Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
MWENYEKITI wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, amesema kwa sasa Tanzania imekosa viongozi wawajibikaji.
Alisema kutokana na hali hiyo, kosa linapotokea katika idara wanazoziongoza hushindwa kuwajibika kwa kujiuzulu.
Akizungumza katika kipindi cha 'Je, Tutafika', kinachorushwa na kituo cha Televisheni ya Channel 10, alisema kuna viongozi walipaswa kuwajibika baada ya kashfa za ubadhirifu wa mabilioni ya fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Alisema kama kiongozi anaweza kudanganywa na akatoa uamuzi wenye kuligharimu taifa fedha nyingi, hastahili kuendelea kuishikilia nafasi hiyo.
"Wananchi watawezaje kulala kama kiongozi wanayemtegemea anaweza kudanganywa na akapitisha uamuzi wenye athari kwa taifa?" alihoji Butiku.
Alisema hayati Mwalimu Julius Nyerere aliweka misingi imara ya uwajibikaji kwa viongozi wake, lakini misingi hiyo hivi sasa inaelekea kutofuatwa.
Alisema kuna kipindi wanajeshi mkoani Mwanza waliwapiga raia na aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wakati ule, Ali Hassan Mwinyi, aliamua kujiuzulu, jambo lililomjengea heshima zaidi.
"Alichokifanya Mwinyi wakati ule ndiyo uwajibikaji ambao hivi sasa haupo .. kila kiongozi anajiangalia mwenyewe, huu ni udhaifu mkubwa," alisema Butiku.
Naye msomi maarufu nchini, Profesa Mwesiga Baregu, akizungumza katika kipindi hicho, alisema tatizo la kutokuwa na viongozi imara ndilo ambalo limesababisha kuvunjika kwa dhana ya kujitegemea.
Alisema kuvunjika kwa dhana hiyo kunawafanya Watanzania waendelee kutegemea misaada ya wahisani wakati wana rasilimali za kutosha.
Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Sengondo Mvungi, alisema makosa ambayo Tanzania inayajutia hivi sasa ni zoezi la ubinafsishaji.
Alisema dhana hiyo imewarudisha Watanzania katika enzi za umanamba na kuwa vibarua wa wageni ambao hivi sasa wanamiliki uchumi wa nchi.
"Wageni kamwe hawawezi kunusuru uchumi wa nchi, wao huangalia zaidi wanachopata, hapo ndipo Tanzania imekosea, kuruhusu uwekezaji," alisema Mvungi.
Alisema hayati Mwalimu Nyerere alijenga dhana ya kujitegemea, ili kila Mtanzania aweze kupata neema ya rasilimali zilizopo kwenye nchi yake.
Source: Tanzania Daima