Busta Rhymes Kuinogesha Fiesta Jioni Hii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Busta Rhymes Kuinogesha Fiesta Jioni Hii

Discussion in 'Entertainment' started by MziziMkavu, Nov 21, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Busta Rhymes Kuinogesha Fiesta Jioni Hii
  [​IMG]
  Busta Rhymes Saturday, November 21, 2009 5:39 PM
  MKALI wa muziki wa hip hop, Busta Rhymes anatarajiwa kutumbuiza jioni hii kwenye tamasha la Fiesta One Love linalofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Posta jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo ambalo tayari limeshaanza, na kuandaliwa na Clouds FM linafanyika kwa mara ya 10 na linashirikisha wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Ruge Mutahaba amesema Rhymes ametua nchi akiwa na kundi lake lenye wasanii tisa tayari kwa kuwapa burudani mashabiki.

  Tamasha hilo linafanyika kwenye viwanja vya kilichokuwa Chuo cha Kampuni ya Simu Tanzania, Kijitonyama, Dar es Salaam.

  Mutahaba alisema nyota wa hip hop atatumbuiza kwa muda wa saa moja na nusu bila mapumziko lengo ni kuwapa burudani ya kutosha mashabiki wake na kwamba mwaka huu tamasha hilo litakuwa la aina yake.

  Alisema litakuwa majukwaa matatu ambayo yote yatakuwa bize na hakutakuwa na muda wa kupumzika kwa wasanii.

  "Rhymes ni msanii mahiri ambaye amewahi kupata tuzo mbalimbali za billboard, ni msanii anayebadilika kulingana na mazingira anakubalika kwa vijana na wazee,"alisema mratibu huyo.

  Baadhi ya nyimbo ambazo anatamba nazo msanii huyo ni pamoja na Arab money, Turn it Up, Woo Hah, Make it Clap ambao kamshirikisha Spliff Star, Hey Ladies, I ever saw on.

  Msanii huyo wa kimataifa atashirikiana na wasanii wa wazawa wakiwamo Ali Kiba, Marlow, Barnabas, Daz Nundaz, Bushoke, TMK Famili, Juma Nature na Wanaume Halisi, Profesa Jay, Belenine, Hussein Machozi, Lady Jaydee na Ray C

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=3588010&&Cat=8
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,523
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  and if you dont know noow you know..................ft big tyger
   
Loading...