Burundi: Agathon Rwasa, kiongozi wa chama pinzani adai serikali inapanga njama ya kumuua

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Ikiwa ni miezi takribani mitano imesalia kabla ya nchi ya Burundi kufanya uchaguzi wake mkuu, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha CNL, Agathon Rwasa amelalamikia kuhusu kile alichosema ni njama za Serikali kutaka kukifuta chama chake.

RWASA_0.JPG

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Burundi cha CNL, Agathon Rwasa.
Mbabe huyo wa zamani wa kivita amesema anazo taarifa kuwa idara za usalama nchini Burundi zinapanga kumzushia uasi kama njia ya kumuua au kumtia mbaroni.

Matamshi yake anayatoa wakati huu wafuasi wa chama hicho wakiripotiwa kushambuliwa, kuuawa na hata ofisi zao kuchomwa moto na watu wasiofahamika.

Taarifa hii imethibitshwa na katibu mkuu wa chama cha CNL, Simon Bizimungu.

“Tunazo taarifa za kweli zinazosema kuwa kuna mpango unaondaliwa katika ngazi ya kitaifa kuhusu kuuawa kwa viongozi wa chama cha CNL na kuwazuia jela baadhi yao. Mpango unawalenga viongozi wa juu wa chama, ikiwa ni pamoja na Agathon Rwansa. Mpango huo unaadaliwa na chama tawala CNDD-FDD na viongozi mbalimbali katika jeshi na polisi”, amesema Simon Bizimungu.

“Mpango huo unalenga kuwapa watu silaha na sare za chama cha CNL, ili waonekane kuwa ni wapiganaji wa chama cha CNL. Mwendesha mashitaka papo hapo atachukuwa hatua ya kukamata viongozi mbalimbali wa chama na kufuta chama cha CNL, huo ndio mpango unaoandaliwa, “ ameongeza Agathon Rwasa.

Hata hivyo Rwasa amesema hana nia yoyote ya kuingia msituni au kutoroka nchi yake.



Chanzo: RFI Kiswahili
 
Back
Top Bottom