Bush kutembelea Ngorongoro creater

Mpaka Kieleweke

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
4,132
1,571
Taarifa rasmi zilizotolewa na waziri wa utalii na maliasili dakika mbili zilizopita wakati anatoa majumuisho ya hoja za utalii ni kuwa Rais Bush atatembelea Ngorongoro crater wakati wa ziara yake hapo tarehe 16 mwezi huu.

Je?matembezi hayo yatalinufaisha vipi taifa?

Je?wananchi wa Ngorongoro wataweza kunufaika vipi na ujio huo?

Wizara ya utalii na maliasili wanaweza kumudu kuhakikisha kuwa safari jhiyo inatumika kulitangaza taifa?

Je?hii ni safari ya kikazi ya rais Bush ama ni ziara ya kuja kutalii?
 
MK,

Pamoja na kutokumpenda Bush lakini naamini kwenda kwake Ngorongoro Crater ni
advertisement tosha kwa Tanzania na Ngorongoro yenyewe.

Ni matumaini yangu Watanzania watafaidika inderectly na hiyo safari yake.

Dunia ya leo watu wanaangalia interests, kuja kwa Bush Tanzania huenda kukawa na faida kuliko hasara. Faida kubwa itakuwa upande wa utalii na pia
services hasa kwa hotel na hao wanaofanya kazi hotelini.
 
MK,

Pamoja na kutokumpenda Bush lakini naamini kwenda kwake Ngorongoro Crater ni
advertisement tosha kwa Tanzania na Ngorongoro yenyewe.

Ni matumaini yangu Watanzania watafaidika inderectly na hiyo safari yake.

Dunia ya leo watu wanaangalia interests, kuja kwa Bush Tanzania huenda kukawa na faida kuliko hasara. Faida kubwa itakuwa upande wa utalii na pia
services hasa kwa hotel na hao wanaofanya kazi hotelini.


Hivi atakuwa anatoa tip kama watalii wengine? LOL
 
Lo!

Tanzania wamemkuna nini Bush??

Yaani out of 7 days in Africa he will spend 4 in Tanzania?

Why?
 
Mzalendohalisi,

Nafikiri hili ni jambo zuri sana maana kuna Watanzania watafaidika.

Namsifu JK kwa kufanikisha hii ziara. I hope hawataanza kuitumia kisiasa
maana Bush anakuja kwasababu ya Watanzania wote.

Laiti baadhi yetu tungeamua kuchukua mapanga na rungu wala asingeliweza kuja TZ.
 
Sometimes last year nilimuona Clinton kwenye Oprah naye alikuwa anazungumzoa jinsi alivyokuwa amazed na Ngorongoro Crater na Serengeti na akasema atawashauri marafiki zake watembelee, so you never know labda amemwambia Bush Jr.
 
Rais Bush wa Marekani kukaa Tanzania siku nne ziara ya Afrika
*Kutembelea Arusha, Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu


Rais George Bush anatarajiwa kukaa kwa siku nne nchini Tanzania kati siku saba za ziara yake kutembelea Bara la Afrika.


Akizungumza katika kikao cha wahariri kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jana, Msemaji wa ubalozi wa Marekani nchini, Jeffery Salaiz alisema katika ziara hiyo Rais Bush atatembelea mikoa ya Dar es Salaam na Arusha.


Alisema kwamba ziara hiyo ina malengo makuu matatu, ambapo kwa pamoja yanadhihirisha nia ya Marekani kuijali Afrika.


Wakati wa ziara hiyo, Bush atakagua baadhi ya miradi mbalimbali ambayo serikali chini ya uongozi wake imekuwa inasimamia na kufadhili kwa karibu.


Alitaja miradhi hiyo kuwa ni ya Ukimwi na Malaria ambayo kwa sehemu kubwa imesaidia idadi ya wagonjwa na vifo vitokanavyo na malaria katika Visiwa vya Pemba.


Rais Bush anatarajiwa kuanza ziara ya kutembelea nchi tano za Afrika kuanzia Februari 15 hadi 21. Nchi hizo ni Benin, Tanzania, Rwanda, Ghana and Liberia.


Marekani ni moja ya nchi ambazo ni wafadhili wakubwa kwa Tanzania, ikiwa imetoa Sh700 bilioni kwa mwaka huu. Kuanzia mwaka 2003 Marekani imetoa zaidi ya Sh700 bilioni kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya Ukimwi.


Katika mradi wake wa kupambana na malaria, Marekani imekwishatoa zaidi ya Sh77 bilioni.


Ziara ya Bush inatarajia kujenga uhusiano mzuri kati ya nchi hizi mbili na kuitangaza Tanzania duniani kwa kuwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa wanatarajiwa kuaambatana naye.


Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Marekani kukaa Tanzania kwa siku nne kwani mara ya mwisho Rais wa nchi hiyo, Bill Clinton alipotembelea nchini mwaka 2003 alikaa nchini kwa masaa matatu tu.
 
Zamani wazungu walileta vioo na ushanga, wakaondoka na almasi na dhahabu na mali kede-kede.

Sasa bush anakuja, ujuwe si bure, ya amma kuna mafuta yamegundiliwa kwa wingi, anakuja kuhakikisha wamerekani ndio watakuwa wakombaji wakuu, amma kuna ngome ya kijeshi anataka kuiweka hapa kwetu. Amma kuna uranium anataka kuwa wamerekani wawe wachimbaji pekee.

Au unafikiri zile dola walizoidhinisha kutupa ni za bure? haiwezekani hata kidogo. Lazima ana anachokifata si kuona wanyama wa ngorongoro. NgoroNgoro alisha kuja zamani hata kabla hajawa rais.
 
jamani jamani mweee!.

Hivi kweli mnaamini Bush kutembelea Ngorongoro kutaleta matunda?... ataitangaza vipi maanake sijasikia hata siku moja rais akitembelea sehemu fulani kunakuwepo na matangazo ama umuhimu wa watu wa nchi nyingine kuelewa Bush ati alifika sehemu gani.

Kisha tembelea nchi kibao sasa nyie mnambieni mimi ni sehemu zipi mnazozikumbuka zilitembelewa na Bush leo hii ni tangazo tosha kwa sehemu hiyo?

Jukumu la kuitangaza Ngorongoro ni letu wenyewe na wala Bush ambaye anamaliza wakati wake hawezi kuitangaza Ngorongoro tena basi kulingana na chanzo cha ziara za Bush Tanzania tumekuja pewa nafasi hiyo baada ya machafuzi Kenya. Mwanzo wa safari zake Afrika Kenya ndio iliyokuwa imepewa kipaumbele lakini baada ya machafuko ndio sisi tumepewa... na navyosikia ( tetesi) ni kutokana na sisi kukubali Marekani kuweka kambi yao Tanzania.

Hizi habari hadi leo hii sidhani kama zimeisha jadiliwa bungeni na kupitishwa isipokuwa zinatembea chini chini na wananchi tutakuja shitukizwa na kama kawaida yetu mijadala baada ya kupigwa goli...
 
Ningekuwa na sauti nisingetaka huyu jamaa atembelee nchi yetu maana sioni umuhimu wowote wa yeye kutembelea Tanzania. Hawa jamaa urafiki wao ni wa kinafiki, wanapotaka urafiki basi ujue wanataka kukutumia kwa namna moja au nyingine ili wakidhi matakwa yao. Saddam pia alikuwa rafiki yao mkuu mnajua yaliyotokea pale alipoamua kutofuata matakw yao. Kuna nchi chungu nzima duniani ambazo tunaweza kuwa na urafiki nazo lakini si hawa jamaa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom