Busara isipotumika mgomo wa madaktari utasambaa kwa wafanyakazi wote na wananchi wataingia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Busara isipotumika mgomo wa madaktari utasambaa kwa wafanyakazi wote na wananchi wataingia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Mar 9, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Mambo yanavyozidi kuvurugika, na serikali inavyoonyesha udhaifu na kutokuliona tatizo kwa undani. Maamuzi ya kibabe na kukurupuka yanayotolewa na waandamizi wa serikali sasa mahakama, hayataleta suluhu kwenye mgogoro huu zaidi ya kuusambaza kwa kada nyingine na hatimaye wananchi.

  Serikali ijui imetumia muda mwingi sana kusomesha wasomi mbali mbali. Tanzania inahitaji sana wataalamu, madaktari, manesi, waalimu hawatoshi na uzalishaji wake ni aghali sana.

  Muda umefika wa serikali kutumia busara na kujua inapamabana na wataalamu wenye ujuzi na akili timamu. Serikali ijue nchi imebadilika na wengi wanajua haki zao. Serikali ijui muda wa ahadi za uongo na kuzima moto umefika mwisho.

  Sasa ni wakati wa Serikali kuachana na viongozi wazembe na wasiojua wafanyacho. Mgomo wa madaktari ni uzembe wa viongozi wa wizara wa afya wakiwa chini ya waziri wa afya na waandamizi wake, lugha chafu, ukatili na kudhalilisha taalamu ya utabibu.

  Mizengo Pinda anahusika kwa kutokufanya homework yake vizuri, kutoa kauli tata na suluhu ya kila siku, wapumbaze watasahau tutasonga mbele, ameshindwa kusoma nyakati na akili za anao watawala. Katumia muda mwingi sana kuspin maneno yake mwenyewe. Kila nikisikiliza record ya maneno ya Pinda pale CPL na anachosema leo naona mzaha mkubwa sana wa utatuzi wa hili janga.

  Serikali ingeweza kutatua mgomo huu na kuuzuia usitokee kama watawala wangejua kuwa Tanzania imebadilika, huwezi kuwaburuza tena.

  Nani mwenye busara asaidie hili ndani ya serikali ya JK??? Vitisho havileti suluhu hata siku moja. Kila aliyetishwa Duniani alidikiriki kufa.

  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Tunakupa Elimu ujikomboe sio utawaliwe............sasa najikomboa
   
Loading...