Busara za Dr. Slaa imekuwa Lulu kwa Kinana na CCM

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
1,500
Kweli siasa is always the game. Wameponda upinzani weeeee, halafu baadaye unakuja na busara zake chumbani!
Hongera mzee wetu Kinana kwa jambo jema, maana watanzania wanahitaji maendeleo, na siyo kila kisemwacho na upinzani ni kibaya.
Umeonyesha kuwa at least unataka kuijenga ccm imara kwa busara za chadema............ tunaomba Mwenyekiti wako aige mfano wako:

KATIBU Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechota busara za Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kwa kuitaka serikali iondoshe kodi kwenye vifaa vya ujenzi ili kutoa motisha kwa wananchi kujenga nyumba za bei nafuu.

Hoja ya kutaka vifaa vya ujenzi kama vile mabati, saruji na nondo vipunguzwe bei ili kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora iliasisiwa na Dk. Slaa na kuingizwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA na kutumika kumnadi Dk. Slaa kwenye mikutano ya kampeni za urais mwaka 2010.

Wakati Dk. Slaa akitumia kete hiyo kujinadi nchi nzima, alisema CHADEMA ikiingia madarakani itahakikisha bei ya saruji, mabati, nondo na vifaa vingine vya ujenzi vinapungua bei hadi kufikia sh 5,000, badala ya bei ya wakati ule, ambapo mfuko mmoja wa saruji ulikuwa unauzwa kwa sh 15,000.

Hadi sasa bei ya vifaa hivyo iko juu zaidi ikilinganishwa na mwaka 2010 na hali hiyo imeendelea kuwa kikwazo kwa watu wa kipato cha chini kuweza kujenga na kumiliki nyumba.
Wakati akiinadi sera hiyo iliyomo kwenye Ilani yao ya uchaguzi, Dk. Slaa alisema vifaa hivyo vya ujenzi vinaweza kuuzwa kwa bei poa na kuwawezesha wananchi kumiliki nyumba zao.
Alisema CHADEMA itakapoingia madarakani, itapunguza kodi na kutoa ruzuku ya mabilioni ya fedha kila mwezi kwa viwanda vinavyozalisha vifaa vya ujenzi wa nyumba ili ziuzwe kwa bei rahisi.

Hata hivyo hoja hiyo ilionekana kuwasumbua sana CCM kwa kumwita Dk. Slaa muongo na kisha kumwita Meneja wa Kiwanda cha Saruji cha Wazo Hill, kinachozalisha saruji ya Twinga Cement ili kutoa ufafanuzi.
Katika ufafanuzi wake, meneja huyo alisema ni vigumu kwa bei ya saruji kupungua kwa kiwango cha sh 5,000 anachotaka Dk. Slaa kutokana na ugumu wa upatikanaji wa malighafi.
Lakni akisoma maazimio ya Mkutano Mkuu wa Nane wa CCM taifa juzi mjini Dodoma, Kinana ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maazimio, alisema CCM inatambua kwamba kila Mtanzania ana haki ya kuishi katika nyumba bora na iliyo na staha, hivyo mkutano mkuu unaiagiza serikali itoe kipaumbele katika suala la ujenzi wa nyumba, hasa nyumba za kupanga au kununua kwa bei rahisi.

"Mkutano Mkuu unaiagiza serikali katika kutekeleza Ilani ya uchaguzi kuhusu sekta hii, ichukue hatua zifuatazo; mosi, kutoa motisha kwa ujenzi wa nyumba bora na za bei nafuu kwa kuangalia uwezekano wa kuondoa kodi katika vifaa vya ujenzi wa nyumba kama vile saruji, mabati, nondo na vingine.

"Pili, kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika nyumba za bei nafuu zinazojengwa na kuuzwa na mashirika ya kiserikali na ya sekta binafsi ili kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kumudu kuzinunua kwa njia ya mikopo," alisema Kinana.

Katika azimio hilo, Kinana na kamati yake walikwenda mbali zaidi kwa kutaka utaratibu wa kujenga au kununua nyumba urahisishwe kwa Benki Kuu kudhibiti riba na kuitaka serikali ianzishe taasisi itakayosimamia na kudhibiti kodi za pango la nyumba ambazo hivi sasa ni kubwa mno na zinatozwa kwa mwaka mzima, hivyo kuwatesa wapangaji hususan wa kipato cha chini.

Akizungumza na Tanzania Dima Jumapili kuhusu sera ya CHADEMA aliyokuwa akiinadi kuchukuliwa na CCM, Dk. Slaa alikumbusha jinsi ambavyo Rais Jakaya Kikwete na CCM walivyowaita waongo wakati CHADEMA walipokuja na sera ya matumaini kwa Watanzania mwaka 2010, wakisema nyumba za tembe na nyasi sasa basi na kueleza mikakati yao ya kushusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi.

"Nimefurahi juzi kusikia CCM katika maazimio ya Mkutano Mkuu wao wakisema watashusha bei ya saruji na vifaa vya ujenzi. "Sasa CCM na CHADEMA nani waongo? Mimi nasema hakuna kitu kinachotushangaza katika uongozi wa sasa wa CCM," alisema Dk. Slaa.

Wakati sera nyingine ya CHADEMA mwaka 2010 ilitaka elimu ya msingi kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne iwe bure na iwe haki ya msingi ya kila mtoto, CCM katika maazimio yake imeitaka serikali kutazama uwezekano wa kuifanya elimu ya sekondari kuwa ya wote ili fursa hiyo ipatikane kwa watoto wote na iwe ni haki ya msingi kwa kila mtoto nchini.

Baadhi ya maazimio mengine yaliyopitishwa na mkutano huo mkuu ni pamoja na suala la nidhamu na uwajibikaji ambapo wajumbe wameiagiza Halmashauri Kuu (NEC kuendelea na zoezi la kuwabaini na kuwaondoa viongozi na watendaji wa chama wanaokwenda kinyume cha maadili ya uongozi na wanaokipaka matope chama.

"Mkutano Mkuu pia unaiagiza serikali kuwachukulia hatua kali na za haraka viongozi na watendaji wa serikali ambao ni wala rushwa, wabadhirifu na wanaotumia vibaya madaraka yao," alisema Kinana wakati akisoma maazimio hayo.

Maazimio mengine ni pamoja na kuitaka serikali kupandisha kipato cha wafanyakazi kwa kuzingatia upandaji wa gharama za maisha na sekta binafsi pia isimamiwe kutekeleza azima hiyo ya CCM wakati kwa upande wa wakulima, chama hicho kimeitaka serikali iongeze kasi ya usambazaji nishati ya umeme vijijini na kusukuma ujenzi wa miundombinu vijijini ili kuwe na mazingira ya kuvutia uwekezaji.

Siri ya uteuzi wa Kinana yafichuka
Katika hatua nyingine, siri ya uteuzi wa Kinana kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), imejulikana. Habari kutoka ndani ya chama hicho, zilisema kuwa siri ya uteuzi wa nguli huyo wa siasa za CCM, imetokana na juhudi za Rais Benjamin Mkapa kumshawishi kushika nafasi hiyo ili kukinusuru chama.

Awali ilielezwa kuwa Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM taifa, alijaribu bila mafanikio kumtaka Kinana awe katibu mkuu. Hata hivyo ili kukubali majukumu hayo, Kinana aliweka masharti ambayo mwenyekiti alikubaliana nayo na kuahidi kuleta mabadiliko makubwa ndani ya CCM ambayo katika siku za hivi karibuni imepoteza mvuto.

sifa moja kubwa anayotajwa kuwa nayo Kinana ni msimamo mkali dhidi ya masuala ya ufisadi, na kubwa zaidi anatajwa kuwa bingwa wa mikakati ya kisiasa ndani ya chama hicho, jambo linalothibitishwa na kuteuliwa kwake kuongoza kampeni za wagombea urais katika mazingira ya ushindani mkali. Itakumbukwa kuwa Kinana ndiye aliyeongoza kampeni za Benjamin Mkapa mwaka 1995, dhidi ya Augustine Mrema, aliyekuwa mwanasiasa maarufu na aliyekubalika kwa wakati huo.

Tangu wakati huo, Kinana amekuwa akiongoza kampeni za urais. Ni mtu anayetajwa kusimamia mawazo anayoamini ni sahihi, lakini akiwa tayari kuunga mkono hoja zenye lengo la kukijenga chama.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechuliwa na Philip Mangula akirithi mikoba ya Pius Msekwa, mwanasiasa mkongwe na mzoefu akiwa na rekodi ya kuwahi kuwa katibu mtendaji mkuu wa kwanza wa CCM.
 

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,698
1,195
Ndio maana tunawaambia CCM inatawala nchi lakini Chadema inaongoza nchi.
 

KYALUMUKUNZA

Senior Member
Aug 19, 2012
145
0
kwa hili basi tuipongeze CMM kwa kuiga baadhi ya sera za chadema zenye manufaa kwa watanzania badala ya kuendeleza malumbano yasiyokuwa na tija kwa jamii ya kitanzania.
 

Mwanyasi

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
7,834
2,000
Ukweli wanaujua vizuri kuwa CDM inatoa mawazo yanayotekelezeka ya kuijenga nchi yetu, lakini wanaona aibu kisa upinzani (CDM) imesema! watanyoka tu hawa.............!
 

Genekai

R I P
Feb 9, 2010
12,537
2,000
Nchi hii bwana, jembe langu lilipoyasema haya tukaambiwa "mropokaji na mzushi". Sasa mbona wameyala maneno yake!!!!!
 

50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,237
2,000
Miongoni mwa matatizo yaliyomo CCM ni wivu, mbaya zaidi hawana wivu wa maendeleo ama fikra endelevu, badala yake wanawivu wa kuumiza yeyote mwenye fikra endelevu ambaye hajavaa shati la kijani na suruali nyeusi....!
 

lufungulo k

JF-Expert Member
Apr 19, 2012
2,115
2,000
ni ukomavu wa kuendesha nchi, na binafsi nawaomba CDM waendelee kukosoa na kubuni mikakati thabiti juu ya mustakabali wa taifa siyo kuimba ngonjera [ufisadi] kila kukicha. ccm ilipotea njia lkn sasa imerudia njia yake najua tabia ya CCM ni usikivu inapokosolewa majembe yaliochukua uongozi yanafahamu saaana tabia hii ya usikivu, unyenyekevu na uadilifu kila lililozuri liliko popote litamfikia mtanzania.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
1,500
Walisema Dr. Slaa ni mzandiki, sasa waseme Kinana naye ni mzandiki
 

Ngandema Bwila

JF-Expert Member
Sep 8, 2010
1,003
1,195
Shida CCM ni slow leraners inawachukuwa muda mrefu sana kuelewa mambo, wananza kwa kupinga na kudai haiweekani! Lipumba aliwambie wafute kodi ya mandeleo walipinga kwa muda wa miaka kadhaa, CDM walianza kutumia HELIKOPTA wakaponda sana baadaye tuanona sasa wantumia tena tatu.
 

Lukolo

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
5,146
1,250
Duh, tulidhani wangekopi suala la katiba peke yake, kumbe hata haya ya vifaa vya ujenzi na elimu wameamua kuyakopi? Inapendeza hata hivyo kwa kuwa ni kwa maslahi ya taifa. Ila isije ikafika mahali CHADEMA wakajikuta hawana sera tena mwaka 2015. Maana hadi sasa CCM imeiacha ilani yake ya uchaguzi imeanza kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CHADEMA. Mambo inayotaka kuyafanya sasa CCM yangekuwa yanafanywa na CHADEMA kama kingekuwa madarakani na kujipatia uungwaji mkono mkubwa. Anyway tunaamini CHADEMA ni jungu kuu lisilokaukiwa na mawazo mapya.
 

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,615
1,195
wapi zombie a.k.a zomba,ritz 1, rejao, cuf ngangari, na washabikia ufisadi wote... hii ni copy yenu.
 

Soki

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
1,306
1,195
Walisema Dr. Slaa ni mzandiki, sasa waseme Kinana naye ni mzandiki
Na bado!

Waige na miongozo mingine ya CHADEMA.

Wawashughulikie mafisadi kama wanaweza.

Wathubutu kuwapeleka mahakamani na kuhukumiwa ipasavyo kama wahujumu uchumi na KUWAFILISI na kuwavua uongozi au hata kuwafukuza katika Chama chao.

Its too late for them, the part is now in critical condition!
 

afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
1,250
Kazi ya vyama vya upinazani ni kutoa alternative solutions kwa matatizo yanayoikabili jamii. Chama tawala ni lazima kwa namna moja au nyingine kitathmini mapendekezo hayo na kuona kama yanfaa na pale inaporidhika sio kosa kuimplement. Bila shaka wakitekeleza yaliyo mengi toka upinzani ina ashiria udhaifu walionao hivyo ni jukumu la wapiga kura kukiondoa madarakani kwa kuthibitika kuwa pamoja na kutawala kimekosa uwezo wa kuwa na mikakati yake chenyewe kutatua matatizo ya nchi.
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
1,500
Kazi ya vyama vya upinazani ni kutoa alternative solutions kwa matatizo yanayoikabili jamii. Chama tawala ni lazima kwa namna moja au nyingine kitathmini mapendekezo hayo na kuona kama yanfaa na pale inaporidhika sio kosa kuimplement. Bila shaka wakitekeleza yaliyo mengi toka upinzani ina ashiria udhaifu walionao hivyo ni jukumu la wapiga kura kukiondoa madarakani kwa kuthibitika kuwa pamoja na kutawala kimekosa uwezo wa kuwa na mikakati yake chenyewe kutatua matatizo ya nchi.
Ni kweli, lakini ukumbuke Dr. Slaa aliposema kuwa vifaa vya ujenzi vishushwe bei wao wakasema haiwezekani, bali Dr. Slaa alikuwa anaropoka tu.............. sasa wamegundua inafaa. tunataka wawatumikie wananchi, either kwa mawazo ya chadema ama Dr. Slaa......................... la msingi ni kwamba ccm wakitaka kufanikiwa kuongoza tanzania mpaka 2015, wakaombe ushauri kwa chadema
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,194
2,000
Ni kweli, lakini ukumbuke Dr. Slaa aliposema kuwa vifaa vya ujenzi vishushwe bei wao wakasema haiwezekani, bali Dr. Slaa alikuwa anaropoka tu.............. sasa wamegundua inafaa. tunataka wawatumikie wananchi, either kwa mawazo ya chadema ama Dr. Slaa......................... la msingi ni kwamba ccm wakitaka kufanikiwa kuongoza tanzania mpaka 2015, wakaombe ushauri kwa chadema
Tayari kinana atakuwa na bifu na yule shangazi mlopokaji wa CCM aka mzee wa makarolite....maana alikuwa anashupalia kweli swala hili kuwa chadema tulisema vitu ambavyo haviwezekani sas leo ccm wanaona vinawezekana na vina faa...
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,981
1,500
Tayari kinana atakuwa na bifu na yule shangazi mlopokaji wa CCM aka mzee wa makarolite....maana alikuwa anashupalia kweli swala hili kuwa chadema tulisema vitu ambavyo haviwezekani sas leo ccm wanaona vinawezekana na vina faa...
Hahaaaa Mkuu kumbe ile ni carolite...................... ile kitu inababu mpaka akili, siyo ngozi peke yake
 
Top Bottom