Kila mara tunaambiwa humo humo ndani ya CCM bado wamo watu waadilifu. Watu hao hawaonekani kwa sababu wanaogopa kupoteza nafasi zao.
Panapotokea watu kama Butiku aliyemo CCM, na akawa na ujasiri wa kusema wanaCCM wenzake ni dalili nzuri. Pengine hata hao wazuri ambao ni waoga huenda siku moja wakadandia kwa ujasiri wa huyu mmoja, hata kama na yeye sio malaika. Vinginevyo hatuwezi kujua uzuri wa hao wanaoendelea kukaa kimya wakiendelea kuchunga maslahi yao.
Butiku kama ni fisadi na bado anao ujasiri wa kuwasuta mafisadi wenzake, basi ufisadi wake tutauvumilia hadi hapo ushahidi utakapoonyesha ufisadi wake ulivyo.