Bus la UDA limedondoka

Dannycage

Senior Member
Oct 25, 2010
104
36
Habari za usiku ndugu, bus la kampuni la UDA limedondokea mtaroni usiku huu maeneo ya tabata shule jirani na green light hotel, lilikuwa likitokea tabata na nahisi (sina uhakika) lilikuwa linaenda sheli kama kawaida yao kujaza tena abiria. Sina habari zaidi kwani nilikuwa mpita njia nawahi kwetu. Usiku mwema kwenu wote.
 
Madereva wa UDA wanakua overworked mno. Hapo ujue dereva alikabithiwa gari jana saa kumi alfajiri. hajapumzika na utakuta muda huu wa ajali alikua hajala na hesabu haijatimia. CHEZEA TAJIRI MBONGO WEWE. WANAKUKAMUA MPAKA UTOKE DAMU. PALE UDA HUFUKUZWI KAZI ILA UKIDUMU NAO MIEZI MITATU WEWE KIDUME. WEENGI MADEREVA WAMEACHA KAZI.
 
Wacha yadondoke ikiwezekana yayeyuke kabisa.Madereva na makonda wana lugha chafu balaa.Gari zimekaa kichangudoa.Hazijulikani zinaenda wapi, zinatoka wapi wala nauli yake ni ipi.Anae bisha na aje Kibanda cha mkaa Mbezi aone uchafu huu.Narudia tena, na yaanguke tuu hata chuma chakavu kisipatikane.Wapi vipanya vyetu????
 
:smile-big:huna habari hata za majeruhi ama halikuwa na watu?
Kuna uzi humu ndani kuhusu ajali hii.Hakuna majeruhi hata mmoja.Hii ni habari njema.Chanzo cha ajali ni dereva kutaka kusimamisha basi sehemu isiyo na kituo kupakia abiria mmoja.
 
Kuna uzi humu ndani kuhusu ajali hii.Hakuna majeruhi hata mmoja.Hii ni habari njema.Chanzo cha ajali ni dereva kutaka kusimamisha basi sehemu isiyo na kituo kupakia abiria mmoja.

Bora imekuwa hivyo maana ajali kwasasa ni janga kubwa
 
Hayo magari yako rafu sana siku hizi....kwanza ustaarabu hakuna kuanzia dereva mpk konda...bora uda ya enzi hizo
 
hili hapa...

IMG_5467.jpg
 
kuna mwingine nae kataka kushindana na mwenzie kuangusha lingine cheki hapo...

IMG_4513.JPG
 
Hatuombei ajali ila kwa hili linaweza kuwa chachu ya wenye mamlaka (kama wapo) kuhoji maadhi ya mapungufu ya kampuni hiyo onayoaibosha mamlaka zilizowekwa kwa kutokuwa na mstari wa kuonesha routes na upendeleao ambao upo sasa kwa UDA pekee kufika Ferry!
 
Back
Top Bottom