Busega: Aua Mkewe kisha naye kujinyonga kutokana na tuhuma za kusaliti Ndoa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Edward Manyangu (41) mkazi wa kijiji cha Ijitu Wilaya ya Busega mkoani Simiyu anadaiwa kumuua mkewe, Dalali Maunga (41) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao akizungumza leo Jumanne Mei 11, 2021 amesema tukio hilo lilitokea jana Mei 10, 2021 baada ya wanandoa hao kuingia kwenye mvutano kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kuwa na uhusiano nje ya ndoa.

“Baada ya kutekeleza mauaji hayo, Manyangu naye alijiua kwa kujinyonga kwa kamba aliyofunga juu ya mti ulioko nje ya nyumba yao,” amesema Kamanda Abwao

Amebainisha kuwa kwa mujibu wa ujumbe wa maandishi unaoaminika kuandikwa na kuchwa na Manyangu, alikuwa akimthumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.

Kamanda Abwao amesema baada ya uchunguzi wa kitabibu, miili ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Mwananchi
 
Kabla sijachangia naomba niseme sentesi haijakamilika; siku zote lazima uandike "kitu kizito chenye ncha kali" hata kama ni rungu
 
Hizi habari bana, unaweza fikiria hawa watu hawna purpose kwenye maisha?, kweli mtu anaona hana sababu nyingine ya kuishi kabisa au vp?

Kumbe unakuta ulikua ugomvi wa kawaida tu jamaa akamtwanga la kichwa akapata head injury akafa nae akajiua kwa baada ya kuwa shocked.

Sizani kama mtu mwenye akili za kawaida ana amka asubuhi kupanga kumuua mkwewe kisha nae kujiua!
 
Ncha kali lazima iwe ncha kweli kama panga, sime au kisu. Rungu halichomi hivo sio ncha kali
 
Huku kanda ya ziwa hukuwezi mkuu.....
nenda nyanda za juu kusini kaoe wajukuu wa chifu Mkwawa.....
Wahehe wako loyal huwezi amini. Ila siwezi kaa nao poa, sasa Wasukuma huwa nawaelewa lakini kila siku wanauana wao uko. Hivi kule Zanzibar watu huwa wanauana hivi?
 
Edward Manyangu (41) mkazi wa kijiji cha Ijitu Wilaya ya Busega mkoani Simiyu anadaiwa kumuua mkewe, Dalali Maunga (41) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao akizungumza leo Jumanne Mei 11, 2021 amesema tukio hilo lilitokea jana Mei 10, 2021 baada ya wanandoa hao kuingia kwenye mvutano kutokana na mwanaume kumtuhumu mkewe kuwa na uhusiano nje ya ndoa.

“Baada ya kutekeleza mauaji hayo, Manyangu naye alijiua kwa kujinyonga kwa kamba aliyofunga juu ya mti ulioko nje ya nyumba yao,” amesema Kamanda Abwao

Amebainisha kuwa kwa mujibu wa ujumbe wa maandishi unaoaminika kuandikwa na kuchwa na Manyangu, alikuwa akimthumu mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine.

Kamanda Abwao amesema baada ya uchunguzi wa kitabibu, miili ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Mwananchi
Kichwa cha habari sahihu kabisa. TUHUMA ZA USALITI WA NDOA. siyo wengine wanaandika WIVU WA MAPENZI.
 
Wanawake wa kisukuma wanagawa sana yaani...
Wahehe wako loyal huwezi amini. Ila siwezi kaa nao poa, sasa Wasukuma huwa nawaelewa lakini kila siku wanauana wao uko. Hivi kule Zanzibar watu huwa wanauana hivi?
 
Hizi habari bana, unaweza fikiria hawa watu hawna purpose kwenye maisha?, kweli mtu anaona hana sababu nyingine ya kuishi kabisa au vp?

Kumbe unakuta ulikua ugomvi wa kawaida tu jamaa akamtwanga la kichwa akapata head injury akafa nae akajiua kwa baada ya kuwa shocked.

Sizani kama mtu mwenye akili za kawaida ana amka asubuhi kupanga kumuua mkwewe kisha nae kujiua!
Kuua bila kukusudia kweli kupo,
Vipi kujiua nako, inawezekana bila kukusudia??? Labda kama ndio ile unajinyonga huku mkononi una kisu mda wa kuteseka ukizidi unakata kwanza upumzike/ubadilishe kamba au uendelee na maisha.
 
Ncha kali lazima iwe ncha kweli kama panga, sime au kisu. Rungu halichomi hivo sio ncha kali
Hiyo ni kwa mujibu wa wenye sentesi yao, kumbuka yule mwandishi wa habari aliyeuawa Mufindi enzi za mkwere, walisema amepigwa na kitu kizito chenye ncha kali, na huu ni mwendelezo
 
Back
Top Bottom