Busara kubwa kutoka Kwa mkuu wa Majeshi

Juzi nilienda land force kibaha kumtembelea best yangu ambae aliwahi nisaidia sana kipindi nipo chuo,harassment niliopewa na hawa jamaa sitosahau nimenyoosha maelezo nikawapa picha na number ya simu ya MTU nnae mfuata cha ajabu nikawa nabadilishiwa maswali huku wakinikandamiza kuwa mi ni mamluki.
Usipende ushikaji na wajeshi hata kama ni prestige kuwa nae acha
 
Bora hapo wamekuheshimu sana nenda airforce unaweza uliwa kabisa , na sio vizuri raia tu ghafla bin vuu kutimba maeneo Kama hayo siovizuri sana
Juzi nilienda land force kibaha kumtembelea best yangu ambae aliwahi nisaidia sana kipindi nipo chuo,harassment niliopewa na hawa jamaa sitosahau nimenyoosha maelezo nikawapa picha na number ya simu ya MTU nnae mfuata cha ajabu nikawa nabadilishiwa maswali huku wakinikandamiza kuwa mi ni mamluki.
! Hakiyamungu.
 
MKUU WA MAJESHI MMOJA ALIWAHI KUNIAMBIA MAMBO MAWILI AMBAYO HUWAAMBIA WAFANYAKAZI WENZAKE, MAMBO HAYA, YALINIKAA SANA NA NIKAYAELEWA

Alisema ....

1.
Kila siku kabla ya kulala, andaa sare yako na itundike
Karibu na kitanda chako,

Unapopanda kitandani, iangalie sare yako na kisha jiulize.... kitatokea nini nisipovaa sare hii na nikajaribu kuingia kwenye maeneo ya jeshi?

Jibu lake ni, hakuna saluti yeyote itakuja njia yako! Kwanza utasimamishwa getini na kuulizwa maswali!

Na ikitokea mwingine amevaa sare hii hii na akapita pembeni ya mlinzi wa jeshi, hakika atapewa saluti.

Hivyo basi, saluti haikuwa ya kwako bali ni ya sare iliyotundikwa ukutani ambayo imekutengeneza lakini kumbuka, sare hiyo haitakuwa ya kwako milele! Siku moja itaenda kwa mwingine....

Kwahiyo, jiandae kwa hilo tafadhali!

2.
Kila siku ukimaliza kazi zako, hakikisha kila mtu ametoka ofisini kwako.

Nyanyuka kwenye kiti chako, tembea elekea upande ule mwingine, kaa kwenye kiti, na kisha kitazame kiti chako.

Huenda kwa nafasi yako umepitisha mambo mengi sana leo ukiamini ni ya muhimu sana...

Lakini ukae ukijua, kesho kutakuwa kuna mwingine kwenye kiti hicho, na anaweza akayageuza mambo yote ambayo unadhani ni ya muhimu leo!

Mambo uliyoyapitisha, ukiamini wewe ni mtu muhimu... ilikuwa ni kiti ndo kinayapitisha na si wewe. Kiti hichi kipo kwa mda tu! Hakitakuwa cha kwako milele. Kiti hicho kimekupa mamlaka kwa mda ambapo mamlaka hayo yataondoka pale tu utakapo kiachia kiti hicho.

Tumia mamlaka hayo katika misingi ya haki

Tumia mda huo kuandika jina lako kwa DHAHABU

Tumia mamlaka hayo kuyafuta machozi ya watu wenye mazingira magumu waliopo katika jamii yetu

Tumia mamlaka hayo kujenga taifa na si kuwa na kiburi au kushehenisha ukuu wako.

Naomba nikuulize

Unatimia sare yako na kiti chako kufanya nini leo?

- Je unavitumia kuwakandamiza watu na kuwaonyesha kuwa wewe ndo mwenye mamlaka?

- Unavitumia kuwasaidia washkaji na marafiki tu kwasababu wanakusifu hata pale ambapo hawastahili?

- unavitumia kugawa na kutawala na kujenga uadui?

- Unavitumiaje?

- Kumbuka, mtu ambaye unamkandamiza au kumkosea kupitia sare yako au kiti chako huenda akawa msimamizi wa mtoto wako, mjukuu wako, mjomba wako, mdogo wako au hata rafiki yako.

- Je utajisikiaje kama yote uliyomfanyia, yakarudiwa kwa ndugu yako?

- Fikirini, ndugu zangu, fikirini. Kwani hakuna aijuae kesho.

- Tumia sare yako au kiti chako kuwaendeleza na kuwasaidia wote.

- kuwa mama, baba, dada, na rafiki kwa wote.

Uwe jaji mwaminifu. Sikiliza pande zote mbili za simulizi.

Muogope Muumba wako.

- Usimchukie mtu, wapende wote. Hakuna aijuae kesho.Muwe na jioni njema
Mule mule kudadadeki mwanangu.

Nime'like' sana thread yako hii iliyojaa mafunzo na hamasa za utu.
 
Juzi nilienda land force kibaha kumtembelea best yangu ambae aliwahi nisaidia sana kipindi nipo chuo,harassment niliopewa na hawa jamaa sitosahau nimenyoosha maelezo nikawapa picha na number ya simu ya MTU nnae mfuata cha ajabu nikawa nabadilishiwa maswali huku wakinikandamiza kuwa mi ni mamluki.
Kwani ulishindwa kusubiri uonane nae nje ya muda wa kazi ?Au ulitaka kutosha kwa demu wako? Bora wamekunyonya kidogo rudi tena siku nyingine uone.
 
Hayo hufanyika kwa majeshi ya third world countries tu.
Kwa kawaida Jeshi Ni Mali ya wananchi.
Duh inashangaza kwa kweli...
Kwa hiyo kama ni mali ya wananchi ndiyo iwe free pass.
Hebu jaribu kwenda huko mkuu first worlds countries kama area 51 au kambi yoyote ya jeshi waambie nimekuja kuwasalimia tu uone kama hauta enda kupimwa akili kama zina charge.
 
Hiyo first world country anayoona majeshi ni wananchi kuingia makambini kiholela kisa ni mali ya wananchi ni ipi? Atueleze alienda kambi gani huko bila kuhojiwa!
 
  • Thanks
Reactions: 7ve
Juzi nilienda land force kibaha kumtembelea best yangu ambae aliwahi nisaidia sana kipindi nipo chuo,harassment niliopewa na hawa jamaa sitosahau nimenyoosha maelezo nikawapa picha na number ya simu ya MTU nnae mfuata cha ajabu nikawa nabadilishiwa maswali huku wakinikandamiza kuwa mi ni mamluki.
Ulitakiwa umpigie simu mtu wako aje muongozane
 
Wenye sifa hizo huwa hawadumu hapa Duniani tambua hilo.
Na wenye Roho za Upendo, Utu, Huruma na kutopenda Dharau, Uonevu kwa Watu, Uwongo na Unafiki kama GENTAMYCINE si tu huwa tunachukiwa bali huwa hata tunaishia Kurogwa au kutaka Kuuliwa huku 24/7 tukizushiwa kila baya ili mradi tu tuchafuke na tuonekane hatuna la maana.

Ila Kitu kizuri ni kwamba tunapatwa na kila aina ya Jaribu kutoka kwa Wanadamu wenye Husuda nasi ( na ambao pengine hata hakuna baya tulilowafanyia na wengine huenda Mafanikio yao ya leo yametokana na Juhudi zetu Kuwapigania ) lakini Mwenyezi Mungu anatulinda na kutuepusha na kila Mitego wanayotutega.
 
Gentamycine bhana nimecheka sana unavyojipa promo
 
Back
Top Bottom