Burkina Faso:Jeshi lachukua mamlaka ya Nchi

mzenjiboy

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
907
382
Habari za hivi punde kutoka CNN jeshi la nchi hiyo limeshika uongozi wa nchi.

Jeshi limevunja serikali pamoja na bunge.

Iyeleweke mzizi wa matatizo haya ni kwamba rais aliyeko madarakani bado hajashiba madaraka juu ya kuwa yupo kwa miaka 27 na anataka katiba irekebishwe ili aweze kugombea tena.

To hell viongozi wa Afrika wamejigeuza Masultani hawashibi madaraka kama Mugabe.

141030185907_sp_burkinafaso3_624x351_afp.jpg

Bunge la Burkina Faso limetekezwa moto


_78640417_08abf538-8efc-46b9-8896-bdd7d9abeddc.jpg

Amiri jeshi mkuu wa jeshi la Burkina Faso Jenerali Honore Traore ametangaza kuvunjwa kwa serikali na bunge la taifa.

Jenerali Traore hata hivyo hakutangaza ni nani atakayechukua uongozi wa taifa hilo.
Jenerali-Honore-Traore.jpg

Honore Traore

Jenerali Traore aliwaambia waandishi wa habari kuwa kutaundwa serikali ya mpito baada ya kufanyika mazungumzo baina ya wanasiasa wa upinzani na kiongozi Bwana Campaore.

Jenerali Traore alikuwa akiwahutubia waandishi wa habari baada ya kushuhudia fuzo la maandamano katika mji mkuu wa Ouagadougou.
141030185338_sp_burkinafaso2_624x351_afp.jpg

Mmoja wa wabunge nchini Burkina Faso akitorokea kuokoa maisha yake.


Waandamanaji walivamia majengo ya bunge na majumba ya wafuasi wa rais Blaise Compaore wakipinga azimio lake la kutaka kubadilisha katiba ya taifa ilikumruhusu kuwania kipindi kingine cha uongozi baada ya kutawala kwa zaidi ya miaka 27.

Awali Waandamanaji waliteketeza majengo ya Bunge mjini Ougadougou, na kuwafurusha wabunge .

Runinga ya taifa ililazimika kusitisha matangazo baada ya waandamanaji kuvamia shirika la utangazaji.
Waandamanaji kisha wameelekea Ikulu ya Rais na wanajeshi wamekua wakiwafyatulia risasi.

Vilevile baraza la jiji pamoja na makao makuu ya chama tawala yameteketezwa moto.
Umati mkubwa wa watu umeonekana ukielekea ikulu ya Rais huku uwanja wa ndege ukifungwa.

Rais Blaise Compaore ameomba utulivu ,katika ujume aliotumwa kwa Twitter.

Wabunge wamelazimika kuahirisha kura hiyo ya kubadilisha katiba kumkubalia Compaore kuwania tena Urais mwaka ujao.
141030110850_burkina_faso_624x351_afp.jpg

Uharibifu katika majengo ya serikali Ougadougou


Watu watano wameuawa katika maandamanao hayo ambayo yametajwa kuwa mabaya zaidi kukumba utawala wa Blaise Compaore.

Awali wanajeshi waliwafyatulia risasi waandamanaji waliovamia majengo ya bunge.

Compaore alitwaa madaraka kupitia mapinduzi mwaka wa 1987.
Amekua akishinda uchaguzi lakini kura hio hukumbwa na utata.
Ufaransa na muungano wa Ulaya zimemuomba Rais Compaore kutobadilisha katiba ili kuwania tena.Mia

Chanzo:BBC
 
Habari za hivi punde kutoka CNN jeshi la nchi hiyo limeshika uongozi wa nchi.

Jeshi limevunja serikali pamoja na bunge.

Iyeleweke mzizi wa matatizo haya ni kwamba rais aliyeko madarakani bado hajashiba madaraka juu ya kuwa yupo kwa miaka 27 na anataka katiba irekebishwe ili aweze kugombea tena.

To hell viongozi wa Afrika wamejigeuza Masultani hawashibi madaraka kama Mugabe.

na mengine yako busy kulisisha watoto wao ubunge, urais mfano waziri wa ulinzi anvyobebwa na nafasi zote nzuri humu nchini
 
Ukiona mwenziyo ananyolewa, wewe anza kutia maji. Bado ccm na polisi wao. Waendelee kuleta fuja nchini kwa urafi wa madaraka as if Tzania ni ya ccm. Mtakiona cha moto.

Wehu
 
Ukiona mwenziyo ananyolewa, wewe anza kutia maji. Bado ccm na polisi wao. Waendelee kuleta fuja nchini kwa urafi wa madaraka as if Tzania ni ya ccm. Mtakiona cha moto.

Wehu

ccm na serikali si wanawaona watz mambwigaaa ngja siku yao ifike
 
Duh bonge la coincidence, ni jana tu nimetazama documentary kuhusu Thomas Sankara (Thomas Sankara: The Upright Man)
 
Back
Top Bottom