Indume
Member
- Apr 11, 2011
- 81
- 36
Hivi karibuni Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA alitangaza kuongeza ama kusogeza muda wa kufanyika kwa uchaguzi wa nafasi mbalimbali za chama ndani ya CHADEMA. Nilifuatilia kwa makini maoni ya wadau kuhusu mabadiriko ya muda ikaonekana ni kweli muda ulioongezwa wa mwaka mmoja ni mzuri kwa kuangalia namna ya kuwapata viongozi makini wa kuipeleka CHADEMA Magogoni 2015.
Kwa hali jinsi ilivyo katika mikoa (baadhi )hapa nchini, kumekuwepo na mvutano wa kimasilahi na kutokuelewana kwa viongozi na watendaji ndani ya CHADEMA kiasi cha kuleta vurugu nyingi za kisiasa zinazoonekana kuvuruga kabisa mkakati wa "Vuguvugu la Mabadiriko" - M4C. Mkoani Mwanza, Arusha na hata maeneo mengine tumeshuhudia Madiwani wengine wakifutwa uanachama, wengine wakikimbilia Mahakamani na hata wengine kukaa kimya tu kwa kile kinachoonekana sasa ni kama vurugu za kisiasa ndani ya CHADEMA ambayo ninaamini pia ndo ukomavu wa kisiasa. Lakini siyo siku zote ni kweli kuwa misukosuko hii inakomaza siasa bali mingine inaua kabisa harakati za kisiasa. Mikoa ambayo tayari imeonekana ni migumu kisiasa ndani ya CHADEMA kama Mwanza basi ni busara kutafakari kwa kina chanzo cha vurugu, athari zake, na nani atakaye simama imara kuleta muunganiko wa fikra CHADEMA.
Kwa hali hiyo ninatoa rai kuwa chaguzi zinazokuja za CHADEMA itumike busara kabisa ili kuwapata Viongozi/watendaji ambao wataelewa nini CHADEMA inataka kufanya kulingana na misukosuko yote hii. Hata wale waliosimamishwa, kufukuzwa , ama bado wamekaripiwa tukumbuke pia huenda wana timu itakayoshiriki kikamilifu katika chaguzi zijazo. Kwa hiyo ni BUSARA zaidi itumike kuwapata viongozi thabiti wanaoendana na kauli mbiu ya sasa "Movement for Changes" ili kuiandaa jamii kufanya mabadiriko ya maamuzi ifikapo 2015. Kila jambo jema litawezekana 2015.