Business Opportunity in DNA Testing (tujadili, anayeweza ajitose) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Business Opportunity in DNA Testing (tujadili, anayeweza ajitose)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Dar_Millionaire, Apr 10, 2009.

 1. Dar_Millionaire

  Dar_Millionaire JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2009
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Wadau,

  Nina uhakika kuna baadhi yenu kama mimi idea ya kuinvest kwenye DNA testing itakuwa imeshacross your minds.

  Ila baada ya kupitia article ya Michuzi leo nadhani hakuna ubishi kuwa kuna pesa kibao ziko nje nje.

  MICHUZI

  Ukiangalia market analysis:

  1. Inaelekea kuna service provider (SP) mmoja ambaye ni Mkemia Mkuu wa Serikali.
  2. Service provider huyo ana ukiritimba wa hali ya juu kwamba mteja haruhusiwi kupata huduma isipokuwa kwa kupitia kwa Mwanasheria au Afisa Ustawi wa Jamii.
  3. SP ana products mbili ambazo ni (i) kuthibitisha mtoto kama ni wa baba yake na (ii) kuthibitisha uhusika wa watuhumiwa katika kesi mbalimbali

  Katika mazingira ya kawaida kwa mjasiriamali perhaps kuuza product namba (ii) hapo juu itakuwa ngumu, lakini product namba (i) ambayo ndio iko very sensational na potential customers ni wengi itakuwa rahisi sana kuuza.

  CHALLENGES

  1. Uhalali na ubatili wa matokeo

  Kuna mdau mmoja pale kwa Issa Michuzi (ambaye ni mtoa maoni anon wa April 10, 2009 7:34 AM) kahoji uhalali wa matokeo kwamba inawezekana TANESCO walifanya vitu vyao wakati testi inaendelea, n.k.

  Hivyo njia mojawapo kwa mjasiriamali atayekuwa tayari kuwekeza katika sekta hii kuondoa mashaka na kupata publicity baaab kubwa ya bure ni kufanya test hadharani au kwa kualika wanafamilia idadi fulani (eg 10, watano toka upande wa mama watano toka kwa baba) ili kushuhudia LIVE test inavyokwenda.

  Pia mjasiriamali huyo itabidi atoa elimu kwa umma jinsi DNA test inavyofanyika, matokeo huwa yanakuwaje na yanatafsiriwaje, vitu gani vinaweza kuathiri matokeo yakawa batili, na vitu gani haviwezi kuathiri matokeo.

  2. Sheria zikoje?

  Je kuna sheria yoyote inayozuia wajasiriamali kufanya biashara ya DNA testing? Hii setup ya sasa aliyozungumzia Mkemi Mkuu inajenga taswira fulani mbaya kana kwamba hii ni sekta ambayo iko regulated kwamba mpaka wanasehria na maafisa ustawi wa jamii wawe involved.

  Kama kuna kesi kuhusu paternity well and good, lakini kutokana na reaction ya wato maoni wachache pale kwa michuzi, na general common sense ni lazima kutakuwa na mamilioni ya wananchi ambao wangependa tu kujua kwamba watoto wanaolea ni wao ama la.

  Tujadili...
   
 2. M

  Mkora JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 360
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mkuu nchi ina opportunity ya kila aina sasa ukitaka kuwekeza itabidi mtu mwingine ajiingize kati (halafu hatoi chochote)
  Ukifanya mwenyewe utapoteza kila kitu
   
 3. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,307
  Trophy Points: 280
  Mkuu DM,

  Umefanya good observation and analysis.

  Ni kweli kuna kila sababu ya kuwekeza kwenye mradi wa namna hii lakini sisi watanzania ni wavivu na waoga kutake chance/risks ama tunadharau

  On the other hand tatizo kubwa tulilonalo kwa Tanzania ni Capital, kuwekeza kwenye mitambo ya DNA testing sio mchezo ingawa sijui exactly ni kiasi gani. Nimesema hivyo maaana nimeona offisi ya Mkeamia imefanya tests chini ya 1000 kwa miaka 3, je ni ugumu wa kufanya hizo test ndio maana wanafanya on average moja kwa siku? Ama ni garama za kufanya hizo test ndio ziko juu? au ni upatikanaji wa vitendea kazi ndio umefanya hiyo hali??? ama hakuna mahitaji makubwa????

  Kitu kingine muhimu kwa Tanzania ni kuanzisha DNA database kiasi kwamba mtu ameugua kafariki, kaungua moto, kapata ajali basi utambulisho wake unaweza kufanywa kwa kutumia DNA. Hii ndio inaweza kuwa njia pekee ya kucreate demand ya huduma ya DNA test
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...naamini kuhusishwa kwa mkemia mkuu wa serikali kupitia kwa mwanasheria ama maafisa wa ustawi wa jamii ni katika kumlinda mama na mtoto, kwani reaction ya baba/wababa baada ya kupewa majibu ya hapana, athari zake huenda zikawa kubwa kuliko inavyotarajiwa.

  Kwa maoni yangu, uchunguzi huo uendelee kuwa mikononi mwa mkemia mkuu wa serikali kuratibu mapokeo ya jamii husika, mpaka hapo zoezi litapoeleweka. Takwimu tayari zinajionyesha karibia 60% ya sampuli 250 zilizokusanywa mwaka 2005/2006 kina baba wamebambikiwa mimba nchini Tanzania.

  wataalamu washeria watazidi kutufafanulia, wakati huo huo vipi kuwekeza kwenye huduma ya ushauri (counselling i.e marriage, fostering, adoption, divorce, etc )?
   
Loading...