Vigogo Wamshutumu Rais kwa Kukosa Kuchukua Hatua Dhidi ya Rushwa, Ubadhirifu na Ufisadi

Badala ya kumjibu vizuri mwenyekiti huyo, ambaye pia alikuwa mjumbe halali wa kikao hicho, alikemewa na kuzomewa. Miongoni mwa waliomkemea na kumdhalilisha ni wajumbe wa Kamati Kuu, ambao ni viongozi wakuu wa chama.


Wallahi! Kumbe ka-mchezo ka kuzomea viongozi walikaanzisha wenyewe ndani ya CCM? Kumbe ni sawa wananchi huko mikoani kuwazomea maana ndio lugha wanayoijua vizuri!

Wazee Masatu na Killtime, mnasikia hii kutoka kwa Butiku!

Nitarudi baadaye kuikata hiii barua kwa undani!
 
Mambo yanavyokwenda, nina imani Butiku ana kundi kubwa sana nyuma yake ambalo liko ndani ya ccm. hili ni kundi la wapiganaji ndani kwa ndani ambalo limechoshwa na mambo yanavyokwenda kiholela. lipo pia kundi neutral, hili linatazama upepo unaelekea wapi na lipo kundi la mtandao.

kwa haraka haraka hesabu zangu zinaonyesha upinzani unatakiwa kulitumia sana kundi la kwanza kujenga hoja. hoja zikipata nguvu na kuungwa mkono na wananchi wengi, kazi itakuwa rahisi sana ya kuikomboa hii nchi kutoka kwenye mikono ya kundi la mtandao ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo wanaipeleka nchi kusiko.

Barua ya Butiku ilikuwa na hoja na bado ina hoja nzito ambazo Mwenyekiti wa sasa pia kama anayo nia inaweza kumsaidia kukirudisha Chama kwenye mstari ingawa kwa mwendo uliopo tunaota ndoto za mchana kufikiri JK anaweza kurekebisha mambo ndani ya CCm na ndani ya serikali yake. Teuzi zake za hivi karibuni kwenye idara mbalimbali za serikali yake zinatoa ushahidi kwamba hakuna kitakachofanyika kwa sasa.

Tegemeo pekee kuikwamua Nchi kwa amani ni Kura za wananchi, lakini ikishindikana pia zipo njia........ila Watanzania hawataki kufika huko kwani naamini busara zinaweza kutuongoza tukafika salama tuendako.
 
Kinachonifurahisha ni kwamba Taifa, liko kwenye transition state, tukiweza kuweza kuingia kwenye demokrasia ya kweli ambayo naona tunaelekea huko, kama watu wanakuwa na haki ya kutoa maoni na maoni yanaonekana kwa watu kama hivi then soon tutakuwa mahali pazuri tu!

Lakini kama tutaenda kwa pupa, sitashangaa tukiangukia pua!
 
Lowassa, asema mkataba wa Buzwagi, ni safi sana kwa maendeleo ya taifa letu, na kwamba Karamagi hana sababu yoyote ya kujiuzulu!

Na pia leo, kuna habari kuwa Mbunge wa zamani wa upinzani, anatazamiwa kufungwa jela rasmi, leo huko Bukoba!
 
FMES

Lowasa anahusika na mkataba wa Buzwagi, lazima aseme safi!

Mbunge wa Zamani ni Lwakatare, hukumu imeshatoka. Amepatikana na hatia, lakini hajafungwa. Amepewa onyo na anatakiwa kutokufanya kosa ndani ya mwaka mmoja. Kwa kweli naipongeza mahakama kwa hili. Mazingira ya kosa la Lwakatare, Lwakatare mwenyewe tabia yake, udogo wa kiasi cha madhara ya kosa na sensitivity ya kesi yenyewe kwa umma inafanya niamini busara ya kisheria iliyotumika. Maelfu ya Vijana walizunguka mahakama na baada ya hukumu kutangazwa zilikuwa ni nderemo na vifijo barabarani na hata kwenye mabaa.

Mtu wa Meli-naomba tuwasiliane kupitia mnyika@yahoo.com

Natabaruku

JJ
 
Kilitime,

Transition state/stage inachukua miaka mingapi? Ni kweli tunaelekea kwenye demokrasia ya kweli?

Baada ya kusoma barua ya Mzee Butiku kilichowazi ni kwamba barua hii iliandikwa wakati wa vuguvugu la uchaguzi ambapo demokrasia ya kweli ilikuwa inatakiwa zaidi kuliko kipindi kingine. Barua imeweka wazi mapungufu ya uvunjaji wa kanuni za uchaguzi wakati wa mchakato na hata namna watu walivyoenguliwa. Reading between the lines it is clear that Mkapa alikuwa anatuhumiwa kubeba kundi la wenye hela ambao ni wazi kwamba ni wanamtandao.

Since August 2005 mpaka leo hii ni miaka mingapi imepita? Barua imewekwa wazi kwa wananchi ili kuonyesha kwamba siku hizi ndani ya CCM ule utaratibu wa kupokea maoni na kuyafanyia kazi haupo tena. Mkapa kama angekuwa ni muungwana na mwenye nia thabiti ya kusikiliza maoni ninatumaini angemwita Butiku au kama anaona hawezi kuongea nae basi angemjibu au kumwita kwenye vikao vya chama, lakini hayo yote hayakufanyika. Hayakufanyika kwa makusudi maana kama yangefanyika Butiku angeweza ku-spill more beans na kwa kuwa ilikuwa ni kipindi cha kuelekea kwenye uchaguzi basi hilo lingekuwa ni kaburi la CCM hata hizo 80% za JK zisingepatikana.

Mkapa kaondoka kama Rais na Mwenyekiti wa CCM bila kujibu barua, JK kaingia kwenye Urais na baadaye u-Mwenyekiti wa CCM lakini hatujasikia akiongelea haya maoni ambayo Bwana Butiku baada ya kuona hakuna anayeyafanyia kazi ameamua kuyaweka hadharani ili watu tujue yaliyokuwa yanafanyika kwenye vikao vya ndani kabisa vya CCM wakati wa mchakato wa kusaka mgombea wa urais kupitia CCM. Kwa kiasi kikubwa rafu zilizoorodheshwa kwenye barua ya Butiku zinamgusa JK moja kwa moja kwa jinsi kambi ya mtandao ilivyokuwa ikiwashughulikia washindani wa JK. Leo hii unategemea JK atafanya nini kwenye haya maoni ambayo yanamgusa yeye na wapambe wake? Key players wa mtandao ndiyo walio kwenye CC na NEC, unategemea watasikiliza maoni na kuyafanyia kazi wakati yanawagusa wao wenyewe?

Bado sijashawishika kwamba CCM inaelekea kwenye demokrasia ya kweli. Kinachofanyika sasa hivi ni kuanza kuumbuana tu mbele ya wananchi ili hao wanaofanya madudu waweze kujulikana, lakini as long as akina EL, RA na JK ndo vinara wa CCM kwa sasa, hakuna mtu wa kuwanyooshea kidole na hawawezi kuweka demokrasia ya kweli kwa kuwa malengo yao yako beyond 2015 ambapo lazima mrithi wa JK atoke kwenye kundi lao ili aendelee kulinda maslahi yao, maana akiingia mwingine ambaye ana mrengo wa ki-Nyerere basi lazima atawashikisha adabu na nina uhakika hawako tayari kufanya kosa kama hilo maana gharama yake ni kubwa sana!

CCM ina wenyewe na wenyewe ni wanamtandao! Labda tusubiri CCM asilia ijitenge na CCM mtandao ndipo tutaweza kuwa na demokrasia ya kweli. Hilo la kuwa na CCM mbili ninaliona liko wazi na soon linaweza kujitokeza. Subiri 2010 ipite na mchakato mzima wa kuteua wagombea Ubunge upite, baada ya uchaguzi wa CCM wa 2012 lazima kutakuwa na CCM asilia (mrengo wa Nyerere) na CCM mtandao (wafanyabiashara/mafisadi na maharamia)!
 
FMES

Hilo la Buzwagi na la Lwakatare hayahusiani na barua ya Butiku. Nadhani ungeyafungulia Kamba zake.

Ingawa maneno ya Butiku sio mageni, naendelea kuyatakari kwa kuwa sasa yametoka kwa umma, ushahidi wa ndani kuwa CCM imetoka toka kuwa Chama Cha Mapanduzi, ikapita katika njia ya Chukua Chako Mapema na sasa imegeuka kuwa Chama Cha Mafisadi(CCM). Kitila naomba uweke hapa makala yako ya Lucifer effect, tuone jinsi waovu wa ndani ya CCM wanavyoweza kuwabadili wema kuwa waovu. Wema wote ndani ya CCM sasa ndio wakati wao wa kusimama na kuhesabiwa. Wasema sasa au watanyamazishwa milele!

JJ
 
John Mnyika

FMES

Hilo la Buzwagi na la Lwakatare hayahusiani na barua ya Butiku. Nadhani ungeyafungulia Kamba zake.


Mkuu Mnyika,

Heshima yako mkuu, angalia maneno ya Butiku, kuhusu Rushwa, halafu uniambie ni kwa nini Rwakatare anafungwa kama sio rushwa?

Mkataba wa Buzwagi ni nini kama sio rushwa?

Tano: Mimi naamini CCM sasa imeanza safari ya kuelekea kwenye kifo chake, imekumbatia jambo ovu – RUSHWA – ambayo imeua viongozi wazuri wengi, vyama vya siasa na serikali makini duniani.

Heshima mbele mkuu, tuendelee kumkoma nyani mkuu!
 
Wema wote ndani ya CCM sasa ndio wakati wao wa kusimama na kuhesabiwa.

Tatizo la wana CCM na wanasiasa wengi ni ma-opportunists ambao wanaangalia kwanza maslahi ya matumbo yao. Sina hakika kama kwenye kundi la wema wanaweza kusimama na kukubali kuhesabiwa, bali watabaki wanakufa na tai shingoni wakitegemea kwamba labda siku moja JK na wanamtandao wanaweza kuwakumbuka kwa kuwapatia post.

Angalia mtu kama Dr. Mwakyembe ambaye kesi yake na Mwakipesile ilishaonyesha wazi kwamba hatakiwi kwa wana mtandao, lakini the very same person yuko bega kwa bega kutetea madudu yanayofanywa na serikali with expectations kwamba labda iko siku atakuja kuukwaa uwaziri! Kusimama na kukemea uchafu ndani ya CCM unatakiwa uwe na roho ngumu kama ya mwendawazimu ambaye hajali kama anasikilizwa au hasikilizwi lakini msg imekuwa sent and delivered, ni juu yao kuifanyia kazi au kutoifanyia kazi.

Kwa wale walio na interest za kugombea ubunge ndiyo mbaya zaidi maana kila siku utakuwa unakumbushwa kwamba uteuzi wa ugombea Ubunge wako lazima upitishwe na CC na NEC. Na pale inapobidi hata kura za maoni huwa haziheshimiwi, na maamuzi ya CC na NEC huwa hayahojiwi, sasa sijui ndiyo demokrasia au udikteta?
 
Jamani hii barua ni nzuri sana. Nampa hongera sana Mzee Butiku kwa kuamua kuandika barua hii na hatimaye kuiweka wazi ili Watanzania waisome.

Mkapa kama kawaida yake kwa kujiona mungu mtu na kiburi na dharau aliyokuwa nayo, inaelekea hakujibu barua hii halafu alikuwa anaiita awamu yake ya UWAZI NA UKWELI! kumbe ni fisadi, mtetea wala rushwa, na pia aliyeweka mbele maslahi yake badala ya Taifa. Mungu mkubwa, Mwalimu alipoamua kumchapa viboko alipokuwa mwanafunzi pale UDSM wala hakukosea.
 
huyu mkapa sio siri kumbe hana pesa mbili,muhuni wa kutupwa.

nimeisoma barua yote na kuunganisha na nnayoyasikia huyu hafai hata kuitwa kiongozi bora, nnaamini ubaya wa ccm sio chama bali baadhi ya viongozi wake kama huyu muhuni na wenziwe. na kama hatua za haraka hazijachukuliwa hatari iko mbele
 
Mtu wa Pwani,

Hatua zipi zichukuliwe wakati che Nkapa alishayaharibu mambo na akaomba ang'atuke mapema kwenye uongozi wa CCM ili amwaachie JK bomu ambalo amelitengeneza na sasa naona linaweza kulipuka any time. Mpe ushauri JK afanye nini ili kukinusuru chama na kurudisha imani ya baadhi ya wanachama wakongwe kama akina Butiku.

Nina amini kuna akina Butiku wengi tu lakini wameamua kukaa kimya na kuangalia nini kinaendelea. Unadhani akina Salim A. Salim wakisoma barua kama hizi wanajisikiaje? Akina J. S. Malecela na wengineo ambao walikumbana na rungu la mtandao bila kujijua, wanajisikiaje wanapoona mambo kama haya yako machoni mwa wananchi wa kawaida? JK ana kazi ya ziada na asipokuwa makini Chama chake ndiyo kitakuwa kinaelekea kuzimu kwa kusambaratika kwenye mapande zaidi ya 2.

Nani alaumiwe? Mkapa aliyeacha wanamtandao wakakiharibu chama au wanamtandao ambao walifanya hayo kwa sababu ya kutaka kutwaa dola????? Je, watu waliokumbana na rungu la wanamtandao wako tayari kusamehe hiyo dhambi?

Nina uhakika Salim A. Salim jeraha alilo nalo ni kubwa sana. Uanachama wa Hizbu wa miaka ile unaingiaje kwenye credibility ya mtu kwenye kutaka kugombea uongozi? Kuwa mwarabu ni dhambi? Mbona RA ni m-Iran na bado ni kinara wa CCM na Mbunge pia? Tuhuma ya mauaji ni nzito sana na hasa mauaji ya kiongozi wa kitaifa, iweje tuhuma hizo ziibuliwe wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi? Wanamtandao wanaweza kuwa wanafurahia ushindi wa chee lakini majeraha waliyowaachia wahusika wote walioguswa na rungu lao sidhani kama yanatibika kirahisi!!!!!! Barua hii imeibua mengi sana na nina uhakika Butiku anayo mengi zaidi ya haya.

Ombi kwa Mwanakijiji ... tupatie raha weekend hii kwa kumhoji Mzee Butiku LIVE ili tupate mengi zaidi. Nina imani huyu Mzee anayo mengi sana lakini hajaweza kuyaandika yote na kuna mengi yametokea tangu August 2005 mpaka leo hii. Ukifanikiwa kumhoji nina uhakika utapata mengi sana na tunaweza kufunguka macho zaidi ili wana CCM na wananchi kwa ujumla waweze kujua kiini cha uozo uliopo sasa ni nini na nini kifanyike ili kuondoa huo uozo! Ni ombi tu Mzee mwenzangu!
 
Butiku amchokonoa Mkapa

*Amtaka ajitokeze hadharani ajibu tuhuma
*Asema haamini kama zina ukweli wowote
*Asisitiza uadilifu, hekima, vita ya rushwa


Na Gladness Mboma

MKURUGENZI Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Bw. Joseph Butiku, amemshauri Rais mstaafu Benjamin Mkapa kujitokeza hadharani kujibu tuhuma za ulanguzi akiwa Ikulu katika kipindi cha uongozi wake.

Bw. Butiku alitoa kauli hiyo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Idara ya Habari (MAELEZO) Dar es Salaam, kuhusu hali ya sasa ya Taifa.

Alisema baadhi ya vyombo vya habari nchini vimekuwa vikidai, kuwa Bw. Mkapa katika kipindi chote cha miaka kumi aliyokaa Ikulu, alikuwa mlanguzi, jambo ambalo yeye binafsi haliafiki hata kidogo.

"Mimi ninakanusha kwa nguvu zote kama kweli Bw. Mkapa alikuwa mlanguzi wakati wa urais wake, nashangaa vyombo vya habari vimekuwa vikimwelezea hivyo pamoja na mambo mengine.

"Kutokana na tuhuma hizo kama ni kweli, Rais Mkapa alikuwa mlanguzi, aueleze umma kama kweli alikuwa hivyo," alisisitiza Bw. Butiku.

Akizungumzia rushwa, alisema ni sawa na UKIMWI wa maadili na kwamba mtu kupenda mali au kuwa na ulafi wa mali akiwa kiongozi wa siasa, ni sawa na kuugua UKIMWI

"Katika kujadili hoja hii, tukumbuke na kuzingatia ukweli huo, wala tusigombane, kusingiziana au kuchukiana, tupo hatarini tujadili kama ndugu na bila kuogopana lakini tukiheshimiana.

"Nawaombeni mlisaidie Taifa, Watanzania wote tujadili hoja, si watu au vituko vya aina mbalimbali vya watu, Taifa lina matatizo mengi lakini pia lina misingi inayoliongoza, sheria zake kanuni zake na taratibu zake," alisema Bw. Butiku.

Alisema ameamua kujitosa kama bubu, kuchangia hoja ya uongozi bora na uraia mwema wa Taifa, kutokana na hali halisi ya Taifa kwa sasa.

Bw. Butiku alisema zipo kelele nyingi sana, miluzi na maneno ya kejeli, tabia zisizo za kawaida za kuzomeana na hata kufikia hatua ya wananchi kumsimamisha Rais na kumtaka ajieleze barabarani na tuhuma zingine za ufisadi zinazowahusu viongozi.

"Hii si kawaida yetu, matokeo yake yanaweza yasiwe mazuri, tuelewane tunalofanya ni nini, tujipunguzie matatizo na kuepuka kuharibu sifa za viongozi na Taifa letu," alisema Bw. Butiku.

Alisema hamsemi mtu, bali anazungumzia mfumo wa vyombo vya uongozi na misingi yake, yaani chama tawala na misingi yake na uendeshaji wa chama hicho kwa mujibu wa misingi hiyo.

Alisema CCM ni chama cha imani, matendo ya viongozi na wanachama wake yeye akiwa mmojawao sharti yafanane na imani ya chama hicho.

Bw. Butiku alisema kuongoza si wajibu au kazi ya kubuni tu na si jambo la mtu au kundi la watu binafsi wanaotaka kujifurahisha. Ni wajibu na kazi ya kutii na kulinda Katiba, maadili, kanuni na taratibu.

Alisema kuongoza pia ni kazi inayohitaji umakini, unyenyekevu, hekima, upole, ukali wa muda, uimara wa mawazo, kutulia, kusikiliza, kupokea na kupima ushauri.

"Uongozi wa nchi siyo utaratibu wa mtu mmoja binafsi, familia, urafiki, vikundi, au utashi wa kiongozi au raia yeyote uongozi ni kioo mali ya wote, nguzo muhimu ya Taifa na Utaifa,"alisema Bw. Butiku.

"Kama viongozi wangesimamia mambo kwa mujibu wa katika na kanuni za vyama vyao mambo haya yanayojitokeza sasa hivi ikiwemo rushwa yasingekuwapo.

"Sisi tunaosimamiwa hatujisimamii vizuri, Watanzania tumekuwa makinda ya ndege tunapanua midomo tunafurahi na kuomba rushwa kwa viongozi wanaotaka uongozi," alisema Bw. Butiku.

Alisema wananchi wamekuwa wakichagua viongozi kwa rushwa na hata wanaofanya vizuri katika uongozi, wanalazimika kutoa rushwa, ili waweze kuchaguliwa tena kwa kung'ang'anizwa na wananchi.

Alitolea mfano kwa Mbunge wa Musoma Vijijini, Bw.Nimrod Mkono, ambaye katika kipindi chote cha uongozi wake amefanya mambo ya maana katika jimbo lake, lakini pamoja na mambo ya maendeleo aliyoyafanya katika kipindi cha awamu ya pili, uchaguzi mwaka 2005 waliokuwa wakimsaidia walimwomba rushwa ili kumchagua.

"Hii ni hali ya hatari katika nchi, watu wanathamini rushwa kuliko sifa ya mtu, wako tayari kumchagua mtu asiyekuwa na sifa, kwa kuwa tu ametoa rushwa, hatutafika mbali," alionya Bw. Butiku.

Alisema mtu akitaka uongozi kwa kutoa rushwa hafai kuwa kiongozi na kwamba kiongozi anatakiwa kuongozwa na dhamira na kwamba akishindwa kuongoza kwa stahili hiyo, atakuwa akiongoza ovyo.

Bw. Butiku alisema siku hizi fedha ni sifa, mtu akiwa na gunia la fedha ana uhakika wa kuwa mbunge bila kupingwa.

Source: Majira
 
Rais Mstaafu Mkapa azidi kukabwa ajitokeze kujibu tuhuma

Irene Lipende na James Magai


MKURUGENZI wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere na mwanachama mwanzilishi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Joseph Butiku amemtaka Rais Mstaafu Benjamini Mkapa ajitokeze na kujieleza kwa wananchi kuhusiana na tuhuma mbalimbali zinazotolewa dhidi yake likiwepo suala la kufanya biashara Ikulu.

Butiku, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tatizo la rushwa na ufisadi ambalo linaikabili Taifa hivi sasa.

Alisema Mkapa kama Rais Mstaafu alipaswa kujitokeza hadharani kujibu tuhuma hizo ili wananchi wajue kama tuhuma hizo dhidi yake ni za kweli au uongo pamoja na kurudisha imani kwa wananchi. “Kumekuwapo na tuhuma za namna hii dhidi ya Rais Mkapa kuwa alihusika kufanya biashara Ikulu.

Mimi siamini kama ni kweli, lakini Mkapa anatakiwa ajitokeze sasa na kuwaeleza wananchi kama ni kweli alifanya biashara ndani ya Ikulu ili wananchi tujue,” alisema Butiku.

Alisema kabla ya kufikia kutoa kauli hiyo, kwa waandishi wa habari alimuandikia barua Mkapa ambayo aliipeleka yeye mwenyewe hadi Chamwino kwa wahudumu wake, akimtaka afafanue tuhuma hizo kwa wananchi.

“Mwaka 2005 nilimuandikia barua Rais Mkapa na nakumbuka ilikuwa ni usiku niliondoka na kwenda mimi mwenyewe hadi Ikulu ya Chamwino na kuikabidhi barua hiyo kabla ya kumfikia mtu mwingine yeyote,” alisisitiza Butiku, bila ya kueleza kwa undani kama Mkapa alijibu nini baada ya kumwandikia barua hiyo.

Butiku ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za chama na serikali alisema ingawa kwa mujibu wa katiba, Rais anapewa kinga ya kutokushitakiwa mahakamani, bado anapaswa kuwaeleza wananchi kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Kuhusiana na sakata la ufisadi dhidi ya baadhi ya viongozi wa serikali ya Awamu ya Nne, Butiku alisisitiza kuwa viongozi hao, wanapaswa kujiuzulu kwa kuwa wananchi wamepoteza imani dhidi yao.

“Katika nchi yoyote yenye utawala wa kisheria kiongozi yeyote wa juu anapotuhumiwa kuhusika katika kashfa hasa rushwa anapaswa kujiuzulu kwa kuwa wananchi wanakuwa wamepoteza imani kwake,” alisisitiza Butiku.

Alisema tatizo la rushwa nchini, linatokana na viongozi kushindwa kusimamia ipasavyo misingi ya katiba na kwamba wananchi wenyewe ndio wamekuwa chanzo cha kutoa rushwa.

“Nchi sasa inanuka rushwa, Watanzania tumekuwa sawa na makinda ya ndege, tumepanua midomo yetu na wenye mikono ya rushwa wametumbukiza mikono yao vinywani mwetu,” alisema Butiku.

Butiku alisema matatizo ya ufisadi na rushwa yameshamiri baada ya viongozi kutozingatia maadili ya uongozi, yaliojengwa na Baba wa Taifa katika Azimio la Arusha ambalo lilikuwa linasisitiza miiko na maadili ya uongozi bora.

Alisema rushwa ni sawa na Virusi Vya Ukimwi (VVU) wa maadili na kwamba kupenda mali ni sawa na ulafi kwa kiongozi wa siasa ambaye ana VVU.

Hivyo aliwataka Watanzania kujadili kwa uwazi suala la viongozi na maadili ya uongozi kuhusiana na rushwa na ufisadi kama hoja ya msingi bila mzaha ushabiki wala kujitafutia umaarufu kwamba maadili mema ya uongozi ndio uhai na uzima wa taifa letu.

Source: Mwananchi
 
Mbona toka BCS mzee ES alileta(sikumbuki vizuri)/kuongela hili?

Sio mpya hii kwa baadhi yetu!
 
Mimi nafikiri kwa kifupi sana Hawa jamaa tukiwaita Wanamtandao tunawakuza sana. Haya yalikuwa majeraha waliyoyapata mwaka 1995, kilichofanyikia waliteka nchi kama vile majeshi ya uasi yanavyofanya.Hila ya kwao ilikuwa soft switching.

Nidhamu inayoonekana ndani ya CCM ni nidhamu ya woga na kutojua kesho nitakuwa mgeni wa nani/nitakura nini?. Na hili ndilo linawapa kiburi hawa wanamtandao, imefikia wakati hata kama mtu ana uwezo wake lakini amani hana. Hapa ni utawala mwingine wa Kibabe. Watu wanajifisha kwenye kivuli cha Amani na utulivu na Mwalimu nyerere (Njia nyingine ya utapeli).

Lakini vile vile Mkapa hawezi kukimbia ukweli, haya aliyoyaona Butiku hata akienda wapi lazima litamfuata. Historia itammaliza tu.

Nafikiri mtu mwingine ambaye ana majeraha sana ni aliyekuwa katibu wa CCM zamani, mzee Mangula nafikiri naye anaweza kutoa kilimtokea ktk hili.
 
Nafikiri mtu mwingine ambaye ana majeraha sana ni aliyekuwa katibu wa CCM zamani, mzee Mangula nafikiri naye anaweza kutoa kilimtokea ktk hili.

Lakini Mangula alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa na aliona yote hayo yakifanyika mbele ya uso wake na aliishia kukaa kimya bila kukemea wala kumwambia Mwenyekiti wake kwamba Chama kinaendaa mrama. Hata kama ni majeruhi wa wanamtandao bado alikuwa na nafasi nzuri sana ya kukemea uozo kwa kuwa alikuwa kwenye CC na NEC na pia ndiye alikuwa mtendaji mkuu wa CCM.

Mojawapo ya sababu za Mwalimu (RIP) kuwakataa Kolimba (RIP) na Malecela ilikuwa ni pamoja na kuwaambia kwamba walishindwa kumshauri Mwenyekiti wa CCM na Rais wa wakati ule. Kwa hiyo nina uhakika kwamba Mangula kwa capacity yake kama Katibu Mkuu alipaswa kumshauri Bwana Kibri Che Nkapa kwamba yakhe huko unakokipeleka chama siko, angalia nyendo zako. Lakini Mangula sikuwahi kumsikia akiongelea ubaya wa rushwa na alikuwa mstari wa mbele kutetea takrima ambayo ndiyo imewaweka wana mtandao kwenye uso wa wapiga kura na hivyo kujichukulia uongozi kwenye chama na serikali kwa njia rahisi zaidi.

Ninamuonea huruma Mangula kwamba amepigika na wanamtandao, lakini alikuwa jikoni na alikuwa na uwezo wa kurekebisha mambo kabla jahazi halijaenda mrama. Huo ndiyo ujira wa kukaa kimya kwake. Kama alikaa kimya kwa unafiki akitegemea JK angemkumbuka basi ameula wa chuya na hivyo aendelee kulima viazi huko Njombe!
 
Back
Top Bottom