Busara kwa Machinga Mwanza haikutumia wakati wa Bomoabomoa DSM

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,772
102,128
20151118030950.jpg
indexdd.jpe

Bomoa Bomoa iliyofanyika Kindondoni. Ilidaiwa kuwa ilifanywa kwa mujibu wa Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995

Rais ameonekana kupongezwa kwa kutumia busara kuwarudishwa wamachinga walitimuliwa katikati ya mji wa Mwanza na kuwarudisha wachimbaji wadogowadogo mkoani Shinyanga. Rais alisikika akitoa amri hiyo kwamba hata kama ni sharia lazima wapiga kura wake walindwe wasibughudhiwe

Ikumbukwe kuwa wakati wa bomoa bomoa Dar es Salaam tulipiga kelele kuwa huu ni unyama tukimuomba rais aamuru utu uzingatiwe. Ikatamkwa kuwa hiyo ni kwa mujibu wa Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995.
Je, busara hizi zina msimu na maeneo spesheli? Je wamachinga waliondolewa Dar na Mbeya wao sio masikini? Wao rais wao ni yupi?
 
Bomoa bomoa ya Kinondoni ilikuwa ni kuwakomesha wananchi kwa kuchagua UKAWA , ule ulikuwa ni unyama na uhalifu dhidi ya binadamu.

Kuhusu machinga , pamoja na kwamba tamko lilihusu Mwanza lakini Tayari Kariakoo madereva wote wamekwama baada ya machinga kurudi kwa kishindo na kuanza tena kusonga ugali katikati ya barabara ya msimbazi .
 
hao sio wa nyumbani kwetu....ngoja waisome namba

mlitunyanyasa muda mrefu sana...
mkituita kabila kubwa la watu wajinga wasio na elimu....sasa tumepata mtetezi...anatulinda

hiyo ni kauli ya kina ngosha ....
 
Kuna Kipindi magu inabidi awe anapiga tu kimya sio lazima kila cku tantala ntantalila.
 
Tanzania inapita katika awamu ambayo tokea tupate Uhuru haijawahi kutokea.. mpaka haijulikani tunakwenda wapi.. Hivi vibanda vya maboksi vya barabarani vimtie hasira bwana yule kuongea hadi macho yanataka kutokea kwenye vioo vya miwani..hakupatwa na uchungu wala kuongea kwa jazba wakati makaazi ya wanyonge yakibomolewa zaidi alitoa kejeli tu.. kwa uongozi huu tumeingia cha kike ndugu wananchi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom