEWEKI
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Ushirikishwaji wa raia wote lazima utokane na sheria siyo hiari ya viongozi......................na ya kuwa mapendekezo ya raia siyo yachakachuliwe na viongozi kupitia Tume ya Raisi ambaye hana mamlaka ya kisheria ya kurekebisha katiba.............................

  Ni vyema Butiku angelikuwa wazi kuwa kuheshimu katiba iliyopo kunamaanisha ya kuwa Bunge tu ndilo liongoze huu mchakato na wala siyo IKulu.................Kwa lugha nyingine JK atakuwa amevunja katiba kuunda Tume ambayo haitambuliwi na Katiba iliyopo .................
   
 3. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo zamani nilikuwa nam-regard mhe Butiku kama mzalendo, lakini tangu ajifungie Butikama kimya bila kukemea vituko vya Kikwete, amenitoka akilini!!!.
  Kule kuzungumza kwa kujificha ndani ya Nyerere Foundation wakati yeye ni kada wa CCM bila kukemea vitendo viovu vya Kikwete na CCM kunaonyesha upungufu mkubwa sana wa sifa ya uongozi!!!!!!!.Hafai kabisa!!!!!!!!!!!!!!!
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Ameshafundishwa unafiki huyu si vinginevyo na watamtumia kweli kutimiza matakwa yao
   
 5. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  anasema hayo baada ya kupewa eneo la AVALON CINEMA

  useless kabisa huyu
   
 6. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  mzee butiku in his last minutes in politics! makamba laishamuita mwehu kama sikosei
   
Loading...