Burundi vs Tanzania wapi wabaki wa demokrasia??

mgombea uvccm2017

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
505
376
Niseme ukweli wa wazi nasikitishwa sana na kinachofanywa na chama changu juu ya uchaguzi wa Zanzibar
Ukiona mpaka watu wenye heshima kama Karume wameongea ujue imevuka kipimo
Ivi tunaweza jipambanua vip kutoka kwa matendo kama yale ya Burundi?
Hata ningekuwa mimi Nkurunzinza ningegoma kupokea vikosi vya usalama kwa sababu hao wanaotaka kuleta vikosi wenyewe wanafiki vile vile na hawako tayali kuachia madaraka.
Iv chama changu kinadhani CUF ikiongoza Zanzibar basi maana ya mapinduzi itakuwa imekufa??

Naamin rais wangu Magufuli hakubaliani na huu ujinga sema tu hajapewa rungu na mnafiki Mkwere ndo maana anashindwa kuchukua maamuzi magumu.

CCM hatuko tayali kuachia madaraka hata tushindwe tena! Najua cha changu kimejipanga kupeleka wabara kupiga kura na najua hata mimi nitafatwa kuombwa kupelekwa Zanzibar uchaguzi ukirudiwa

CUF gomeni kwa sababu hakuna mantiki ya kurudia uchaguzi na mkikosea mkakubali kurudia nawaapia hamtashinda kwa sababu tutakuja kupiga kura huko

Nkurunzinza wakikwambia walete vikosi waambie wavipeleke kwanza Zanzibar
 
Back
Top Bottom