Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,370
- 39,186

It is with sadness, I found about the passing of Fr. Joseph Bill, a friend and confidant for many years back. Nilimfahamu kwa karibu na kwake nilijifunza mengi.
Baadhi ya jinsi nilivyo sasa ni matokeo ya maongozi ya mtumishi huyu wa Mungu ambaye kwa hakika ameyagusa maisha ya watu wengi hasa katika eneo letu la Afrika ya Mashariki na nje.
Ni pigo kubwa kwangu, na kwa wengi ambao tulimuita rafiki na siyo padre tu au mhubiri, lakini mtu ambaye tulimuona, kuzungumza naye, kucheka, na kula pamoja naye nje ya altare au kwenye "Popular missions".
Alifariki siku ya 14 March 2008 na kuzikwa jana, ambayo kwa wakatoliki ni siku Kuu ya Mt. Joseph (wajina wake).
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.
Unaweza kujifunza mengi kuhusu Fr. Bill (kama wengi tulivyozoea kumuita) hapa: http://frbillusa.net/news.html na kama uliwahi kumfahamu unaweza kutia sahihi kitabu cha maombolezo hapa: CELEBRATRE FR. BILL'S LIFE
It has been a shocking day for me but also a day that I'm eternally grateful to have known this gifted priest of the Catholic Church.
Nawaombea ndugu jamaa, na marafiki wote faraja wakati huu.
M. M.