Vigogo Wamshutumu Rais kwa Kukosa Kuchukua Hatua Dhidi ya Rushwa, Ubadhirifu na Ufisadi

Bubu naomba ufafanuzi kidogo ... wananchi wana uwezo wa kusimamisha marupurupu yake? How? Jeuri ya wananchi iko wapi? Kwenye sanduku la kura? Yaani mpaka 2010 ndipo tumuonyeshe jeuri? Je wadanganyika wakinunuliwa na pilau ya RA tena?

Kuna kila dalili kwamba kutakuja kutokea aina fulani ya hawa viongozi waliopita mmoja wao akanyang'anywa mali zote alizopata wakati akiwa rais si mwingine ni huyu huyu Mzee wa Lupaso Mkapa. Amejaa kiburi cha ajabu sana.
 
Kwa nini lisijitokeze kundi la wafurukutwa wampeleke mahakamani? Si nasikia wanasheria wetu walishasema kuna huo uwezekano? Huko atasema tu mwizi mkubwa huyo. Ana kiburi cha ajabu. Yaani kujitu tuhuma zake za uwizi ni kurudi kwenye siasa? Kwa hiyo anataka kutuambia ukiwa kwenye siasa ni ruksa kuiba?
 
Mbona Mkapa anazunguka kila kukicha kukata issues?

Iweje ashindwe kujibu maswali aliyoulizwa? Kwa kushindwa kwake na kutoa majibu ya mkato ni hukumu tosha kuwa kuna mengi anayajua/aliyoyafanya ya kuhujumu taifa na hataki kuyatolea ufafanuzi.

Mafao ya Rais Mstaafu wanaopaswa kuyapata ni viongozi waadilifu tu Waliotumikia nchi yetu bila kufanya biashara.

Kama hawezi kujibu tuhuma za kufanya biashara kuna haja ya kuwabana Muungwana pamoja na Bunge watuondolee sheria ambazo zinaendana kinyume na masilahi ya taifa.

Watanzania tumezidi upole mno wa kuwatukuza MAFISADI na kuwaona ndio watu wa maana.

"Ukitaka kumuua nyani usimwangalie usoni".

Yoyote anayemtetea FISADI naye ni FISADI tena ni hatari sana zaidi ya FISADI mwenyewe.

Tunaomba Bunge libadilishe vifungu vinavyotetea MAFISADI
 
Well, where should i start. Maana nowadays nikisikia jina la Mkapa nywele zangu zote zinansimama kwa hasira. This guy ametuburuza wabongo for ten years, nakumbuka alipokua akihutubia waandishi wa habari alikua anaongea kwa ubabe kichizi na kutishia waandhishi wa habari kiasi hata wanaogopa kumuuliza maswali magumu. Sasa haka katabia kake ka kudharau watu ameendelea nako hata baada ya kutoa urais, nadhani muda umefika kwa huyu jamaa kushughulikiwa. Kama sio kisheria then hata kihuni.

Halafu ningependa kujua, hivi hiyo NGO yake ni nani anampa fedha? Kama anapata fedha toka nje, then inabidi kuwasiliana na hao wafadhili wake na kuwaeleza who this guy really is - kwamba ni kibaka kama vibaka wengine wa mtaani and that they shold stop financing his NGO.
 
Huyu jamaa anakiburi kilichozidi kiasi, anaona watanzania wengine kama sisimizi kwamba anaweza kuwakanyaga anavyotaka. Nakumbuka akiwa Uingeleza aliulizwa swali katika kipindi cha hard talk - akamjibu mwanahabari tim kwa jeuri "Go and ask them" Ben zama hizo zimeshapita, watanzania wa sasa si wale wa zamani, lazima utawajibu tu, kama si leo basi ni kesho. Zama za uwazi naukweli? Sh*******, what did you mean?? Kiwila, ANNBEN or Filisi sawa tu.

Changes are innevitable, and here they are, CCM is Gone.
 
Posted Date::10/19/2007
Malecela: Butiku ana haki ya kuzungumza
Na Jackson Odoyo
Mwananchi

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, John Malecela, amesema Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ana haki ya kuzungumza kama alivyosema katika kauli yake kumtaka Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ajitokeze kujibu tuhuma za ufisadi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Malecela alisema ni vyema mtu anapotuhumiwa kama ilivyokuwa kwa Rais Mstaafu Mkapa, ajitokeze kujibu tuhuma hizo ili wananchi wafahamu ukweli kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Malecela alisema hatua ya Butiku kumtaka rais wa awamu ya tatu kujitokeza ili aweze kujibu tuhuma zilizotolewa dhidi yake ni sahihi, kwasababu ni Mtanzania na yuko ndani ya CCM kwa miaka mingi.

"Butiku ana haki ya kusema kwa sababu ni Mtanzania na mwanachama wa CCM, kwa sababu moja ya kanuni za katiba ya CCM inasema nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko hivyo hata yeye ana haki ya kusema," alisema Malecela.

Alisema Bukitu hakuyasema hayo pembeni bali aliyasema mbele ya waandishi wa habari, hivyo Mkapa mwenyewe ana nafasi ya kukubali ama kukanusha.

Makamu Mwenyekiti huyo wa Tanzania Bara aliongeza kwamba Butiku aliwahi kumuandikia Mkapa barua na nakala ikasambazwa kwa wanachama wote na Mkapa analifahamu hilo.

"Niseme ukweli, ninajua Butiku aliwahi kumuandikia Mkapa barua miaka miwili iliyopita na nakala ikasambazwa kwa wanachama ...," alisema Malecela.

Alisema Butiku anaifahamu CCM kwa undani zaidi kwa sababu aliingia ndani ya chama hicho tangu wakati wa TANU na ASP akitokea masomoni Makerere Uganda na aliwahi kuwa Msaidizi wa Mwalimu Julius Nyerere mpaka Nyerere alipofariki dunia, hivyo ana haki ya kusema chochote anachoona kina faida ndani na nje ya CCM.

Kuhusiana na sakata la ufisadi dhidi ya baadhi ya viongozi wa serikali ya Awamu ya Nne, Malecela alisema kuna vyombo maalum vya sheria vilivyowekwa na viongozi hao waliotajwa kama mafisadi na ikibainika watafikishwa mbele ya sheria na kila atakayekutwa na hatia, CCM haitamtetea hata kidogo, kwa sababu wanaharibu heshima ya Tanzania.

Alisema kama kiongozi, ikabainika kuwa katika idara yako kuna tuhuma nyingi ni vyema kujiuzulu ili kulinda heshima yako kuliko kukaidi.

Malecela alisema hayo ikiwa ni siku ya nne tangu Butiku aliposema Rais Mstaafu Mkapa anapaswa kujitokeza kujibu tuhuma hizo ili zijulikane kama ni kweli au uongo na kurudisha imani yake kwa wananchi.

Naye Paulina David kutoka Mwanza anaripoti kuwa, Katibu Mwenezi wa CCM Taifa, Aggrey Mwanri alisema kuwa binafsi hajawahi kuona barua inayoelezwa na Butiku.

Alisema kuwa kama kuna kitu ambacho kinamkera Butiku basi ipo siku atakiongea kwenye chama kwa kuwa ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi na anafahamu taratibu zinazofanywa na wanachama wa chama hicho kama kuna jambo ambalo linaenda visivyo.

Butiku ni mtu ambaye tunamuheshimu sana katika nchi hii kwa kuwa amefanya kazi kwa karibu na Baba wa Taifa, hivyo tunaamini kama kuna kitu kimemkera atakifikisha kwenye chama," alisema.
 
Kwa nini lisijitokeze kundi la wafurukutwa wampeleke mahakamani? Si nasikia wanasheria wetu walishasema kuna huo uwezekano? Huko atasema tu mwizi mkubwa huyo. Ana kiburi cha ajabu. Yaani kujitu tuhuma zake za uwizi ni kurudi kwenye siasa? Kwa hiyo anataka kutuambia ukiwa kwenye siasa ni ruksa kuiba?
kumhusisha Rais na wizi ushahidi ni mdogo sana,na mara nyingi yeye hausiki moja kwa moja..ndio ujanja wa viongozi wetu,Muungwana anaweza asign mkataba wowote ila akwa anafaidika na huo mkataba
Dawa ni kuwang'oa madarakani alafu tunawashughulikia.
 
katika maraisi tazania ilowahi kupata, Mkapa namvulia kofia. jamaa huyu ni kiburi kupindukia. na kwa kumsubiri ajibu tuhuma mwenyewe hatojibu kamwe.

kama kuna uwezo wa kumlazimisha kujibu tuhuma na zitumike, hata kama ni kuwaendea wafadhili wa hiyo NGO yake kuwaambia ufisadi wake aloufanya
 
Huyu mzee malecela nadhani anatakiwa kukiri kuwa chama kimekosa mwelekeo. Mbona ndugu yake Horace Kolimba alishasema hayo toka 1994?? 1995?? Sasa anaposema kuwa anamuunga mkono butiku, wakati huo huo anasema chama hakijapoteza mwelekeo mbona anajikanganya??? Kwanza huyu mzee ndio alikuwa mtu wa mwisho kupiga msumari kwenye jeneza la zitto dodoma. Ni ujumbe gani anaotoa katika umma wa watanzania???
 
Mwaka huu watamalizana, Kila mwenye dukuduku atalitoa. Huenda ni mwanzo wa kuwa na demokrasia ya kweli nchini.
 
Malecela anasahau kuwa yeye ndiye alie ua Azimio la Arusha na kutuletea Azimio la Zanzibar, ambalo kwalo limefungua milango kwa viongozi (akiwemo yeye na Mkapa) kujilimbikizia mali.

Tunaangalia tulipoangukia badala ya tulipo jikwaa!
 
Ni kweli Mzee Butiku ana hoja,lakini je ni kweli kashindwa kuwatumia wazee wenzake kumshauri Mr Clean baada ya kutojibu barua yake?Maana sasa wazee wanaanza kupambana wenyewe.Mzee Malicela nae anasema Mkapa ajibu hoja,si alikuwa mwenyekiti wake huyu.Hawatupigi changa la macho hawa?
 
Malecela anasahau kuwa yeye ndiye alie ua Azimio la Arusha na kutuletea Azimio la Zanzibar, ambalo kwalo limefungua milango kwa viongozi (akiwemo yeye na Mkapa) kujilimbikizia mali.

Tunaangalia tulipoangukia badala ya tulipo jikwaa!

Sawa sawa kabisa Masatu, ni sawa na mjamzito kumtukana mkunga kumbe yu tayari ana mimba, yeye alivunja Azimio la Arusha kwa unafiki alioshirikiana nao hao matawi ya juu, anahangaika pamoja nasi hapa chini. Jikaze mzee ndio hali yenyewe.
 
Back
Top Bottom