Burkina Faso: Magaidi wenye silaha waua watu 138

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
156
500
Wapiganaji wenye silaha wanaodhaniwa kuwa wa Jihadi wamewaua takriban watu 138 kaskazini mwa Burkina Faso, katika shambulio linalotajwa kuwa baya zaidi kushuhudiwa tangu mwaka 2015.

Rais wa taifa hilo, Roch Marc Christian Kabore amelaani shambulio hilo akiliita la kishenzi na lililofanywa kwa woga, akiwataka wananchi wa Burkina Faso kusimama imara na kutotishwa na magaidi hao. Pamoja na hayo, Rais Kabore ametangaza siku tatu za maombolezo zinazoisha siku ya Jumatatu saa 5.59 usiku.

Magaidi hao waliwaua watu, kuchoma nyumba na soko katika kijiji cha Solhan, wakishambulia kwanza Kikosi cha Kujitolea Kulinda Nchi (VPD) kinachopambana na ugaidi na kinachoungwa mkono na jeshi la nchi hiyo, kabla ya kuvamia makazi ya watu na kufanya mauaji.

Serikali imetoa tahadhari kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka.

Burkina Faso imekumbwa na mashambulio ya makundi ya wapiganaji wenye silaha walio na mafungamano na Makundi ya Kigaidi ya Al Qaeda na Islamic State (IS) tangu mwaka 2015. Takriban watu 1,400 wamefariki huku mamilioni wakiyakimbia makazi yao.

Chanzo: AFP

1622978904781.png
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
8,174
2,000
Ni mawakala wa shetani 😈 hao, wanajifanya kuwafukuzia mabikra 72 wa kusadikika.
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
61,976
2,000
Hawa watu walitulia kwa muda mrefu sana...

Pole yao sana wafiwa wote...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom