Uchaguzi 2020 Busara, hekima na kuvumiliana vinahitajika kwenye suala la ushirikiano wa CHADEMA na ACT-Wazalendo

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,129
18,743
Kuna mambo fulani yanaweza kuwa yanakiukwa katika suala zima la ushirikiano wa Chadema na Act wazalendo kuhusu kumuunga mkono Tundu LIssu wenye kugombea uraisi.

Lakini kila mtu, pamoja na CCM wenyewe, anajua kwamba NEC wamekuwa wakifumbia macho ukiukwaji tatibu za uchaguzi katika mambo mengi sana Magufuli kama Mgombea Uraisi wa CCM amekuwa akifanya. Kwa mfano katika ziara nyingi za kampeni Magufuli amekuwa akitoa ahadi za misaada akidai yeye ni raisi, jambo ambalo NEC wanajua sio sahihi, kwa kuwa Magufuli amefanya hivyo akiwa katika misafara ya kampeni sio ziara za kiserikali. In fact hiyo ni rushwa Magufuli amekuwa akitoa.

Sasa basi, ushauri wangu kwa NEC ni kwamba, kwa hili la Chadema na ACT Wazalendo ni bora tu wakae kimya kama walivyokaa kimya kama walivyokaa kimya kwenye ahadi za misaada za Magufuli wakati wa misafara ya kampeni. NEC wakijifanya vijogoo ili kumfurahisha Magufuli na CCM yake katika hili wanaweza kuleta vurugu ambayo haijawahi kutokea hapa nchini. Kwa hiyo it is not worth it kuanza kuwaandikia barua Chadema au ACT Wazalendo. Acheni tu, siku zimebaki kidogo sana.

Kwa kiswahili cha mitaani tunasema NEC kausheni kama vile hamjaona kama mlivyofanya kwa Magufuli!
 
Nafikiri Membe ataunga mkono juhudi za Lissu tu hata kama ni mwishoni.
 
Hata huko Zanzibar ACT wasiende kupiga kura tarehe 27 cause wakienda watakamatwa kwa muda watafanya hiyo tarehe 28 washindwe kupiga kura wao wapambane na wanasheria wao na idadi ya kura ya tarehe 27 ijulikane mapema.
 
Udhalimu haukuwahi kushinda.
 
Hata huko Zanzibar ACT wasiende kupiga kura tarehe 27 cause wakienda watakamatwa kwa muda watafanya hiyo tarehe 28 washindwe kupiga kura wao wapambane na wanasheria wao na idadi ya kura ya tarehe 27 ijulikane mapema.

Nadhani ZEC waachane na kura ya tarehe 27.

wanaotakiwa kupiga kura tarehe 27, watalazimika kupiga kura nyingine tarehe 28.

..kwa maoni yangu ni busara wote wapige kura siku moja, tarehe 28.
 
Ni kosa gani ambalo Raisi Magufuli amefanya kusema yeye ni Raisi? Hivi unaijua hata Katiba ya JMTZ kwanza? Unajua kwamba Raisi Magufuli ana uwezo wa Kikatiba hata sasa hivi wa kusitisha au kuahirisha uchaguzi wenyewe akiwa kama Raisi wa JMTZ?
 
Back
Top Bottom