Vigogo Wamshutumu Rais kwa Kukosa Kuchukua Hatua Dhidi ya Rushwa, Ubadhirifu na Ufisadi

Sasa subiri majibu watakayoyatoa CCM.

Kitila Mkumbo tupe ya bongo mapya? Vipi umeme haukatiki tena huko?
 
Huu ni mfano wa kuigwa.
Nilitarajia watu kama akina warioba,Kawawa na wakongwe wengineo kukemea rushwa kwa uwazi kama alivyofanya Butiku.

Kwangu mimi sikubaliani na raisi kutumia majukwaa ya kidini na mbaya zaidi jukwaa la kuhitimish mbio za mwenge kwa kutetea hao mafisadi wake kwa kisingizio cha kupata ushahidi na kuthibitishwa na mahakama eti ndipo hatua zichukuliwe!!
Ni aibu kwa rais kusemea tuhuma kwa upande mmoja badala ya kuwataka watuhumiwa wote kujiuzuru kitendo ambacho kingelikuwa ni cha kiungwana.
Imani kwa wananchi imeshatoka na hakuna cha kuirudisha isipokuwa kujiuzuru kwa watuhumiwa wote.

Kati ya wote wanaotuhumiwa hakuna hata mmoja aliyetoa majibu ya uhakika ya kutohusishwa na rushwa.
Sumaye aliwahi kutishia kwenda mahakamani,hadi leo hajakwenda na amehakikisha anaukwaa uNEC.

Mkapa ndiye kabisa hajibu hoja hata moja juu ya kusakamwa na tuhuma nzito alizozifanya wakati akiwa madarakani.

Si rahisi kwa hicho chombo cha kuzuia rushwa kuwakamata maboss wao ambao ndiyo waliowaweka baadhi yao madarakani kama vile Hosea.

Laana inatutafuna sasa ni ile ya kutofuata maagizo ya Baba wa taifa.Alituasa kwa mifano aina ya RAIS anayetufaa.Baba huyu ndiye aliyewaengua hawa BOYS2MEN kugombea urais.
Badala ya kutatua kero za wananchi,Rais anatalii tu ulaya na kwingineko.Mawaziri wake wanatalii mikoani huku wakiambulia kuzomewa.Inatia aibu,na haijawahi kutokea mawaziri kutembea nchi nzima eti kuelimisha wananchi juu ya bajeti!!!ni nani asiyejua kuwa maisha yamepanda?Unaelisha nini wakati hukumshirikisha kupanga bajeti yenyewe?

Wabunge wamekuwa ni bendera fuata upepo,na zaidi wale wa chama tawala wamefika mahala wamekuwa ni mawakili wa chama chao kwa maana kupinga hata hoja nzuri kutoka upinzani ili mradi tu zao zipite.

Ili kuinusuru nchi hii ni bora baraza la mawaziri livunjwe na zije sura mpya.

Hatutaki mtandao kuchukua mamlaka ya nchi hii.
Mawaziri wamekuwa ni matajiri wakubwa na wanashares katika makampuni makubwa makubwa,na wengine wanamilki migodi ya madini.

Mwisho nitalia na kufariki bure naona niishie hapo.
 
Taifa linapitia kipindi muhimu sana, kama wananchi wote wa upande wa upinzani, upande wa chama tawala na wale wa mrengo wa kati (wazalendo halisi), watakubali kujadili mambo kwa uwazi bila kutupiana mawe na kadhalika naona taifa litafikia mahali pazuri sana, wananchi wajadili mambo kwa uwazi,,, baba akikosea wakati mwingine sio lazima aseme amekosea anaweza kujisahihisha tu... na mambo yakaendelea vizuri.

Tuendelee kujadili hoja, report za TANESCO kujulikana ni ukombozi mkubwa sana, mikataba kuonekana ni ukombozi mkubwa sana, wasomi kuiteta serikali waziwazi na kwa hoja zinazoeleweka ni mambo mazuri sana...

Na kwa maana nyingine wasomi wanatakiwa wao wenyewe waongezi mchango wao wa kuikosoa serikali at least kwa 20% na 50% vyama vya upinzani, 10% wanaharakati, 20% vyombo vya habari,,, mizania hii italeta mabadiliko makubwa sana kwenye nchi yetu...


Mashaka yangu makumbwa ni speed without control!!!
 
butikuep7.jpg



I DARE YOU: Joseph Butiku challenged the ex-president Mkapa to defend himself against mounting allegations of abuse of office, pointing out that the late Father of the Nation was a firm believer in the principle that State House and presidents should always remain ``beyond suspicion`` as far as leadership ethics and integrity were concerned.

Credit: THISDAY IPP MEDIA
 
Angalau kina Butiku wanaamka kutoka usingizini...
hata hivyo ninafuatialia tamko lake cautiously...
akifanikiwa kushinda kashfa ambazo kama Waryoba na kukwepa raha ya nafasi serikalini atakayopewa atulie atakuwa amefanya kazi kubwa
 
Mkapa atajitetea nini wakati kakutwa akiiba? Atasema alikuwa na njaa?

Mkapa kinachotakiwa ni sheria kuchukua mkondo wake. Apelekwe mahakamani na labda huko ndiko akajitetee.

Kibaya bado anazidi huku nje anazidi kupewa nafasi na kupewa mamilioni ya pesa za kuwasaidia maskini na zilizo nyingi hazifikishi kwa wahusika.

Inabidi wenye CCM wachukue CCM yao maana hawa waliokabidhiwa
ni ujinga mtupu.

Namshangaa Kawawa kakaa kimya.
 
Akirejea kuhusu kile kilichotokea wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM ambao Rais Jakaya Kikwete aliibuka mshindi, Butiku alimlaumu Mkapa kwa kubadili kanuni za uchaguzi katikati ya vikao na bila ya ushauri wa kiongozi mwingine yeyote.

Ndio hapa ambapo haya madudu tunayoyaona sasa katika sisiemu yalipokuwa katika kilele. Iweje Mkapa alipindisha kwa makusudi kanuni za chama chao?
 
Kwa mara nyingine nakupa tano Sam au Mzee FM kwani hii barua uliieleza sana kule kijiweni enzi zile.
Mafuchila
Watu wengi humu hawajui historia ukisema Sam unakuwa unawachanganya au nilirudishe jina kwa mwenyewe na mimi neendelee na langu.
Kwa watu tuliokuwepo kule bcstimes hii siyo breaking news, nakumbuka ulitokea ugomvi mkubwa sana ni lini hii barua itatolewa hatimaye kesho itakuwepo kwenye magazeti.
 
Alisema kutokana na kuuona mwelekeo huo wa CCM kupoteza dira, Agosti 10, mwaka 2005 aliandika barua kwenda kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa Tanzania, Benjamin Mkapa kumueleza kuhusu hali hiyo ya kusikitisha.

Ngoja nicheki cheki, hali ya hewa huenda sasa ukawa wakati muafaka kuitoa hako ka-barua! Aaah kumbe inatoka kesho, basi saafi!
 
Alisema kutokana na kuuona mwelekeo huo wa CCM kupoteza dira, Agosti 10, mwaka 2005 aliandika barua kwenda kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM na Rais wa Tanzania, Benjamin Mkapa kumueleza kuhusu hali hiyo ya kusikitisha.

Ngoja nicheki cheki, hali ya hewa huenda sasa ukawa wakati muafaka kuitoa hako ka-barua! Aaah kumbe inatoka kesho, basi saafi!

FMES,

Nakumbuka uliandika kuhusu hili kule Business Times japo hukuweza kutumegea yaliyokuwemo kwenye hiyo barua.

Lakini nakumbuka uliongelea suala la Butiku kutokufurashishwa na mambo ya Mkapa. Naona kayarudia tena wiki hii.
 
Ngoja nicheki cheki, hali ya hewa huenda sasa ukawa wakati muafaka kuitoa hako ka-barua! Aaah kumbe inatoka kesho, basi saafi!

Komandoo ES, heshima mbele Mkuu ... sina hakika kama hiyo barua itawekwa kwenye website (mara nyingi huwa wanaweka makala na news kubwa tu). Ombi kwako Mkuu, unaonaje ukitufanyia hisani ya kutuwekea hako ka-barua kutoka kwa Mzee Butiku kwenda kwa BWM! Hilo lifanyike iwapo tu Tanzania Daima watakuwa wameshindwa kuiweka kwenye mtandao kama walivyoahidi kwamba itachapishwa kwenye gazeti la Jumatano!
 
Mkapa kinachotakiwa ni sheria kuchukua mkondo wake. Apelekwe mahakamani na labda huko ndiko akajitetee.

Mzee wazo lako ni zuri sana ... lakini ni chombo gani cha dola ambacho kiko tayari kumpeleka BWM mahakamani?

Mahakama zenyewe ndiyo hizi za Jaji Ramadhani ambazo mtu akipeleka kesi under private prosecution anatakiwa atoe evidence kwamba vyombo vya dola viligoma kushughulikia kesi hiyo na hivyo wanatumia vibaya fursa ya private prosecution (nina refer hukumu ya kesi ya Chitalilo).

Je, Mahakama zetu ni kweli ziko huru katika kushughulikia kesi nzito kama ya BWM? Kwanini Jaji Mkuu mstaafu Bwana Samatta aliropoka kwamba uhuru wa mahakama una walakini baada ya yeye kustaafu? Kwanini hakusema hayo wakati akiwa bado yuko ofisini?

The msg was clear kwamba katika mfumo wa kimahakama katika nchi nyingine ujaji mkuu unaenda kwa kufuata seniority na kwamba Rais hawezi kupingana na hilo na hivyo Rais anafanya kazi ya kuteua tu na hivyo jaji mkuu akiteuliwa na Rais haingiliwi katika utendaji kazi wake. Kwa case ya Tanzania hilo halipo (nina refer mahojiano ya Samatta na Gazeti la Tanzania Daima) hii ina maanisha kwamba kuna politics katika kuteua majaji na Jaji Mkuu.

Kwa mantiki hiyo Jaji Mkuu yeyote akiteuliwa lazima aende sambamba na matakwa ya serikali na hata ikibidi kupindisha sheria basi itapindishwa kwa kuwa hakuna chombo kingine kilicho na uwezo wa kutafsiri sheria za nchi zaidi ya mahakama na mahakama ya juu kabisa ndani ya nchi ndiyo yenye mamlaka ya mwisho ya kutoa tafsiri na hukumu ya kisheria. Whether sheria ilipindishwa kwa maslahi ya wachache au serikali hakuna tena anaeweza ku-question hukumu ya mahakama hiyo yenye maamuzi ya mwisho. Ndiyo maana kwenye case sensitive sana ambazo serikali ina maslahi, uteuzi wa majaji wa kusikiliza kesi hizo huwa unafanywa kwa makini sana na ikiwezekana kuweka majaji ambao ni pro-serikali ili wasije wakatoa maamuzi ya kuimaliza serikali! Je, kwa mtindo huu unategemea haki itendeke kwa Mkapa kushitakiwa kwenye mahakama ipi?

Kwenye hii issue ya Mkapa ninaona kuna ka-vicious circle fulani ambako kana ugumu fulani katika kukavunja. Swala la kwanza ni kwamba kwanini Mkapa alionyesha side yake wazi wakati wa mchakato wa kusaka mgombea urais mwaka 2005? Hotuba ya Mkapa ya Chimwaga kwenye Mkutano Mkuu kama mtu ukiisikiliza kwa makini ilikuwa na clear msg kwa wapiga kura ... Leo hii unategemea JK awaruhusu PCCB au Polisi wamchunguze Mkapa? Hata kama PCCB watamchunguza na kupeleka recommendations kwa DPP, bado DPP ana mamlaka makubwa sana ya kusema jalada halina kesi ya kujibu! Bado hata ukienda mahakamani under private prosecution unaweza kukumbana na kiini macho cha matumizi mabaya ya private prosecution. Hiyo vicious circle kuivunja ni kazi ngumu, kuna complications nyingi zaidi kwa kuwa kuna dalili zote za kulindana na JK alishasema wazi kwamba hana nia ya kuanza kuwachunguza marais wastaafu, kwanini atoe kauli kama hiyo kama utawala wake ni utawala wa sheria???????

Lakini yote haya yana mwisho na iko siku tutaona mwanga mwisho wa tanuru japo hajui urefu wa tanuru lenyewe!
 
Wazee tulizeni boli, wa-Zaire wanasema "...tombola malembe mokili ya bato...", tembea pole pole dunia ya watu hii,nimewasikieni ka-barua ninako toka enzi zile niliposema BCS, ila nchi ya watu hii, niliposema kule BCs kuwa ninako nilipewa matusi mengi sana lakini huu ukweli umekuja aliyeiandika mwenyewe anasema,

Mnajua kuwa ningeshaiweka longtime ago, lakini nani naniiii kidogo, sasa midhali mwenyewe mwenye ka-barua ametoa idhini ngoja tuone upepo kwanza wakuu, subira yavuta heri hii na wala sio shari, ahsante mkuu Keila na wengine wote, lakini ninawaahidi subira inafikia ukingoni sasa,

Maneno yanakuja!
 
Nasubiri kusikia Salim anaunga mkono mawazo hayo na kama Butiku alizungumza kama Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu.
Nafikiri Salim ananilielewa hili kwani nakumbuka ulimuuliza swali kuhusu Kama Yupo mtu ambaye anaweza kukemea yale ambayo yanatokea sasa hivi ndani ya nchi yetu baada ya Baba wa Taifa Kuondoka na alijibu kwamba Hakuna anaemfikia baba wa TAIFA KWANI ALIKUWA NI MTU WA AINA YA PEKEE Kwa Tanzania Kama walivyo watu waina yake Nchi nyingine ,kwa Afrika ya kusini Mandela nk, Lakini anaamini wapo ambao bado wanaweza pamoja na kwamba sikatika uwezo wa Mwalimu,Nafikiri Butiku Ni mmoja kati ya aliyekuwa akiwazungumzia Salim Hasa ukizingatia wanafanya pamoja ktk hiyo Taasisi.
 
Nimeisoma kwa kweli ilikuwa yenye kuitakia mema Tanzania.

Lakini Mkapa akaendelea kukaidi!

Ninadhani sasa wana JAMBO NA WATANZAIA WENYE KUITAKIMA MEMA NCHI YETU TUAMKE WEZI WAMEIVAMIA CCM.

WAKATI WA CCM KUGAWANYIKA NI HUU. IILI WEZI WABAKI NA CHAMA NA WANAOTAKIA MEMA NCHI HII WABAKI NA CHAMA CHENYE NIA NZURI.

TIME HAS COME! WAKE UP! WAKE UP!
 
Mnajua kuwa ningeshaiweka longtime ago, lakini nani naniiii kidogo, sasa midhali mwenyewe mwenye ka-barua ametoa idhini ngoja tuone upepo kwanza wakuu, subira yavuta heri hii na wala sio shari, ahsante mkuu Keila na wengine wote, lakini ninawaahidi subira inafikia ukingoni sasa,

Maneno yanakuja!

Nilikuwa sijasoma hapa. Ok Let's wait a bit longer.
 
Nimeisoma kwa kweli ilikuwa yenye kuitakia mema Tanzania.

Lakini Mkapa akaendelea kukaidi!

Ninadhani sasa wana JAMBO NA WATANZAIA WENYE KUITAKIMA MEMA NCHI YETU TUAMKE WEZI WAMEIVAMIA CCM.

WAKATI WA CCM KUGAWANYIKA NI HUU. IILI WEZI WABAKI NA CHAMA NA WANAOTAKIA MEMA NCHI HII WABAKI NA CHAMA CHENYE NIA NZURI.

TIME HAS COME! WAKE UP! WAKE UP!
Kama unaweza kutuwekea hapa tutashukuru na wengine waliokwishaisoma wafanye jitihada watuweke na hapa.Natanguliza shukran!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom