Bus la Abood la kwenda Mbeya lapata ajali

Teacher1

JF-Expert Member
Jan 29, 2011
333
149
Mida hii basi la Abood liendalo Mbeya limepata ajali mbaya katika eneo la Makambako mkoani Iringa. Basi hilo likiwa katika mwendo kasi limegonga kundi la ng'ombe waliokuwa wakivuka barabara nje kidogo ya mji wa Makambako ukielekea mbeya. Ng'ombe wengi wamekufa na wengine kujeruhiwa lakini cha kumshukuru Mungu ni kuwa watu wamenusulika.
 
Kwani wiki ya NENDA KWA USALAMA si inaishia leo???

Eee Mola tuepushie hiki kikombe!!
 
Mida hii basi la Abood liendalo Mbeya limepata ajali mbaya katika eneo la Makambako mkoani Iringa. Basi hilo likiwa katika mwendo kasi limegonga kundi la ng'ombe waliokuwa wakivuka barabara nje kidogo ya mji wa Makambako ukielekea mbeya. Ng'ombe wengi wamekufa na wengine kujeruhiwa lakini cha kumshukuru Mungu ni kuwa watu wamenusulika.

Mkuu mbona habari hii tangu jana cjaickia mahali pengine popote ikiripotiwa?
 
Labda Kwasababu hamna kifo chochote, basi halijapinduka wala kugongana na gari lingine...yani ni kama sio issue vile japo muanzishaji kaandika ajali mbaya.
 
Mida hii basi la Abood liendalo Mbeya limepata ajali mbaya katika eneo la Makambako mkoani Iringa. Basi hilo likiwa katika mwendo kasi limegonga kundi la ng'ombe waliokuwa wakivuka barabara nje kidogo ya mji wa Makambako ukielekea mbeya. Ng'ombe wengi wamekufa na wengine kujeruhiwa lakini cha kumshukuru Mungu ni kuwa watu wamenusulika.
Ni kweli mwendo kasi si mzuri lakini tujiulize hao wafugaji nao wanaopenda kuchungia kandokando ya barabara nao wana makosa sana. Nakuthibitishia ukiwa dereva unaweza kugonga mnyama bila kutarajia, sasa hebu jiulize kama dereva ameangalia mbele hakuna kitu barabara imenyooka unataka afenye nini zaidi ya kufidia muda kidogo halafu ghafla linatokea kundi la ng'ombe wanavuka barabara utafanyaje? Nashukuru Mungu hakuna mtu aliyekufa,
 
acha kufia muda ina gharama kubwa san
 
acha kufidia muda ina gharama kubwa sana
Mbeya - Arusha ni ~ 990kms imagine dereva anakwenda 80km/hr mfafika saa ngapi? Ukweli, mbona wenzetu wana barabara nzuri na wanakimbia sana lakini hawapati ajali kama hizi. Ukweli sisi watanzania tumezoea sana kuchungia mifugo yetu kando kando ya barabarani hususani ng'ombe na punda.
 
hakuna basi ya abood inayotoka arusha to mbeya.
 
Back
Top Bottom