BUTIAMA, MARA: Serikali yavunja mkataba na TBA baada ya kumlaghai Waziri Mkuu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF,

Serikali imevunja Mkataba na Wakala wa Majengo(TBA) baada ya kutoa taarifa za uongo kwa Waziri Mkuu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Butiama na Halmashauri mpya wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Ikumbukwe kuwa Wakala huyo wa Majengo wiki iliyopita alipewa onyo na Waziri wa Elimu baada ya kusuasua kuanza maradi wa Ujenzi wa Madarasa, Ofisi za Chuo Kikuu cha Muhimbili Kampasi ya Mloganzila huku wakiwa wamepewa fedha na Serikali
 
TBA NA TANROADS atagonga mwamba tuu
 
Hilo zimwi tu TBA wezi wameajiri vilaza Watoto wa ndg zao kazi haziendi hakuna wa kimsukuma mwingine maana anamwogopa ni Mtoto wa dadake umeona ee! Serikali lazima ifike pahala itafute njia nzuri ya kujenga majengo Yake
 
Habari wanaJF,

Serikali imevunja Mkataba na Wakala wa Majengo(TBA) baada ya kutoa taarifa za uongo kwa Waziri Mkuu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Butiama na Halmashauri mpya wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Ikumbukwe kuwa Wakala huyo wa Majengo wiki iliyopita alipewa onyo na Waziri wa Elimu baada ya kusuasua kuanza maradi wa Ujenzi wa Madarasa, Ofisi za Chuo Kikuu cha Muhimbili Kampasi ya Mloganzila huku wakiwa wamepewa fedha na Serikali
Duniani kote tenda hutolewa kwa ushindani ndiyo kazi hufanyika vizuri lakini ukitoa kwa upendeleo lazima wataharibu kazi
 
Habari wanaJF,

Serikali imevunja Mkataba na Wakala wa Majengo(TBA) baada ya kutoa taarifa za uongo kwa Waziri Mkuu kuhusu maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Butiama na Halmashauri mpya wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Ikumbukwe kuwa Wakala huyo wa Majengo wiki iliyopita alipewa onyo na Waziri wa Elimu baada ya kusuasua kuanza maradi wa Ujenzi wa Madarasa, Ofisi za Chuo Kikuu cha Muhimbili Kampasi ya Mloganzila huku wakiwa wamepewa fedha na Serikali
Tenda zikitolewa kwa wageni malalamiko lukuki basi tukipewa sisi napo shida tupu.
Mungu atusaidie kwakweli tubadilike tunalaumu makocha lakini na sisi wachezaji hatujitumi...
 
Nadhani kulikuwa na makosa kurundika miradi mikubwa kwa TBA kabla ya kuwapa resources za kutosha. Si vibaya kujisahihisha kama hili ni la kweli
 
TBA wamepewa kazi nyingi kuliko uwezo wao.

Bado hawakua na man power na technical capabilities ya kuhandle projects nyingi kwa wakati mmoja.

Ni sawa na mtoto wa miezi 2 uanze kumlisha ugali na maharage na nyama juu, bado hajawa na huo uwezo.
Ukienda kinyume na mtukufu wewe si mzalendo wacha sasa wajionee wenyewe.
 
Back
Top Bottom