Busara ni ipi tujadili kwanza muungano au katiba

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,793
12,238
Bunge letu limeishapitisha muswada wa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Ndugu wadau naomba tuangalie jambo hili kwa kifupi; kipi tulitakiwa kuanza nacho:
  1. Kujadili muundo wa muungano, au
  2. Kujadili katiba mpya?
Kama ikitokea kwamba tutaamua muungano usiwepo kwa kuzingatia kuwa hoja hii inatokana na ukweli kuwa wazanzibari hawaupendi muungano, maana yake tutakuwa tumepoteza muda na fedha zetu bure. Mwisho wa siku tutatakiwa kutengeneza katiba mpya ya Tanganyika na wenzetu wa Zanzibar watakuwa wametupiga bao kwa kuwa wao tayari wamekwisha andika katiba yao!

Narudisha hoja hii baada ya M.M. Mwanakijiji kuweka ufafanuzi mzuri kama ilivyoandikwa na Tanzania Daima leo tarehe 11/04/2012 kama ifuatavyo:

Kitu cha tatu ambacho mzee Mtei amekigusia kwa kupitia ni kuwa Zanzibar inaonekana hawataki Muungano.Sasa, kama tayari kuna mwamko wa kupinga Muungano na tumeona hata juzi Jussa akipigia debe sheria ya ubaguzi dhidi ya watu wa bara (ambao anawaita wageni) lakini mchakato umepangwa kana kwamba watu wote wanaheshimu Muungano huu? Kwanini kwa mfano, kabla ya kuanza kuandika Katiba Mpya ya "Muungano" watu wa Zanzibar wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka kubakia kwenye Muungano au la? Baadhi yetu tunaamini kuwa kabla ya kuandika Katiba Mpya ni vizuri suala la Muungano likaamuliwa peke yake kwanza.Kama Wazanzibar watasema wanataka kutoka kwenye Muungano basi watoke ili Bara waandike katiba yao mpya na hivyo kuwa na mahusiano ya nchi mbili ndugu. Kimsingi mzee Mtei amedodosa tu kwa mbali kuwa mchakato hauheshimu hisia za Wazanzibari wanaotaka Muungano uvunjwe kwa sababu "wanakandamizwa na kuonewa" na "mkoloni" Bara!

Naomba tujadili bila jazba kwa maslahi ya Tanzania/Tanganyika

Kati ya muungano na katiba kipi kinakiongoza kingine? Jibu la swali hili ndicho kinachotakiwa kuanza kujadiliwa.
Katiba ya nchi ni mwongozo ambao wananchi wenyewe kwa umoja wao wameuweka ili utumike katika kujitawala na kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hivyo ili kupata katiba ya nchi lazima nchi yenyewe ijulikane mipaka yake, watu wake, utamaduni wa watu wake, jiografia yake, historia yake nk.

Mambo hayo yakifahamika vizuri kwa wananchi ndipo wanaweza kupanga aina ya utawala na namna ya kuweka viongozi wao, pia wanaweza kuweka malengo yao ya maendeleo ili yaakisi utamaduni wao.

Tanzania hivi sasa tuko njia panda, hatujui kama wananchi bado wanahitaji kuendelea kuwa na muungano au la. Kama wanauhitaji ni muungano wa namna gani; serikali mbli kama sasa , serikali moja au serikali tatu.

Juzi juzi Maalim Self alipendekeza muungano uwe wa mkataba! Kazi kwetu kwa kuwa kama hatujui aina ya nchi tutakayo kuwa nayo basi wasiwasi wangu ni kwamba tutajikuta tunalazimika kuandika katiba nyingine mara baada ya kura za maoini!
 
Katiba ya nchi ni mwongozo ambao wananchi wenyewe kwa umoja wao wameuweka ili utumike katika kujitawala na kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Hivyo ili kupata katiba ya nchi lazima nchi yenyewe ijulikane mipaka yake, watu wake, utamaduni wa watu wake, jiografia yake, historia yake nk.
nini kitatambulisha hayo yaliyoko kwenye bold?
 
nini kitatambulisha hayo yaliyoko kwenye bold?

Mipaka ya Tanzania hivi sasa ni ile inayojumuisha Tanganyika na Zanzibar. Hivyo watu wake ni Watanganyika na Wazanzibari kwa pamoja. Hali kadhalika utamaduni, jiografia na historia ni budi uhusishe Tanganyika na Zanzibar.

Endapo muungano ukivunjika kwa mfano basi mipaka, utamaduni, jiografia na historia vyote vitabadilika na kila nchi kubaki na kuhifadhi vya kwake!
 
Tanganyika inafahamika kijiografia na kadhalika Zanzibar pia. Kwa hali ya sasa ambapo hizi mbili zinajitambua kama nchi moja, naamini tayari masuala ya mipaka, tamaduni, historia, n.k. yanajulikana.
Mjadala wa muungano unasumbuliwa na vitu vikubwa viwili: siasa na uoga. Ikumbukwe kuwa hapakufanyika kura ya maoni kuuliza kama watu wa nchi hizi mbili walitaka kuungana; hili jambo lilifanyika kihuni tu na sasa umefika wakati lifanyiwe uhakiki ili kuona kama bado lina tija.
Kwa hiyo kama hisia za watu ni kwamba muungano uendelee basi katiba ianze kujadiliwa lakini kama ni kinyume basi muungano ujadiliwe kwanza ili ijulikane katiba ikiundwa iwe vipi.
 
Kuna hoja kuwa kama wananchi wangetakiwa kutoa maoni yao kabla ya muungano, basi huenda muungano huu usingekuwapo!

Hivyo kwa busara za Nyerere na Karume waliamua kuunda muungano kwanza halafu kuwafahamisha wananchi baadaye kupitia Bunge kwa Tanganyika na Baraza la mapinduzi kwa Zanzibar.
 
Katiba ndiyo muongozo wa yote, mengine yataelekezwa humo namna ya kufanyika!
 
Narudisha hoja hii baada ya M.M. Mwanakijiji kuweka ufafanuzi mzuri kama ilivyoandikwa na Tanzania Daima leo tarehe 11/04/2012 kama ifuatavyo:

Kitu cha tatu ambacho mzee Mtei amekigusia kwa kupitia ni kuwa Zanzibar inaonekana hawataki Muungano.Sasa, kama tayari kuna mwamko wa kupinga Muungano na tumeona hata juzi Jussa akipigia debe sheria ya ubaguzi dhidi ya watu wa bara (ambao anawaita wageni) lakini mchakato umepangwa kana kwamba watu wote wanaheshimu Muungano huu? Kwanini kwa mfano, kabla ya kuanza kuandika Katiba Mpya ya “Muungano” watu wa Zanzibar wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka kubakia kwenye Muungano au la? Baadhi yetu tunaamini kuwa kabla ya kuandika Katiba Mpya ni vizuri suala la Muungano likaamuliwa peke yake kwanza.Kama Wazanzibar watasema wanataka kutoka kwenye Muungano basi watoke ili Bara waandike katiba yao mpya na hivyo kuwa na mahusiano ya nchi mbili ndugu. Kimsingi mzee Mtei amedodosa tu kwa mbali kuwa mchakato hauheshimu hisia za Wazanzibari wanaotaka Muungano uvunjwe kwa sababu “wanakandamizwa na kuonewa” na “mkoloni” Bara!

Naomba tujadili bila jazba kwa maslahi ya Tanzania/Tanganyika
 
Wala usihangaike...sisi tupo ki kazi zaidi, tunajadili katiba kwanza...muungano utaainishwa ndani ya katiba: kawa utakuwepo basi muundo wake utakuwa humo ndani. kama tutauvunja ni uamuzi wetu pia ....... cha maana ni kuunda majimbo tu ili kupungua kero za centralized plans!!!!
 
Katiba ndiyo muongozo wa yote, mengine yataelekezwa humo namna ya kufanyika!

Wala usihangaike...sisi
tupo ki kazi zaidi,
tunajadili katiba
kwanza...muungano
utaainishwa ndani ya
katiba: kawa utakuwepo basi
muundo wake
utakuwa humo ndani.
kama tutauvunja ni
uamuzi wetu pia .......
cha maana ni kuunda majimbo tu ili
kupungua kero za
centralized plans!!!! Muna hofu kuvunjika Muungano eeeeh!
 
Teh teh teh! Kuna tetesi ya kuwa Muungano ulikua ni wa muda flani( miaka 10) tangu kuunganishwa, na baada ya hapo, Nyerere na Karume wakae kitako, ikiwa wameona unawafaa basi waziunganishe moja kwa moja.
Karume alisema Muungano kama koti, likikutia joto unalivua, na muungano mwisho Chumbe, kauli hizi zilimkasirishe BABA WA TANGANYIKA. Hatimaye Baba wa Visiwani akafariki katika kifo cha utata, may be Nyerere alishiriki indirectly. Sasa huo mkataba wa muungano hakuna alienao, huu ni ujinga wa wanasheria wa pande zote 2. Mkataba huo umeisha zamani, saivi tunaishi kiubishi tu lakini ukweli muungano mkataba umeisha! Sasa mi nashangaa sana watu wanajadili kitu ambacho hakipo as if kipo! :D
Mi nawashauri watanganyika waunde katiba yao mana hapa tulipo tushakupigeni bao zamani!
 
Mmetupiga bao kifikra lakini kiuhalisia bado tumeshika hatamu!
 
kero za muungano zilianza tangu karne iliyopita hadi leo hazijaisha. Mungu yupo hivi mizigo tunayobeba ya kuwahudumia wazenji tutafaidika na nini? mimi binafsi nafikiri tutakubaliane tuwe na serkali tatu ndipo tuandae katiba kwasababu kuna kasoro nyingi sana . hivi jamani sisi bara tunaumisi kiasi gani hadi tunadiriki kuwaondoa viongozi huko zenji ambao wanapingana nao mfano 1984 alifurushwa tu kwasababu ya kuchafua hali hewa ya siasa zanzibar. bora tuvunje muungano ndipo tuewweke utaratibu mpya
 
Bunge letu limeishapitisha muswada wa mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.

Ndugu wadau naomba tuangalie jambo hili kwa kifupi; kipi tulitakiwa kuanza nacho:
  1. Kujadili muundo wa muungano, au
  2. Kujadili katiba mpya?
Kama ikitokea kwamba tutaamua muungano usiwepo kwa kuzingatia kuwa hoja hii inatokana na ukweli kuwa wazanzibari hawaupendi muungano, maana yake tutakuwa tumepoteza muda na fedha zetu bure. Mwisho wa siku tutatakiwa kutengeneza katiba mpya ya Tanganyika na wenzetu wa Zanzibar watakuwa wametupiga bao kwa kuwa wao tayari wamekwisha andika katiba yao!

Narudisha hoja hii baada ya M.M. Mwanakijiji kuweka ufafanuzi mzuri kama ilivyoandikwa na Tanzania Daima leo tarehe 11/04/2012 kama ifuatavyo:

Kitu cha tatu ambacho mzee Mtei amekigusia kwa kupitia ni kuwa Zanzibar inaonekana hawataki Muungano.Sasa, kama tayari kuna mwamko wa kupinga Muungano na tumeona hata juzi Jussa akipigia debe sheria ya ubaguzi dhidi ya watu wa bara (ambao anawaita wageni) lakini mchakato umepangwa kana kwamba watu wote wanaheshimu Muungano huu? Kwanini kwa mfano, kabla ya kuanza kuandika Katiba Mpya ya "Muungano" watu wa Zanzibar wapewe nafasi ya kuamua kama wanataka kubakia kwenye Muungano au la? Baadhi yetu tunaamini kuwa kabla ya kuandika Katiba Mpya ni vizuri suala la Muungano likaamuliwa peke yake kwanza.Kama Wazanzibar watasema wanataka kutoka kwenye Muungano basi watoke ili Bara waandike katiba yao mpya na hivyo kuwa na mahusiano ya nchi mbili ndugu. Kimsingi mzee Mtei amedodosa tu kwa mbali kuwa mchakato hauheshimu hisia za Wazanzibari wanaotaka Muungano uvunjwe kwa sababu "wanakandamizwa na kuonewa" na "mkoloni" Bara!

Naomba tujadili bila jazba kwa maslahi ya Tanzania/Tanganyika

Mimi Mtanganyika kwa kuzaliwa sikushirikishwa kwenye kuunda huo Muungano. Pia mambo yanayoendelea ya sintofahamu juu ya taratibu za uendeshaji wa serikali ya Tanzania kiuchumi na kisiasa kwa kisingizio cha Muungano kinanifu na kunikera hata kunikatisha tamaa. Kwa bahati mbaya ni agenda ya CCM bila kujali maslahi ya baadhi yetu ambao naamini tupo wengi.
 
Hili halina ubishi, ni sula ambalo lilitakiwa kujadiliwa kwa kina sana kabla ya kuandikwa kwa KATIBA mpya.Kusma ukweli mimi binafsi huo Muungano naona ni kama mzigo tu kwa Tanganyika kutokana na ukweli kwamba mambo mengi tunawasaidia na kuwapendelea ili waendelee kuupenda Muungano.Kuna miaka flani tulikuwa tukienda Zanzibar na passpot wakati wao walikuwa wanakuja free tu huku bila kuulizwa hiyo yote ikiwa ni kuwa favour.Mi nadhani katika mchakato mzima wa kutoa maoni ni bora tukawaeleza wazi kuwa kama muundo wa Muungano utaendelea kuwa hivyo, basi sisi hatuutaki,vilevile wakiwa flxible tutoe maoni yetu juu ya aina ya Muungano tunaoutaka.
 
Ilitakiwa kwanza wananchi raia wanaotoka Zanzibar na wale wanaotoka Bara waulizwe kwanza kama wanautaka Muungano. Pande zote mbili zikikubali basi ndio uanze mjadala wa aina gani wa Muungano unaotakiwa na uwakilishi wa pande zote mbili katika serikali, bunge na mahakama za Muungano huo. Wakati wote wa majadiliano hayo, kila pande ipewe haki ya kujitoa kama haikubaliani na kitakachoamuliwa. Kama upande mmoja wa Muungano utakataa Muungano hu basi tuachane na kila mmoja aende kivyake vyake. Tuige kwa Czechoslovakia na si kwa Yugoslavia, Sudan, Ethiopia na nchi nyingine nyingi zilizotaka kulazimisha kitu kisichotakiwa na wananchi wake.

Amandla......
 
Sasa huu waraka wa CCM ndiyo utakaoiua Tanzania endapo Rais wa Muungano atatoka katika chama tofauti na Rais wa Zanzibar!
 
Back
Top Bottom