Bush atetea mbinu za kuwatesa wafungwa

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,266
33,039
Aliyekuwa Rais wa Marekani, George W Bush, ametetea maamuzi yake yaliyosababisha utata mkubwa wakati wa mahojiano yake ya kwanza kwenye televisheni tangu aondoke madarakani.

101103082142_bush304.jpg
George Bush

Akizungumza kweye kituo cha televisheni cha Marekani cha NBC, Bw Bush alitetea mbinu ya kuwatesa wafungwa kwa kuwazamisha ndani ya maji wakati walipokuwa wakihojiwa, akisema ilisaidia kuokoa maisha na kuzuia mashambulio ya kigaidi.
Amesema uamuzi wake wa kuvamia Iraq haukuwa na kasoro na dunia kwa sasa ni salama zaidi bila Saddam Hussein.
Pia alitetea uamuzi wake wa kuyanusuru mabenki ya Marekani yaliyoporomoka kutokana na mdororo wa kiuchumi duniani.
Bwana Bush amesema anatarajia kuwa historia itatambua mafanikio yake ingawa atakuwa ameaga dunia kabla swala hilo kutokea.

Chanzo: BBC Swahili - Habari - Bush atetea mbinu za kuwatesa wafungwa

huyu Bush ni shetani mkubwa aliwatesa sana Wafungwa Mungu atamlipa inshallah
 
Kweli mbaya huyu Bush!!!!!!
Lakini kama serikali ya nchi nyingi hasa nchi za Kiislamu wale wenye utaratibu wa shari'a wasingekuwa wakali kuliko Bush - tayari dunia ingekuwa na maendeleo kuhusu haki za kibinadamu.

Maana nani anashtakiwa kama mtu anapigwa huko Afghanistan (eneo la Taliban), Saudia (nchi ya hajj na Makka), Misri . . . . . . Somalia???
 
Kipala wakati mwengine unachozungumza kiko out of Point tunamzungumzia huyu Shetani mkuu wa karne hii George bush hatuzungumzii matatizo ya Nchi za Afghanistan (eneo la Taliban), Saudia (nchi ya hajj na Makka), Misri . . . . . . Somalia? hebu anzisha Topic za hizi nchi utajibiwa Bwana . Tunachosema madhambi ya bush aliyoyafanya huko Iraq katu hatutosahau bush kauwa Raia wa iraq wapatao Millioni moja yeye huyo Bush akishirikiana na Shetani Mwenzie mkubwa Tony Blair Damu za ndugu zetu wa iraq kamwe hazitosahaulika na Mlipaji mkuu wa hizo Damu ni Mwenyeezi Mungu.
 
Kikwete si kwa Kujigamba kabisa alitamka waziwazi huko kwetu Kigamboni kuwa Bush ni rafiki yake Mkubwa? Bush = kikwete, kuwaua kina mama wajawazito mahospitalini, kuifanya Tanzania iwe nchi ya Familia yake mi sioni tofauti na bush muuaji...
 
kwa kweli vitu vingi tunavyofanya hap aduniani
Mwenyezi Mungu anajua hukumu yetu....
kwa mimi binafsi sijaona sababu yeyote ya Bush
kusababisha kifo cha Sadam Hussen ...
angemfunga tu kifungo cha maisha ...
nway kwa kweli tusubirie tu hiyo siku ya hukumu

kwa sabau watu kama sisi tutaongea tu hatumtaki fulani
kwasabau alifanya hichi...
lakini mtu kama Bush maneno yetu haya mwingii
na hata hatujui......
 
Kikwete si kwa Kujigamba kabisa alitamka waziwazi huko kwetu Kigamboni kuwa Bush ni rafiki yake Mkubwa? Bush = kikwete, kuwaua kina mama wajawazito mahospitalini, kuifanya Tanzania iwe nchi ya Familia yake mi sioni tofauti na bush muuaji...
Mkuu Magulumangu mbona umefika mbali huko ulikokwenda? Mtu kuwa na rafiki shetani sio mbaya Urafiki wa Rais J.Kikwete na shetani mkuu wa dunia bush ni sawa na Mtu kuwa na rafiki na Simba tu. Iko siku huyo Rafiki yako Simba atakugueukia tu. Mkuu Magulumangu usimfananishe Mzee Kikwete na shetani Bush.
 
Kipala wakati mwengine unachozungumza kiko out of Point tunamzungumzia huyu Shetani mkuu wa karne hii George bush hatuzungumzii matatizo ya Nchi za Afghanistan (eneo la Taliban), Saudia (nchi ya hajj na Makka), Misri . . . . . . Somalia? hebu anzisha Topic za hizi nchi utajibiwa Bwana . Tunachosema madhambi ya bush aliyoyafanya huko Iraq katu hatutosahau bush kauwa Raia wa iraq wapatao Millioni moja yeye huyo Bush akishirikiana na Shetani Mwenzie mkubwa Tony Blair Damu za ndugu zetu wa iraq kamwe hazitosahaulika na Mlipaji mkuu wa hizo Damu ni Mwenyeezi Mungu.

Ni kweli Bush anawajibika kwa vifo vya Iraq.
Bahati mbaya idadi kubwa ya mauaji yametekelezwa na Wairaqi (wanamigambo Wasunni, Washia, wafuasi wa Saddam) wenyewe au Al Qaida. Ni hao walioua wengi zaidi kuliko wanajeshi wa Marekani.
Lakini nakubali: wajibu kwake George W.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom