Butiku aibuka tena:Anasema Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
MWENYEKITI wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema kwa sasa Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji.
Alisema kutokana na hali hiyo, kosa linapotokea katika idara wanazoziongoza hushindwa kuwajibika kwa kujiuzulu.
Akizungumza katika kipindi cha 'Je, Tutafika', kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Channel 10, alisema kuna viongozi walipaswa kuwajibika baada ya kashfa za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Alisema kama kiongozi anaweza kudanganywa na akatoa uamuzi wenye kuligharimu taifa fedha nyingi, hastahili kuendelea kuishikilia nafasi hiyo.
"Wananchi watawezaje kulala kama kiongozi wanayemtegemea anaweza kudanganywa na akapitisha uamuzi wenye athari kwa taifa?" alihoji Butiku.
Alisema hayati Mwalimu Julius Nyerere aliweka misingi imara ya uwajibikaji kwa viongozi wake, lakini misingi hiyo hivi sasa inaelekea kutofuatwa.
Alisema kuna kipindi wanajeshi mkoani Mwanza waliwapiga raia na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wakati ule, Ali Hassan Mwinyi, aliamua kujiuzulu, jambo lililomjengea heshima zaidi.
"Alichokifanya Mwinyi wakati ule ndiyo uwajibikaji ambao hivi sasa haupo….. kila kiongozi anajiangalia mwenyewe, huu ni udhaifu mkubwa," alisema Butiku.
Naye msomi maarufu nchini, Profesa Mwesiga Baregu, akizungumza katika kipindi hicho, alisema tatizo la kutokuwa na viongozi imara ndilo ambalo limesababisha kuvunjika kwa dhana ya kujitegemea.
Alisema kuvunjika kwa dhana hiyo kunawafanya Watanzania waendelee kutegemea misaada ya wahisani wakati wana rasilimali za kutosha.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alisema makosa ambayo Tanzania inayajutia hivi sasa ni zoezi la ubinafsishaji.
Alisema dhana hiyo imewarudisha Watanzania katika enzi za umanamba na kuwa vibarua wa wageni ambao hivi sasa wanamiliki uchumi wa nchi.
"Wageni kamwe hawawezi kunusuru uchumi wa nchi, wao huangalia zaidi wanachopata, hapo ndipo Tanzania imekosea, kuruhusu uwekezaji," alisema Mvungi.
Alisema hayati Mwalimu Nyerere alijenga dhana ya kujitegemea, ili kila Mtanzania aweze kupata neema ya rasilimali zilizopo kwenye nchi yake.

Source: Tanzania Daima
 
Huyu mzee anakitu ambacho anataka kuongea kuhusu CCM lakini mbona anendelea kukimezea tumboni. Butiku,Pilipili ni tamu,ndiyo ukweli wenyewe. Hapa ya Baba wa Taifa yalishapitwa na wakati. Kungekuwa na viongozi waadilifu,wafuatao wengejiuzulu, Mramba,Meghji, Karamaghi, Balali na Mr.Clean angetuomba radhi kwa ufisadi wake
 
Nadhani Butiku ni mnafiki ama anatumika kupooza hii ngoma . Yeye mwenyewe hajasema matumizi mabaya ya mfuko wa Mwalimu Nyerere .Au hadi tuanze kusema abishe then ukweli uje ?
 
Nadhani Butiku ni mnafiki .... Yeye mwenyewe hajasema matumizi mabaya ya mfuko wa Mwalimu Nyerere .Au hadi tuanze kusema abishe then ukweli uje ?

Lunyungu

Mtu mzima hatishiwi Nyau kama unajua ubadhirifu aliofanya Butiku weka hadharazani. Maana na yeye atakuwa fisadi vinginevyo unapotosha mada na kwa kudivert attention kwingineko
 
Nadhani Butiku ni mnafiki ama anatumika kupooza hii ngoma . Yeye mwenyewe hajasema matumizi mabaya ya mfuko wa Mwalimu Nyerere .Au hadi tuanze kusema abishe then ukweli uje ?

I agree with you on this. System inajua ya Butiku ndiyo maana haina wasiwasi nae hususan Mfuko wa Mwalimu, nadhani huenda sasa anataka asikike kuwa yupo labda walau ateuliwe mahali fulani. Lakini nina shaka kubwa na uendeshaji na matumizi ya taasisi ile, kwani yuko jamaa mmoja ambaye ni jamaa ya karibu na akina Butiku 'aliliza' sana pale MNF sasa sijui yeye inakuwaje.
 
Pundamilia vipi? mwaga vitu vya huyu fisadi mwingine kama aliliza hapo mahali.. make hapa ni kumkoma nyani, tena kweupe!!!
 
Ufisadi si lazima uwe uko BoT . Kama ukiwa mzinzi hadi unajengea mke wa mwanaume mwenzio jumba kubwa , na kusomesha watoto wote Ulaya kwa pesa ya wavuja jasho huu ni ufisadi pia . Now figure out . Nenda pale BoT muulize yule binti wa Kate Kamba kasoma wapi na pesa nani alilipa .
 
Nadhani Butiku ni mnafiki ama anatumika kupooza hii ngoma . Yeye mwenyewe hajasema matumizi mabaya ya mfuko wa Mwalimu Nyerere .Au hadi tuanze kusema abishe then ukweli uje ?
BUTIKU SHOULD SHUTUP,YEYE AMEKUWA AKIFANYA MNF KUWA NI MALI YAKE,HAIJULIKANI NI LINI ALICHAGULIWA WALA LINI ANAACHIA,KAZEEKA NA HANA MAWAZO MAPYA LAKINI BADO TU AMEKAA,KAZI YAKE KUWASOMESHA WATOTO WA VIMADA WAKE ULAYA.NAKUMBUKA SIKU ZILE AKIWA KATIBU MYEKA WA RAIS ALIKUWA NI MUNGU MTU HUYU NA NDIO MTU WA KWANZA KUJIBINAFSISHIA NYUMBA OYSTERBAY MIAKA YA THEMANINI,NA NYINGINE AKAMPA BINAMU YAKE NIMROD MKONO.GHOROFA LA BUTIKU ALILOJIPA LIKO TOURE DRIVE NAMBA 165 PEMBENI TU YA NYUMBA YA PM.WAKATI ALIPOKUWA RC MARA NYUMBA HIO ALIKUWA ANATUMIA MTOTO WA DADA YAKE MKONO AKIITWA MANG"OMBE KUFIGIA NGURUWE NA KUKU.BUTIKU NDIO ALIEMPA MICHONGO MINGI SANA MKONO KUFAIDI KUANDIKA MIKATABA YA SERIKALI.
 
Alisema kuna kipindi wanajeshi mkoani Mwanza waliwapiga raia na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wakati ule, Ali Hassan Mwinyi, aliamua kujiuzulu, jambo lililomjengea heshima zaidi.
"Alichokifanya Mwinyi wakati ule ndiyo uwajibikaji ambao hivi sasa haupo….. kila kiongozi anajiangalia mwenyewe, huu ni udhaifu mkubwa," alisema Butiku.

Butiku sio tu mnafiki bali pia amepoteza uwezo wa ki akili na kumbukumbu.

Hicho kisa cha wanajeshi kupiga raia Mwanza na Ali Hassan Mwinyi kuwa Waziri wa Ulinzi si kweli na hakijawahi kutokea Tanzania unless mwandishi amemnukuu vibaya.

Ukweli ni Mwinyi alikuwa waziri wa mambo ya ndani wakati askari magereza ( sio wanajeshi) Shinyanga ( sio mwanza) walipo wapiga mahabusu na kuwaua ndipo Mzee Mwinyi aka jiuzuru.

Butiku yeye aendelee kutumbua pesa za mfuko wa Mwalimu asitu yeyushe hapa..
 
Mimi nilionya hapa kwamba Butiku si safi watu wakasema naleta majungu. Kamaliza kabisa MNF haina kitu kabisa sasa wanacheza bahati nasibu nadhani this man is looking for an exit door.Si msafi hata kidogo . Si yeye wala Warioba . Kama ni system CCM kumtumia kuwaponda lakini wanajuana then naweza kuelewa lakini kwa usafi nasema Butiku ni fisadi sana .Mke wa mtu unamjengea ghorofa wapi na wapi .Au ndiyo mwendo wetu vigogo wa CCM vimada nk ?
 
Lunyungu, Masatu, na Fisadi Mtoto.

Mimi nimesomesha watu 3 mlimani, nimmesomesha 2 ulaya (mabinti 2) si ndugu zangu na kuwasaidia maana walikua na bidii ya kusoma na ndio njia muafaka niliona naweza kuwasaidia.

Je unaweza kuniita mimi fisadi? Pili ile ni Foundation na inaweza kupewa offer na vyuo kupeleka watu kusoma nje, Je ni evidence gani unaweza kutupatia kuonyesha kweli amefuja mfuko ili tumshushie makombora.

maana Kwangu haitoshi kusema alisomesha vimada kwa kufuja hela za MNF? Audit reports zao zimeonyesha upotevu wa hela?

Je waliopelekwa kusoma walipata hizo nafasi kwa kutoa rushwa ya ngono?
Ieleweke binti kupewa nafasi yakwenda kusoma na kurudi kuwa hawara haijustfy ufisadi
 
Mahatma Gandh aliongelea juu ya dhambi 7 ambazo Jamii yeyote inapaswa kuto zifanya la sivyo jamii itaharibiwa kabisa.
Fuata hiyo lead usome mwenyewe kisha ulinganishe na Tabia chafu yenye uoza na Ufilauni na mambo mengine nuksi wayafanyayo Mafisadi wa cham cha SISIEMU na serikali yao.

Kwa wale wanajua Kimombo;

"Mahatma Gandhi said that seven things will destroy us. Notice that all of them have to do with social and political conditions. Note also that the antidote of each of these "deadly sins" is an explicit external standard or something that is based on natural principles and laws, not on social values."

http://www.mkgandhi.org/mgmnt.htm\

Wealth Without Work

Pleasure Without Conscience

Knowledge Without Character

Commerce (Business) Without Morality (Ethics)

Science Without Humanity

Religion Without Sacrifice

Politics Without Principle
 
Fisadi Mtoto,
Kwanza Mukono si binamu yake Butiku. Na hii kuwa Mukono alipewa nyumba na Butiku si kweli. Mukono ana fedha nyingi sana na ile nyumba anayokaa kule Masaki alijenga katika miaka ya 70. Mukono anazo ndege 2 kweli mtu kama huyo anahitaji kupewa nyumba? Sema jingine lakini hili la nyumba sikubali kabisa.
 
Masatu,
Sahihisho dogo tu ktk kisa cha Mwinyi.... waliouawa ni vizee waliokuwa wakikisiwa kuwa ni wachawi, ka hiyo mwandishi huyu anaonyesha wazi kapachika maneno kinywani mwa Butiku. Sofar he is the only leader from CCM ambae kasimama na kuulaani ufisadi.
Kuhusu Butiku naomba mtuweee hapa matumizi mabaya ya fedha za foundation ya Nyerere maanake sisi wengine tuna jamaa zetu humo na wahana kitu kabisa hadi leo hii, tena wanalia kuona nchi inaburuzwa na kizazi kipya cha Mafisadi.
 
MNF Nyerere alikuwa mtu safi- na hapa ndo kioo kilichobaki kwa uadilifu wa Mwalimu!

Kama kuna ufujaji wa pesa -basi tujulishwe!

Sasa je ni yupi msafi? Je mimi na wewe ni wasafi? Kwa 100%?

Hata Clinton alichemsha kwa Monika!

Je aaminiwe nani?
 
Butiku, anafahamu anachokifanya. Sidhani kama anaweza kurusha mawe kwa jirani iwapo yeye mwenyewe anaishi kwenye nyumba ya vioo. Bado naamini kuwa Butiku ni msafi, iwapo tunaongelea juu ya uaminifu na uadilifu wake kwa taifa. Binafsi naogopa sana kuhusisha tabia za mtu binafsi na madhaifu yake na uwajibikaji wake kikazi. Ukweli wenyewe, hata kama Butiku anajengea vimada, bado haiwezi kujibu au kufananishwa na madhambi ya mafisadi ambayo yanagusa uhai wa taifa kama BOT.
 
Mimi nilionya hapa kwamba Butiku si safi watu wakasema naleta majungu. Kamaliza kabisa MNF haina kitu kabisa sasa wanacheza bahati nasibu nadhani this man is looking for an exit door.Si msafi hata kidogo . Si yeye wala Warioba . Kama ni system CCM kumtumia kuwaponda lakini wanajuana then naweza kuelewa lakini kwa usafi nasema Butiku ni fisadi sana .Mke wa mtu unamjengea ghorofa wapi na wapi .Au ndiyo mwendo wetu vigogo wa CCM vimada nk ?

Linyungu

Simjui Kiongozi msafi zaidi ya mwenyezi mungu. Navyoelewa, sie ndio image yake. Unaweza-ukajikanganya hapa, fanya peruzi ya usafi kwako, ukipata amani, unaweza kumsema mtu yeyote asie safi.

Huyo ni Warioba yupi?
Kwenye jungu...
Mke wa mtu unamjengea ghorofa wapi na wapi
...hili jungu!

Nikirejea na subject matter: 'Butiku';'Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji'

Mimi nafikiri Butiku alikuwa anajua hili jambo Mheshimiwa ataliongelea- kama sikosei kwenye spichi ya Mheshimiwa amedai wameafikiana kuhusu maadili ya viongozi kwenye kikao chao cha CCM-huyu mzee hajakurupuka! Nafikiri alitaka kutoa duku-duku la nini hicho walichoaafikiana. My take on this, ni demokrasia inaanza kunyemelea CCM.
Tuendelee
 
Sasa mimi nasema tuangalie issue at hand now .Mbona anao wasema hawajibu ? Maana anayesema ni CCM mwenzao bado wanauchuna ?
 
MWENYEKITI wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema kwa sasa Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji.
Alisema kutokana na hali hiyo, kosa linapotokea katika idara wanazoziongoza hushindwa kuwajibika kwa kujiuzulu.
Akizungumza katika kipindi cha 'Je, Tutafika', kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Channel 10, alisema kuna viongozi walipaswa kuwajibika baada ya kashfa za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Alisema kama kiongozi anaweza kudanganywa na akatoa uamuzi wenye kuligharimu taifa fedha nyingi, hastahili kuendelea kuishikilia nafasi hiyo.
"Wananchi watawezaje kulala kama kiongozi wanayemtegemea anaweza kudanganywa na akapitisha uamuzi wenye athari kwa taifa?" alihoji Butiku.
Alisema hayati Mwalimu Julius Nyerere aliweka misingi imara ya uwajibikaji kwa viongozi wake, lakini misingi hiyo hivi sasa inaelekea kutofuatwa.
Alisema kuna kipindi wanajeshi mkoani Mwanza waliwapiga raia na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wakati ule, Ali Hassan Mwinyi, aliamua kujiuzulu, jambo lililomjengea heshima zaidi.
"Alichokifanya Mwinyi wakati ule ndiyo uwajibikaji ambao hivi sasa haupo….. kila kiongozi anajiangalia mwenyewe, huu ni udhaifu mkubwa," alisema Butiku.
Naye msomi maarufu nchini, Profesa Mwesiga Baregu, akizungumza katika kipindi hicho, alisema tatizo la kutokuwa na viongozi imara ndilo ambalo limesababisha kuvunjika kwa dhana ya kujitegemea.
Alisema kuvunjika kwa dhana hiyo kunawafanya Watanzania waendelee kutegemea misaada ya wahisani wakati wana rasilimali za kutosha.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alisema makosa ambayo Tanzania inayajutia hivi sasa ni zoezi la ubinafsishaji.
Alisema dhana hiyo imewarudisha Watanzania katika enzi za umanamba na kuwa vibarua wa wageni ambao hivi sasa wanamiliki uchumi wa nchi.
"Wageni kamwe hawawezi kunusuru uchumi wa nchi, wao huangalia zaidi wanachopata, hapo ndipo Tanzania imekosea, kuruhusu uwekezaji," alisema Mvungi.
Alisema hayati Mwalimu Nyerere alijenga dhana ya kujitegemea, ili kila Mtanzania aweze kupata neema ya rasilimali zilizopo kwenye nchi yake.

Source: Tanzania Daima

Iri ributiku rina usongo si rilafiki rake ririkosaga kukamataga madalaka. rire riarabu ra pemba. ririkuwa rikubwa ra aflika. sasa rinajidai heti rinatetea, renyewe riritumia mipesa ya rire rimufuko ra nyelele iri rikamusaidie rilafiki rake ripewe madalaka. hii mikuriya inajidai kuwa yenyewe ni miarabu ati siyo mibantu. si ndio maana ri nyelele ririkuwa na miwazili chungu mbofu ya kialabu siji ya kihindi. kwenda butiam ukarare ukare mipesa ariyoiiba nyelele. ukasari katika rire ri msikiti arirowacha riusia nyelele rijengwe akisha torewa ri loho rake. si angerijenga hiro ri msikiti kabla arijakufaga.rabuda rimgesaidia kuriomba hiro rimungu renu rimuokowe.sasa rimekifa hiro rimsikiti ritamufanyaga aje. hii mijitu minigine siierewi. au harijapataga mugao toka rife rinyelele. rimeamua kuwa rinaa.
 
Back
Top Bottom