Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,910
- 30,253
- Thread starter
- #61
Mdukuzi,Lengo la nyerere ilikuwa ni kuleta sura ya kitaifa kwenye mambo mengi ndio maana hata shule za kanisa alizitaifisha japo ye mkatoliki, machifu akawafuta japo ye mtoto wa chifu,kumuelewa nyerere haijawahi kuwa rahisi
Sijipigii zumari langu mwenyewe.
Mimi katika kitabu cha Abdul Sykes nimemtafiti Nyerere na kumsoma ndani ya Nyaraka za Sykes na kusoma kila kitabu na kila makala yaliyoandikwa kuhusu yeye na nimesoma vitabu vyake vyote alivyoandika.
Ukiacha haya nimezungumza na watu wengi waliomjua Nyerere.
Ukisoma kitabu cha Abdul Sykes utaanza Dar es Salaam kama ilivyokuwa 1900 ukifika 1952 ndipo utamkuta Nyerere.
Kuanzia hapo utamsoma Nyerere na wale aliokuwanao katika TANU hadi uhuru unapatikana 1961.
Kumuelewa Nyerere kunaweza kuwa shida kwa wengine lakini si kwangu.
Namfahamu vizuri kabisa hadi aina ya sigara aliyokuwa akivuta.
Nilihojiwa na Prof. Issa Shivji wakati wanaandika kitabu cha maisha ya Nyerere na waliniambia kuwa katika watu wanaoijua vyema historia ya Nyerere mimi naongoza.
Kitabu kilipochapwa nikakuta wameisifia Maktaba yangu kuwa ni kati ya tatu zilizo bora walizoziona katika utafiti wao.
Doa kubwa katika historia ya Nyerere ni kukosekana ukweli wa historia yake kama ilivyoandikwa wakati wa uhai wake na yeye kuridhia hadi pale nilipoandika historia ya Abdul Sykes.
Shule za Wakatoliki zilitaifishwa lakini Waislam waliendelea kubanwa katika elimu.
Bahati mbaya sana kuwa wewe unauleta mjadala huu leo.
Huu mjadala umezungumzwa miaka mingi nyuma.
Ni tatizo linalofahamika vyema.