Phd Hewa
JF-Expert Member
- Oct 3, 2016
- 572
- 466
Wadau wa soka wana kila sababu ya kuingia hofu juu ya utendaji wa shirikisho la soka nchini (TFF) lililo chini ya Wallace Karia na Michael Wambura.
Baadhi ya maamuzi yanayofanywa shirikisho hilo linalojinasibu kudhamiria kupeleka mbele soka la Tanzania yamekuwa na 'ukakasi'.
Kumekuwa na maamuzi yasiyo na usawa kwa vilabu vinavyoshiriki ligi kuu katika masuala mbalimbali.
Nakumbuka mwanzoni mwa msimu Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa walifungiwa kutoshiriki michuano yoyote inayoandaliwa na shirikisho hilo baada ya kutuhumiwa kufanya fujo katika mchezo wa mwisho wa ligi kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC msimu uliopita.
Lakini si wachezaji hawa pekee waliostahili kusimamishwa, Haruna Niyonzima ambaye alisajiliwa na Simba yeye hakuhusishwa na rungu la TFF licha ya kuwa miongoni mwa wachezaji waliohusika kwenye sakata hilo.
Baadae TFF inakuja kuwaachia kwa kusema hawakuwa na hatia isipokuwa Simon Msuva ambaye aliomba radhi. Wachezaji hao walikuwa tayari wamekosa michezo ya mwanzo wa msimu kwa ajili tu wamesimamishwa tena bila kosa!
Huku mwenzao Haruna Niyonzima akiitumikia klabu ya Simba bila kubugudhiwa na mtu yeyote.
Huo ulikuwa ni mwanzo tu, swala la kufungiwa kiungo wa Yanga Pius Buswita tena siku moja kabla ya mchezo wa Ngao ya Jamii liliwashangaza wengi.
Buswita alituhumiwa kusajili timu mbili, Simba na Yanga lakini cha ajabu hakuwemo kwenye orodha ya wachezaji waliosajiliwa na Simba. Ni Yanga pekee iliyokuwa imewasilisha jina lake TFF.
Lakini baadae ikaja kubainika kuwa Buswita alirubuniwa na viongozi wa Simba na kuchukua pesa (Tsh Mil 10) (Mwenyewe alikiri) ili asaini klabu ya Simba.
Inadaiwa viongozi wa Simba walitumia njia za panya kufanya nae mazungumzo licha ya kufahamu alikuwa bado na makataba uliozidi miezi sita na klabu ya Mbao FC.
Yanga walifuata taratibu kwa kumalizana na Mbao FC kabla ya kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Baada ya Yanga kukata rufaa TFF ikamfungulia Buswita kwa masharti kwamba arudishe pesa alizochukua kwa klabu ya Simba.
Lakini TFF haikuiadhibu Simba iliyovunja sheria za usajili kwa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na mchezaji ambaye ana mkataba na timu nyingine.
Kwa sababu Simba imekuwa 'mtoto mpendwa' wa TFF imerudia tena mchezo huo kwa beki wa Lipuli FC Asante Kwasi.
Lipuli imethibitisha kuwa Kwasi bado ana mkataba wa miezi nane na klabu hiyo na Mwenyekiti wake Clement Sanga amethibitisha kuwa hawakuwahi kuwa na mazungumzo na uongozi wa Simba juu ya mchezaji huyo.
Wakati ukweli huo ukibainika, Kwasi amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba na upo ushahidi wa picha zinazomuonyesha akisaini mkataba huo sambamba na mchezaji mwingine kutoka Msumbiji.
Simba iliwahi kutumia ushahidi wa aina hiyo kuidai Yanga zaidi ya Mil 200 kwenye sakata la usajili wa Hassani Ramadhani 'Kessy'.
Kitendo cha Kessy kuonekana akiwa amevaa jezi ya Yanga siku tatu kabla ya mkataba wake kumalizika kuliipelekea Yanga iilipe Simba Mil 50.
Mbaya zaidi uongozi wa Lipuli FC umethibitisha kuwa Kwasi aliomba ruhusa kwenda kwao nchini Ghana kuhudhuria msiba wa Baba yake na walimtumia nauli ya kurudia ambapo alitakiwa kuripoti kambini Disemba 16.
Lakini kumbe mchezaji huyo alikuwa amefichwa jijini Dar es salaam akimalizana na viongozi wa Simba kulingana na taarifa zilizochapishwa kwenye magazeti.
Wakati sintofahamu hii ikiviibua vyombo vya Serikali ikiwemo TAKUKURU kuchunguza usajili wake, TFF inaongeza siku za kufunga dirisha la usajili kwa kisingizio kuwa mtandao wa FIFA (TMS) una hitilafu.
Wadadisi wa mambo wanafikiri TFF imetoa mwanya tu kwa 'mtoto mpendwa' kukamilisha taratibu za usajili ili akwepe adhabu.
Sakata la Kwasi ni mtihani maridhawa kwa TFF kujidhihirisha kama inafuata sheria au la ingawa kuna taarifa kuwa viongozi wa TFF wamekuwa wakifanya vikao vya siri na viongozi wa Simba ili kuhakikisha sakati hilo linamalizika salama.