Teacher1
JF-Expert Member
- Jan 29, 2011
- 333
- 149
Mida hii basi la Abood liendalo Mbeya limepata ajali mbaya katika eneo la Makambako mkoani Iringa. Basi hilo likiwa katika mwendo kasi limegonga kundi la ng'ombe waliokuwa wakivuka barabara nje kidogo ya mji wa Makambako ukielekea mbeya. Ng'ombe wengi wamekufa na wengine kujeruhiwa lakini cha kumshukuru Mungu ni kuwa watu wamenusulika.