Kwa wakaazi wa dar es salaam, waliowahi kuvuka kwenda kigamboni kwa kutumia kivuko cha MV Magogoni watakuwa wanamfaham vyema huyu dogo; Ni Kijana aliyeamua kujitaftia ridhiki yake ya kila Siku kwa kuwapa burudani Abiria ndani ya kivuko kwa nyimbo mbalimbali hususani za msanii Diamond platnumz, hatumii kifaa chochote zaidi ya yeye mwenyewe, huimba na kucheza free style mbalimbali mithili ya diamond mwenyewe Ambazo huvunja mbavu watu kwa kucheka, kwakweli kwa wale waoga wa kuvuka maji kwa hofu ya kuzama, Kijana huyu anapoanza kuimba watu wote hutulia na kumsikiliza na hofu ya kuzama hupotea,Nashauri kwa wale mnaosaka vipaji ingekuwa vyema baraza la mziki, bongo star search ,wazamini na wawekezaji mbalimbali wanaojishulisha na mziki waangalie kipaji cha huyu chipukizi Diamond wa kwenye pantony.
Attachments
Last edited: