Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,000
- 9,862
Burundi yatangaza siku saba za kuomboleza kifo cha Rais Nkurunziza
Serikali ya Burundi imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku 7 kufuatia kifo cha rais wake Pierre Nkurunziza, aliyeaga dunia Jumatatu akiwa na umri wa miaka 55 kutokana na mshituko wa moyo.
Tangazo la serikali kwenye Redio na Televisheni ya taifa lililosomwa na msemaji wake Prosper Ntahorwamiye ambaye pia ni Katibu mkuu wa serikali lilisema Nkurunziza alifariki dunia kutokana na mshituko wa moyo katika hospitali ya mkoani Karuzi.
Kulingana na katiba ya Burundi spika wa Bunge Pascal Nyabenda ndiye atakayeshika hatamu za uongozi kwa kipindi cha miezi miwili hadi atakapotawazwa Evariste Ndayishimiye aliyeibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa rais wa Mei 20 mwaka huu.
Hata hivyo taarifa nyingine zinasema muhula wa bunge ulimalizika tangu April 27 ilipozinduliwa kampeni ya uchaguzi hivyo ni makamu wa rais atakayeshika hatamu.
Nkurunziza aliiongoza Burundi kwa kipindi cha miaka 15.
DW
Pia Soma: News Alert: - Serikali ya Burundi yatangaza kifo cha Rais Pierre Nkurunziza